UHALIFU UNAOVUKA MIPAKA KUJADILIWA ARUSHA

Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Arusha. Mkutano mkuu wa  mwaka wa Shirikisho la wakuu wa Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afr...


Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Arusha.

Mkutano mkuu wa  mwaka wa Shirikisho la wakuu wa Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO) unatarajia kufanyika Jumatano Mei 24, 2017 mkoani Arusha chini ya mwenyekiti wa Shirikisho hilo kwa kipindi hiki ambaye ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu. 

Taarifa iliyotoilewa na Msemaji wa Polisi, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Advera Bulimba imesema mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa na Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba na utahudhuruwiwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi kutoka SADC na wale wa Shirikisho la Polisi wa kimataifa INTERPOL ambapo tayari kamati tendaji za shirikisho hilo zinaendelea na mikutano yake kwa ajili ya maandalizi ya mkutano huo mkuu.

Bulimba alisema katika mkutano huo mambo mbalimbali yatajadiliwa ikiwemo jinsi ya kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka kwa kufanya Operesheni za pamoja katika kubaini na kukabiliana na makosa  mbalimbali yakiwemo  dawa za kulevya, wizi wa magari, usafirishaji haramu wa binadamu na ugaidi.

“Vilevile, mkutano huu utajadili utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa na Wakuu wa Upelelezi wa SARPCCO pamoja na kamati tendaji za sheria, Mafunzo na kamati tendaji ya Jinsia na watoto baada ya mkutano wao uliofanyika mwezi Machi mjini Bagamoyo” Alisema Bulimba.

SARPCCO iliundwa mwaka 1995 kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa Majeshi ya Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu. Shirikisho hilo linaundwa na Nchi kumi na tano ambazo ni Tanzania, Angola, Botswana, Malawi, Lesoto, Mauritius, DRC, Msumbiji, Namibia, Afrika Kusini, Zambia, Zimbabwe, Swaziland, Madagascar na Syshelis.
 Naibu Inspekta jenerali wa polisi, Abdulrahmani Kaniki, akitoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa kamati tendaji za shirikisho la wakuu wa polisi kwa nchi za kusini mwa Afrika, (SARPCCO)  ikiwa ni maandalizi ya mkutano mkuu wa mwaka wa shirikisho hilo unaotarajiwa kufanyika  jumatano tarehe 24/05/2017 mkoani Arusha. 
Baadhi ya wajumbe wa kamati tendaji za shirikisho la wakuu wa polisi kwa nchi za kusini mwa Afrika, (SARPCCO) wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kamati hizo ikiwa ni maandalizi ya mkutano mkuu wa mwaka wa shirikisho hilo unaotarajiwa kufanyika  Jumatano tarehe 24/05/2017 mkoani Arusha. (Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi)

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: UHALIFU UNAOVUKA MIPAKA KUJADILIWA ARUSHA
UHALIFU UNAOVUKA MIPAKA KUJADILIWA ARUSHA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhzuPM90WxgiyHxjST91sH7IAGGn6NWSXKzb03hVr6PpXwySYlaX7eElUmPQCYvh14wWZXGacK5hqTkdrI99D0jc615QOhfnhD278RpM3eVS6tcxM5toecOHwksgSpHjK9wJoIUZcqiGUhK/s640/IMG_9191.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhzuPM90WxgiyHxjST91sH7IAGGn6NWSXKzb03hVr6PpXwySYlaX7eElUmPQCYvh14wWZXGacK5hqTkdrI99D0jc615QOhfnhD278RpM3eVS6tcxM5toecOHwksgSpHjK9wJoIUZcqiGUhK/s72-c/IMG_9191.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/uhalifu-unaovuka-mipaka-kujadiliwa.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/uhalifu-unaovuka-mipaka-kujadiliwa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy