Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye Ualbino Tanzania (TAS) Bw. Nemes Temba (katikati) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (h...
Mwenyekiti
wa Chama cha Watu wenye Ualbino Tanzania (TAS) Bw. Nemes Temba
(katikati) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)
wakati akielezea maadhimisho ya siku ya kimataifa ya uelewa juu ya
ualbino mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Mwenyekiti wa
chama hicho mkoa wa Dar es Salaam Bw.Gabriel Aluga na kushoto ni Afisa
Mawasiliano na Habari wa chama hicho Bw. Josephat Torner.
Afisa
Mawasiliano na Habari wa Chama cha Watu wenye Ualbino Tanzania (TAS)
Bw. Josephat Torner (katikati) akifafanua jambokwa waandishi wa habari
(hawapo pichani) wakati akielezea maadhimisho ya siku ya kimataifa ya
uelewa juu ya ualbino mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni
Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Bw. Nemes Temba na kushoto Mwekahazina
wa chama hicho Bw. Abdulah Omar.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye
Ualbino Tanzania (TAS) Bw. Nemes Temba (mwenye koto jeusi) wakati
akielezea maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu wa ngozi mapema hii
leo jijini Dar es Salaam. Picha zote na Eliphace Marwa
Na Husna Said & Nuru Juma- MAELEZO
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya
uelewa juu ya ualbino yatakayofanyika Juni 13 mwaka huu katika uwanja wa
Jamhuri mjini Dodoma.
Hayo
yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Chama cha watu
wenye Ualbino Tanzania Nemes Colman Temba alipokutana na waandishi wa
habari.
Temba
alisema maadhimisho ya mwaka huu yanalenga kuibua mijadala na tafakuri
kwa wadau juu ya ukusanyaji endelevu wa takwimu,uchambuzi na upatikanaji
wa watu wenye Ualbino kwa wakati ili Serikali iweze kuwasajili,
kuwahudumia na kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wa ngozi wanakuwa
salama.
“Bila
ya utaratibu mzuri wa upatikanaji wa Takwimu Serikali haitaweza kupanga
vyema juu ya ustawi wa watu wenye ualbino, hivyo maadhimisho ya mwaka
huu yataibua mjadala wa umuhimu wa upatikanaji wa takwimu sahihi kutoka
ofisi ya Taifa ya takwimu kwaajili ya kusaidia katika mipango ya
maendeleo ya watu wenye ualbino”,alisema Temba.
Aidha
alisema Ofisi ya Taifa ya Takwimu katika sensa ya watu na makazi ya
mwaka 2012 iliyojumuisha takwimu za watu wenye ualbino ilisaidia kubaini
idadi ya watu hao ambapo walikuwa 16,376 wakiwemo Wanaume 7,620 na
Wanawake 8,756.
Mwenyekiti
huyo alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya Mh.Dkt. John Pombe
Magufuli kwa kusikiliza na kutekeleza ombi la masuala ya watu wenye
ulemavu kuhamishiwa ofisi ya Waziri Mkuu kwani lilikuwa ombi la muda
mrefu kwaajili ya ustawi wa watu wenye ualbino na wenye ulemavu kwa
ujumla.
Kwa
upande wake afisa habari na uhusiano wa wa chama hicho, Josephat Torner
alisema kuwa, mauaji dhidi ya watu wenye ualbino yamepungua kwa kiasi
kikbwa kulingana na hapo awali na mapambano dhidi ya vitendo hivyo bado
yanaendelea licha ya ukimya uliokuwepo kwa sasa.
Maadhimisho
hayo yenye kauli mbiu Takwimu na Tafiti kwa Ustawi wa Watu Wenye
Ualbino yatahudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo wadau toka Sweden,
Uholanzi, Marekani, Canada, Uingereza, Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Congo na Mataifa mengine.
Siku
hiyo ya kimataifa ya uelewa juu ya Ualbino itatanguliwa na shughuli
mbalimbali ikiwemo hamasa kupitia vyombo vya habari,uendeshaji wa
kliniki za ngozi kwa maalbino pamoja na utoaji wa msaada wa
kisheria,midahalo na makongamano na ukusanyaji wa takwimu za watu wenye
ualbino.
COMMENTS