UVCCM WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA HATUA ALIZO CHUKUA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Umoja wa  Vijana wa Chama  Cha Mapinduzi (UVCMM), umem pongeza Mwenyekiti wa CCM na Rais wa ...


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Umoja wa  Vijana wa Chama  Cha Mapinduzi (UVCMM), umempongeza Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli kwa kuonesha Uzalendo mkubwa alionao kwa nchi yake, baada ya kuchukua maamuzi yenye maslahi ya nchi  katika sakata la zima la Makinikia.

Hayo yamesemwa leo na Kaimu Katibu mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC)  alipokuwa akitoa salamu za pongezi za Vijana wote katika  ukumbi wa CCM Vijana Kinondoni .

Shaka amesema Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi unampongeza Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa  na uzalendo wa hali ya juu alionao kwa Taifa mara baada ya kuchukua maamuzi yenye masalhi ya nchi katika swala zima la Makinikia.

Amesema Umoja wa Vijana wa CCM unaunga mkono maamuzi yote yaliyopitishwa au kutolewa na Rais Dk John Magufuli mara baada ya kupokea ripoti ya Tume ya Uchunguzi 

“Umoja wa Vijana wa CCM hatuko tayari na hatutakubali kushuhudia tena Tanzania  ikirejea katika zama ya kiza kinene cha ukwapuaji mali,  ulaji, kufilisi mashirika ya umma au wizi wa mali za umma.tunaishauri serikali yetu iendelee na mikakati yake ya kuhakikisha ukwapuaji, ubabaishaji, wizi na ufisadi wa mali za serikali vinavikomeshwa mara moja 

      Amesema kuwa Umoja wa Vijana wa CCM unaiomba kwa dhati Serikali yetu ianze kuipitia upya mikataba yote ya madini ili kubaini kama ni yenye manufaa na maslahi mapana  kwa umma na kumuomba Rais Dk John Magufuli kuwaweka pembeni wasaidizi wake wote ambao bado wanaonekana kuwa na kigugumizi katika kuwatumikia wananchi huku baadhi yao wakiona muhali kupambana na ufisadi. 

       Ameweka wazi kuwa UVCCM Inasisitiza kuwa Watendaji wote waliokuwa na dhamana na ambao wamehusika kwa namna moja au nyingine kupoteza mapato na kulitia hasara Taifa, hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao haraka . 

Amesema wao wanaishauri Serikali kuendelea kuwabaini na kuwachukulia hatua Viongozi na watendaji wa serikali ambao watabainika kumiliki mali, utajiri na vitega uchumi ambavyo havitokani na mapato yasiolingana na vipato vyao wataifishwe kama ilivyofanyika mwaka 1967 baada ya kutangazwa Azimio la Arusha .

“Vijana wote tunaishauri serikali yetu isikubali na isiafiki  mali za umma zitumike kwa maslahi binafsi badala yake kila miliki ya serikali na mali ya umma ifahamike  kuwa kila mwananchi ana haki kufaidika nayo ambayo ni sehemu ya matunda ya Uhuru na Mapinduzi matukufu ya Zanzibar”.

Alimaliza kwa kusema kuwa  Umoja wa Vijana wa CCM unawataka wana CCM na Watanzania wote kwa ujumla kuendelea kumuunga mkono Mheshimiwa Rais na Serikali yake katika mapambano dhidi ya vikundi vya rushwa, ufisadi na uzembe kwa baadhi ya watendaji  ili kuleta maendeleo endelevu katika taifa letu.
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akizungumza na Vijana wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa mkutano wa kumpongeza Rais John Pombe Magufuli kwa maamuzi aliyochukua.
 Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akiwa na Viongozi wa ngazi za juu wa umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM)
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akicheza muziki na baadhi ya wanachama wa UVCCM
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka (MNEC) Akiwa amebebwa juu  na Vijana wa CCM
Sehemu ya Vijana wa Hamasa wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi  wakifurahi juu ya mamuzi yaliyochukuliwa na Rais John Pombe Mgufuli
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akiwasili  katika ukumbi wa Umoja wa Vijana Kinondoni
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akiwasili katika Ukumbi wa Umoja wa Vijana Kinondoni
 smsehemu ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)  wakiwa na furaha kubwa sana
 ehemu ya Vijana wa Hamasa wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi   wakifurahi juu ya mamuzi yaliyochukuliwa na Rais John Pombe Mgufuli
 Mabango ya kumpongeza Rais Magufuli

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: UVCCM WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA HATUA ALIZO CHUKUA
UVCCM WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA HATUA ALIZO CHUKUA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgZAG1jW6QHvz1W2a0jGpn-FG-Si7v8_zqexOkpqujgKl5AUqrM2xVs2nQuu1jmI_P86SWhar5rQnPem5xtyoNChJt_wAjZpeAaUzTLshdMwgPytkNWsDKAyKzFshyBRdk5Dqk9MrLvB5o/s640/_MG_0071.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgZAG1jW6QHvz1W2a0jGpn-FG-Si7v8_zqexOkpqujgKl5AUqrM2xVs2nQuu1jmI_P86SWhar5rQnPem5xtyoNChJt_wAjZpeAaUzTLshdMwgPytkNWsDKAyKzFshyBRdk5Dqk9MrLvB5o/s72-c/_MG_0071.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/uvccm-wampongeza-rais-magufuli-kwa.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/uvccm-wampongeza-rais-magufuli-kwa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy