Timu ya Azania imeondoka nchini kuelekea Uingereza kwa ajili ya kushiriki mashindano ya Standard Chartered Safari kwenda Anfield yatakay...
Timu
ya Azania imeondoka nchini kuelekea Uingereza kwa ajili ya kushiriki
mashindano ya Standard Chartered Safari kwenda Anfield yatakayofanyika
kwenye uwanja wa klabu ya Liverpool wa Anfield.
Timu
hiyo imeondoka na msafara wa watu 10 ambapo kati yao wachezaji ni saba
ambao ni Shabaka Hamisi, Rajabu Ally, Akhamedy Afifu, Abdalah Khalid,
Thomas Bishanga, Alidi Said na Brayan Dobadi.
Azania
itashiriki mashindano hayo ikiwa ni mabingwa wa kombe la Standard
Chartered Safari kwenda Anfield kwa Afrika Mashariki na Kati na ikiwa
kwenye mashindano hayo itakutana na timu zingine kutoka Botswana,
Nigeria, Hong Kong, Korea, Singapore, India pamoja na Uingereza.
Timu
hiyo itafika Uingereza Mei, 19 wakiwa huko watakutana na timu zingine,
Mei, 20 watatembelea uwanja wa Anfield, Mei, 21 watashuhudia mchezo wa
Liverpool na Middlesbrough na baada ya hapo wataingia uwanjani kwa ajili
ya mashindano na watarejea nchini Mei, 22.
COMMENTS