Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Prof Alexander Songorwa akitoa mada ya kwanini watanzania tuhifadhi uoto wa asili na wanyamap...
Mkurugenzi
wa Idara ya Wanyamapori, Prof Alexander Songorwa akitoa mada ya kwanini
watanzania tuhifadhi uoto wa asili na wanyamapori wakati wa semina
kuhusu umuhimu wa uhifadhi wa maliasili, malikale na maendeleo ya utalii
nchini iliyoandaliwa na Wizara Maliasili na Utalii kwa Wabunge na
kufanyika jana Bungeni mjini Dodoma. SOURCE: Daily News-Habarileo Blog.
Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa
Wanyamapori Serengeti (TAWIRI), Dk. Robert Fyumagwa akitoa mada katika semina hiyo juu ya athari za muingiliano wa mifugo na Wanyamapori.
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof Dos Santos Silayo akitoa mada juu ya umuhimu wa uhifadhi misitu nchini.
Profesa Dos Santos Silayo,
wakati akiwasilisha mada ya umuhimu wa uhifadhi wa misitu nchini alisema ni
vyema misitu ikatunzwa kwa kuwa ndio utajiri mkubwa kwa watanzania.
Alisema misitu ndio huzalisha vyanzo vya maji,
husababisha mvua, hutumika kama utalii wa ikolojia, hutunza wanyama na ndege
lakini kubwa zaidi husaidia katika kutunza mazingira.
Katibu
Mtendaji wa Shirikisho la Vyama vya Utalii Tanzania (TCC), Richard
Rugimbana akitoa mada yake juu ya maendeleo ya Utalii na Umuhimu wake
katika uchumi wa Tanzania.
Maofisa wa Wizara ya Mali Asili na Utalii wakiwa katika semina hiyo.
Mkurugenzi
wa Idara ya Wanyamapori, Prof Alexander Songorwa akitoa mada ya kwanini Watanzania tuhifadhi uoto wa asili na wanyamapori.
Profesa Songorwa endapo uoto
wa asili usipohifadhiwa kuna hatari ya kupungua kwa maeneo yaliyohifadhi hewa
ya oxygen.
Changamoto nyingine za kutohifadhi uoto wa asili ni
kufa kwa mfumo wa ikolojia, wanyamapori na vivutio vya kitalii kuharibika na
kupungua na hata kutoweka. BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI.
COMMENTS