F WAETHIOPIA ZAIDI YA NANE WAKUTWA WAMEFARIKI PORINI KATIKA KIJIJI CHA AMANI MAKOLO MKOANI RUVUMA | RobertOkanda

Monday, May 15, 2017

WAETHIOPIA ZAIDI YA NANE WAKUTWA WAMEFARIKI PORINI KATIKA KIJIJI CHA AMANI MAKOLO MKOANI RUVUMA


Ditha Nyoni - RUVUMA

Raia nane kutoka nchi ya Ethiopia wamekutwa wamefariki katika kijiji cha Amani makolo taarafa ya kingonsera wilayani mbinga mkoani wa ruvuma huku wengine 25 wakiwa hai wanashikiriwa na jeshi la polisi.

Habari kutoka jeshi la polisi mkoa wa ruvuma kupitia kaimu kamanda wa polisi ACP Dismas Kisusi zinasema raia hao wa Ethiopia walikuwa wanasafirishwa kwenda nchi ya Afrika ya Kusini kupitia Upande wa Malawi mwa katika ziwa Nyasa.

Vifo vya Waithiopia hao vinatokana na kubebwa kwenye kontena la lori wakitokea Namanga, Arusha hivyo kutokana na hali mbaya ya hewa hali zao zilianza kubadilika na kupelekea kufariki. Huku miili ya marehemu hao ikiwa imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya Mbinga.
Jeshi la polisi mkoa wa Ruvuma kwa kushirikiana na jeshi la uhamiaji linaendelea na uchunguzi kubaini walioleta miili ya marehemu na wale wasiliokamatwa hatua za kisheria zitafuatwa.

0 comments:

Post a Comment