TRUST CARE TANZANIA, TTCL KUWAJENGEA UWEZO WANAFUNZI VYUO VIKUU

Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Injinia Enocent Msasi akizungumza katika mkutano na wanahabari leo kuzung...


Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Injinia Enocent Msasi akizungumza katika mkutano na wanahabari leo kuzungumzia semina ya wanavyuo inayotarajia kufanyika Jumamosi ya tarehe 20/05/2017 katika ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE) kuanzia majira ya saa tatu asubuhi. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Trust Care Tanzania Foundation, Zambert Mbwafu na Ofisa Masoko wa Kampuni ya TTCL, Lulu Kamalamo (kulia) wakiwa katika mkutano huo.

Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Injinia Enocent Msasi akizungumza katika mkutano na wanahabari leo kuzungumzia semina ya wanavyuo inayotarajia kufanyika Jumamosi ya tarehe 20/05/2017 katika ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE) kuanzia majira ya saa tatu asubuhi. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Trust Care Tanzania Foundation, Zambert Mbwafu na Ofisa Masoko wa Kampuni ya TTCL, Lulu Kamalamo (kulia) wakiwa katika mkutano huo.

Kushoto ni Mkurugenzi wa Elimu na Utafiti wa Trust Care Tanzania Foundation, Fadhila Nyoni akifafanua jambo juu ya semina ya wanafunzi wa vyuo vikuu katika mkutano na wanahabari leo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Trust Care Tanzania Foundation, Zambert Mbwafu akifuatilia mazungumzo hayo.
SHIRIKA la Trust Care Tanzania Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wameandaa semina ya kuwajengea uwezo wa kifikra wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali vya jijini Dar es Salaam ikiwa na lengo la kuwabadili wanafunzi kwa ujumla kuwa na mawazo chanya yatakayowawezesha kutumia fursa anuai zinazowazunguka katika jamii mara baada ya masomo yao.
Akizungumzia semina hiyo inayotarajiwa kufanyika Jumamosi ya tarehe 20/05/2017 katika ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE) kuanzia majira ya saa tatu asubuhi, Mkurugenzi Mtendaji wa Trust Care Tanzania Foundation, Zambert Mbwafu alisema semina hiyo ni maalum kwa wanafunzi waliopo vyuoni kwa ajili ya kuwajengea uwezo.
Alizitaja mada ambazo wanafunzi wanatarajia kufundishwa ni pamoja na Umuhimu wa Kujiamini na Kujijengea Uwezo, Uwezo wa Uthubutu, Vipaji na Jinsi ya Kuviendeleza, Maadili na Nidhamu katika Kazi na Ubunifu katika Kufikia Malengo. "Semina inawaandaa vijana waliopo na ambao wanatarajia kumaliza elimu yao ya juu hivi karibuni kupata elimu na ujuzi utakaowasaidia wakiwa shule na baada ya kumaliza masomo yao ili waweze kwenda sambamba na mahitaji ya ulimwengu wa sasa..." alisema Bw. Mbwafu.
Akifafanua zaidi Mkurugenzi, Zambert Mbwafu, alivitaja vyuo vitakavyoshiriki katika semina hiyo; ni pamoja IFM, CBE, DIT, DUCE, TIA, UDSM, MUHAS, CHUO CHA DIPLOMASIA, KIU, CHUO CHA USTAWI WA JAMII NA CHUO KIKUU CHA TUMAINI.
Kwa upande wa wadhamini wakuu wa semina hiyo Kampuni ya TTCL, Injinia Enocent Msasi Mkurugenzi wa Biashara TTCL alisema kampuni hiyo inaunga mkono kampuni ya Trust Care Tanzania kwa dhumuni lake la kuisaidia jamii katika maeneo mbalimbali, ikiwemo sekta za kiafya, kielimu na kijamii. Aliongeza kuwa lengo hilo linashabihiana na lengo la TTCL kuhakikisha inakuwa na jamii bora zaidi kiteknolojia, kielimu, kiafya na kimaendeleo kwa ujumla.
"TTCL imedhamini semina hii kwasababu inatoa mchango mkubwa katika kujenga taifa lenye vijana wachapakazi, vijana wenye mtizamo chanya, vijana wenye uwezo wa uthubutu, na kupambana na changamoto mbalimbali za kimaisha, " alisema Msasi na kuongeza kuwa TTCL kupitia huduma zake bora za intaneti, sauti na SMS inawaunga mkono vijana mara zote na itakuwa mstari wa mbele kufanikisha juhudi zao za kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
"TTCL kwa miaka mingi tumekuwa tukipokea vijana wanaokuja kufanya mafunzo kwa vitendo kutoka vyuo na taasisi mbalimbali za elimu zinazotoa elimu katika fani tofauti tofauti. Lakini safari hii tumekuja kivingine zaidi, kwa kuja na programu ambayo itasaidia vijana kupata uzoefu baada ya kumaliza masomo yao. Hii itasaidia kuondoa changamoto ya vijana wetu waliomaliza elimu ya juu ambao mara nyingi hupoteza fursa mbalimbali za ajira kwa kukosa sifa ya uzoefu."
Vijana watakao pata fursa ya kufanya kazi na TTCL watajifunza mengi kawa vitendo huku wakiongozwa kwa wataalamu wabobezi katika fani mbalimbali. Tunaamini watakapomaliza programu hiyo vijana hao watapata fursa kupata ajira kwenye taasisi na makampuni mbalimbali, au kujiajiri wenyewe," alisisitiza Enocent Msasi akizungumza na wanahabari leo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Trust Care Tanzania Foundation, Zambert Mbwafu akizungumza katika mkutano na wanahabari leo kuzungumzia semina ya wanafunzi wa vyuo vikuu inayotarajia kufanyika Jumamosi ya tarehe 20/05/2017 katika ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE) kuanzia majira ya saa tatu asubuhi. Kulia ni Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Injinia Enocent Msasi akiwa katika mkutano huo.

Baadhi ya wanahabari wakiwa katika mkutano huo.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TRUST CARE TANZANIA, TTCL KUWAJENGEA UWEZO WANAFUNZI VYUO VIKUU
TRUST CARE TANZANIA, TTCL KUWAJENGEA UWEZO WANAFUNZI VYUO VIKUU
https://blogger.googleusercontent.com/img/proxy/AVvXsEisiqfp959_VN5u8Dz6bQmdf5aXKS-Ogwq1peFBXdBk1hctAx9ZB_b7H2Tc07Q6wFVRc4kJEZEWsgJs71TMSrPBrA5ldAMty0r1dPGzI-XUqW2pnLMIzgK_Un-dCNF5ThCeZk2liuNkO4KTQUfLH1X2vbAbHlPdCdpsPpwghe-BLA=s0-d-e1-ft
https://blogger.googleusercontent.com/img/proxy/AVvXsEisiqfp959_VN5u8Dz6bQmdf5aXKS-Ogwq1peFBXdBk1hctAx9ZB_b7H2Tc07Q6wFVRc4kJEZEWsgJs71TMSrPBrA5ldAMty0r1dPGzI-XUqW2pnLMIzgK_Un-dCNF5ThCeZk2liuNkO4KTQUfLH1X2vbAbHlPdCdpsPpwghe-BLA=s72-c-d-e1-ft
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/trust-care-tanzania-ttcl-kuwajengea.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/trust-care-tanzania-ttcl-kuwajengea.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy