Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Mtandao wa Mashirika yanayopinga ndoa za utotoni wameitaka serikali kuweka mfumo madhubuti ut...
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Mtandao
wa Mashirika yanayopinga ndoa za utotoni wameitaka serikali kuweka
mfumo madhubuti utakaowawezesha wanafuzni wa kike kuendelea kufurahia
haki yao ya kupata elimu bora mara baada ya kujifungua.
Akitoa
tamko hilo Mwenyekiti wa mtandao huo, Valerian Msoka amesema Serikali, wabunge na wadau wengine kujikita katika kupambana na changamoto
zinazopelekea mimba za utotoni ikiwemo ubovu wa miundombinu ya elimu
kukosekana kwa elimu bora ya afya ya uzazi.
“Mtandao
wa kupinga ndoa za utotoni unaamini kuwa Tanzania ina uongozi na
wawakilishi wanaojali maslahi ya wananchi ambapo watoto wa kike ni
miongoni mwa hao. Na ni kwa sababu hiyo mtandao una imani kuwa sauti
yao itsikilizwa kwani wasichana hawa wanaopoteza masomo kutokana na
mimba ni sehemu ya nguvu kazi muhimu ya msingi na yenye tija kufikia
Tanzania ya Viwanda” amesema Msoka.
Msoka
amemaliza kwa kusema kuwa utafiti wa kitaifa kuhusu Vichocheo na madhara
ya ndoa za utotoni nchini Tanzania uliofanywa mwaka 2016 umebaini kuwa
wasichana wana uelewa mdogo juu ya afya ya uzazi.
Mwenyekiti wa Mtandao wa kutetea wadada wadogo, Valerian Msoka
Mwenyekiti wa Tamwa , Eda Sanga akizungumza juu ya kuwaomba wabunge kutunga sheria kuwasaidia watoto wanaopata mimba mashuleni
Mkurugenzi wa Tawla nchini ,Tike Mwambipile akizungumza wakati wa kutoa tamko hilo .
Mkurugenzi wa Shirika la Watoto, Koshuma Mtengeti akizungumza juu ya tamko hilo
Waandishi wa habari wakifatilia mkutano huo
Baadhi ya wanachama wa tasisi mbalimbali zisizo za kiserikali wakiwa katika mkutano huo
Waandishi na wana harakati wakisikiliza tamko hilo kwa makini
COMMENTS