VODACOM YAONGEZA BAJETI YA ZAWADI LIGI KUU KWA MWAKA HUU

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt, Harrison Mwakyembe (kushoto) akikaribishwa na Mkuu wa kitengo cha Masoko na Ma...


Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt, Harrison Mwakyembe (kushoto) akikaribishwa na Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC, Nandi Mwiyombella alipowasili kwenye hafla ya utoaji wa tuzo za washindi wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, iliyoandaliwa na wadhamni hao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam jana.
 
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt, Harrison Mwakyembe akimsikiliza jambo kwa makini Mkurugenzi wa biashara wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi (katikati) wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo za washindi wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, iliyoandaliwa na kampuni hiyo ikiwa ndiyo wadhamini wakuu wa ligi na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam jana, kulia ni Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC, Nandi Mwiyombella.
Mkurugenzi wa biashara wa Vodacom Tanzania,Hisham Hendi,akiongea wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo za washindi mbalimbali wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, iliyoandaliwa na kampuni hiyo ikiwa ndiyo wadhamini wakuu wa ligi na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam jana.
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt, Harrison Mwakyembe, akiongea na wadau mbalimbali waliohudhuria hafla ya utoaji wa tuzo mbalimbali za washindi wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, iliyoandaliwa na wadhamini wakuu wa ligi Vodacom Tanzania na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam.
 
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt, Harrison Mwakyembe, akipewa hongera na Mkurugenzi wa biashara wa Vodacom Tanzania,Hisham Hendi baada ya kuongea na wadau walioshiriki katika hafla ya utoaji tuzo mbalimbali za washindi wa Ligi kuu bara, iliyoandaliwa na wadhamini wakuu wa ligi Vodacom Tanzania na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam, katikati ni Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC, Nandi Mwiyombella.
 
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC, Nandi Mwiyombella akimkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 84/- Katibu mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa baada ya timu yao kuibika mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2016/2017 wakati wa halfa ya utoaji tuzo mbalimbali jana katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa masoko wa Vodacom Tanzania, Ashutosh Tiwary (kushoto) akimkabidhi tuzo ya heshima, Kitwana Manara wakati wa halfa ya utoaji tuzo mbalimbali za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara iliyoandaliwa na wadhamini wakuu wa ligi na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt, Harrison Mwakyembe (katikati) Mkurugenzi mkuu wa biashara wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi(kushoto) wakimkabidhi tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2016/2017 baba mzazi wa mchezaji wa Simba, Mohamed Hussein ”Tshabalala” baada ya mtoto wake kuchukua tuzo hiyo hapo jana wakati wa halfa ya utoaji tuzo mbalimbali za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara iliyoandaliwa na wadhamini wakuu wa ligi na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam.
 
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt, Harrison Mwakyembe (katikati) akimshuhudia Mkurugenzi mkuu wa biashara wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi(kushoto)akimpongeza baba mzazi wa mchezaji wa Simba, Mohamed Hussein ”Tshabalala” baada ya mtoto wake kuibuka mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2016/2017 wakati wa halfa ya utoaji tuzo mbalimbali za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara iliyoandaliwa na wadhamini wakuu wa ligi na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam.
Wadhamini wakuu wa Ligi ya Mpira wa miguu Tanzania Bara kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC, jana ilitoa zawadi zenye thamani ya shilingi 232,974,660 kwa washindi mbali mbali wa ligi.
Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji zawadi iliyofanyika jijini Dar es Salaama jana, Mkurugenzi Mkuu wa biashara na Masoko wa kampuni hiyo, Hisham Hendi alisema Vodacom imeongeza kiasi cha fedha zaidi mwaka huu.
Mwaka jana tulitoa shilingi 219,502,500. Kwa ajili ya zawadi lakini mwaka huu fedha hizi zimeongezeka na kufikia shilingi 232,974,660,” alisema
Hendi alisema, Vodacom Tanzania inavutiwa na jinsi ambavyo umaarufu wa ligi unavyokuwa ukiongezeka siku hadi siku huku ukiwavutia na kuwaburudisha Watanzania walio wengi wanaoishi mijini na vijijini bila kujali kama timu za maeneo wanayoishi zinashiriki ligi hii.
“Pamoja na umaarufu wa ligi hii kuongezeka na mafanikio yanayozidi kupatikana, sisi kama wadhamini tunajua kuwa bado kuna changamoto mbalimbali za kuboresha ligi yetu iwe na viwango vya hali ya juu na ili kuondokana na changamoto hizi unahitajika ushirikiano mkubwa baina ya wadau wote wa mchezo wa soka nchini japo mabadiliko hayawezi kuja kwa siku moja,” alieleza.

Mkurugenzi huyo alitoa wito kwa wadau wote kushiriki kubuni mikakati ya kuboresha ligi hii na ikiwezekana wajitokeze wafadhili wengine zaidi ili wachezaji wazidi kunufaika.
“Kama sote tunavyoelewa hivi sasa michezo sio burudani tu kama ilivyokuwa miaka ya zamani bali inasaidia kupunguza tatizo la ajira na kuinua uchumi wa nchi kwani wanamichezo wakiwezeshwa wanaweza kupitia mapato yao kuboresha pato la taifa kama tunavyosikia katika nchi za wenzetu ambako wachezaji na wasanii ni kundi la mamilionea wanaotambulika na hapa tukiamua yote haya yanawezekana na dalili zimeanza kuonekana.
Alisema Vodacom itaendelea kuunga mkono na kufadhili mchezo wa soka na michezo mingine kwa kuwa inaamini wanamichezo ni mabalozi wazuri katika kutangaza Taifa na pia michezo huchangia kuibua na kukuza vipaji vya wanamichezo.
“Kwa niaba ya Vodacom Tanzania naipongeza timu bingwa ya ligi ya Soka ya Vodacom msimu uliomalizika Yanga African bila kusahau timu zote zilizofanya vizuri na wote waliokabidhiwa zawadi zao leo.

Ni matumaini yetu maandalizi ya msimu ujao wa ligi yamekwishaanza kuandaliwa vizuri na wadau wote tutashirikiana tena kuhakikisha ubora wa ligi unazidi kuwa bora zaidi,” alisema Hisham.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: VODACOM YAONGEZA BAJETI YA ZAWADI LIGI KUU KWA MWAKA HUU
VODACOM YAONGEZA BAJETI YA ZAWADI LIGI KUU KWA MWAKA HUU
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiiuuVJAJIZYpSebPlQTacDjfzo2uW6LkUlolYfm7LvNIM_qB-yBmU1sXwqF7HSJLF4btRLYe28Ird1TOv0YfDbc3O4RzNzb4U5NevUtWEjtfAS50mi1L15FJKqJEYwkI37eQgIhta5IWaL/s640/001.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiiuuVJAJIZYpSebPlQTacDjfzo2uW6LkUlolYfm7LvNIM_qB-yBmU1sXwqF7HSJLF4btRLYe28Ird1TOv0YfDbc3O4RzNzb4U5NevUtWEjtfAS50mi1L15FJKqJEYwkI37eQgIhta5IWaL/s72-c/001.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/vodacom-yaongeza-bajeti-ya-zawadi-ligi.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/vodacom-yaongeza-bajeti-ya-zawadi-ligi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy