UMISSETA MKOA WA DAR ES SALAAM YAPAMBA MOTO

Kaimu Katibu Tawala upande wa Uchumi na Uzalisha Mkoa wa Dar es salaam Ndg Edward Otieno akizungumza wakati wa ufunguzi wa  UMISSET...


Kaimu Katibu Tawala upande wa Uchumi na Uzalisha Mkoa wa Dar es salaam Ndg Edward Otieno akizungumza wakati wa ufunguzi wa  UMISSETA Mkoa wa Dar es salaam Leo Mei 28, 2017 katika Uwanja wa Uhuru.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akiwasalimu wanamichezo wakati wa ufunguzi wa UMISSETA Mkoa wa Dar es salaam Leo Mei 28, 2017 katika Uwanja wa Uhuru.
Baadhi ya wanamichezo kutoka Manispaa za Mkoa wa Dar es salaam wakifatilia mchezo kati ya Ilala na Ubungo wakati wa ufunguzi wa UMISSETA Mkoa wa Dar es salaam Leo Mei 28, 2017 katika Uwanja wa Uhuru.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisalimiana na mchezaji wa Mpira wa Miguu Manispaa  ya Ubungo wakati wa ufunguzi wa UMISSETA Mkoa wa Dar es salaam Leo Mei 28, 2017 katika Uwanja wa Uhuru.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kushoto), Kaimu Katibu Tawala upande wa Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Dar es salaam Ndg Edward Otieno (Katikati) na Afisa Elimu Mkoa wa Dar es salaam Khamisi Lissu wakati wa ufunguzi wa UMISSETA Mkoa wa Dar es salaam Leo Mei 28, 2017 katika Uwanja Uhuru.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akitoa hamasa kwa timu ya UMISSETA Wilaya ya Ubungo wakati wa ufunguzi wa  UMISSETA Mkoa wa Dar es salaam Leo Mei 28, 2017 katika Uwanja wa Uhuru.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akiimba wimbo maalumu wa Michezo ya UMISSETA wakati wa ufunguzi wa  UMISSETA Mkoa wa Dar es salaam Leo Mei 28, 2017 katika Uwanja wa Uhuru.
Na Mathias Canal, Dar es salaam
Maandalizi ya ngazi ya Mkoa wa Dar es salaam Kwa Mashindano ya Umoja wa Michezo Shule za Sekondari Tanzania yamezidi kupamba Moto katika Uwanja wa Uhuru na Uwanja wa Taifa Jjijini Dar es salaam.
Maandalizi hayo kwa ngazi ya Mkoa kwa ajili ya kupata timu ya Mkoa Wa Dar es salaam yameanza  Leo Mei 28, 2017 Kwa kuhusisha Manispaa za Mkoa wa Dar es salaam ikiwemo Manispaa ya Ilala, Temeke, Kinondoni, Kgamboni na Ubungo.
Akizungumza katika ufunguzi wa mashindano hayo Kwa ngazi ya Wilaya za Mkoa wa Dar es salaam Kaimu Katibu Tawala katika upande wa Uchumi na Uzalisha Mkoa wa Dar es salaam Ndg Edward Otieno amewasihi washiriki kutumia weledi wao wa mafunzo waliyoyapata kuhusu michezo na kuonyesha umahiri wao ili kuchaguliwa katika timu ya Mkoa.
Wanafunzi hao ambao wameweka kambi katika Shule ya Sekondari Jitegemee mpaka Mei 31, 2017 wataanza safari ya kuelekea Jijini Mwanza kwa ajili ya mashindano hayo ngazi ya Taifa yanayotaraji kuanza kufanyika katika uwanja wa CCM Kirumba June 6, 2017.
Otieno alisema kuwa vijana hao wanapaswa kutambua kuwa michezo ndio ajira inayolipa zaidi Duniani hivyo wanapaswa kudumisha nidhamu kwa kipindi chote Cha mashindano.
Aliongeza kuwa wanapaswa kutambua kuwa timu zote za Mkoa wa Dar es salaam zitakwenda Mwanza kushindana katika michezo hiyo ngazi ya Taifa na si kushiriki pekee.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo aliyezuru katika Uwanja wa Uhuru kujionea Timu ya Vijana wake kutoka Manispaa ya Ubungo ikichuana vikali na timu ya Manispaa ya Ilala amepongeza juhudi za washiriki wote ambao wameonyesha nidhamu ya Hali ya juu.
"Ukiona vijana Wana nidhamu Kama hivi ni vyena kuwapongeza na kuwatia moyo maana Bado Wana safari ndefu kimichezo na kimaisha" Alisema MD Kayombo
Mkurugenzi Kayombo ametilia msisitizo zaidi kutumia weledi wao ili kurejesha heshima ya michezo katika Manispaa ya Ubungo na Mkoa wa Dar es salaam Kwa ujumla.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: UMISSETA MKOA WA DAR ES SALAAM YAPAMBA MOTO
UMISSETA MKOA WA DAR ES SALAAM YAPAMBA MOTO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi9gYpYdHgXftWWz1NIUqex8u7PlpYICTlgBksP3mj0YGsIddFBC52fk1VL5l6Sa_Pr1DMx6E5hFvVVpheiCzP5HQwiwQIQANTdCzRkTnyBoNBVFYWF6D7O8eoTnA3bXBYyoh4BD1ipstkf/s640/IMG-20170528-WA0101.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi9gYpYdHgXftWWz1NIUqex8u7PlpYICTlgBksP3mj0YGsIddFBC52fk1VL5l6Sa_Pr1DMx6E5hFvVVpheiCzP5HQwiwQIQANTdCzRkTnyBoNBVFYWF6D7O8eoTnA3bXBYyoh4BD1ipstkf/s72-c/IMG-20170528-WA0101.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/umisseta-mkoa-wa-dar-es-salaam-yapamba.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/umisseta-mkoa-wa-dar-es-salaam-yapamba.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy