TIMU YA AZANIA KUIWAKILISHA TANZANIA KWENYE MASHINDANO YA STANDARD CHARTERED UINGEREZA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe ameikabidhi bendera timu ya Azania ambayo inaelekea nchini Uinger...

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe ameikabidhi bendera timu ya Azania ambayo inaelekea nchini Uingereza kushiriki mashindano ya Standard Chartered Safari kwenda Anfield. Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi bendera pamoja na hati za kusafiria, Waziri Mwakyembe alisema ni fursa ya kipekee ambayo Tanzania imeipata kushiriki mashindano kama hayo na ni muda sasa dunia kujua kuwa Tanzania kuna vipaji vya soka hivyo wahakikishe wanarudi nchini na kikombe. “Mtuwakilishe vyema huko muendako ni muda sasa wa dunia kuwa Tanzania tuna uwezo wa kisoka, kila mmoja acheze vizuri na kuonyesha uwezo wake, tunaamini mtarudi na kikombe na nawatakia kila la kheri,” alisema Waziri Mwakyembe. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi bendera pamoja na hati za kusafiria kwa timu ya Azania ambayo inaelekea nchini Uingereza kushiriki mashindano ya Standard Chartered Safari kwenda Anfield iliyofanyika katika hoteli ya Southern Sun jijini Dar Es Salaam.[/caption] Nae Mjumbe wa Bodi ya Standard Chartered Tanzania, Ami Mpungwe amesema benki yao inajivunia kupata wawaklishi kutoka Tanzania na wamesimamia gharama zote za safari kwa muda wote ambao timu itakuwa Uingereza na ni matumaini yao kuwa timu hiyo ya Azania itarejea nchini na kikombe. “Tupo hapa kuiaga timu ya Azania ambao ni mabingwa wa Tanzania na Afrika Mashariki wa kombe la Standard Chartered Safari kwenda Anfield, tunajivunia timu hii sababu imetuletea heshima kubwa, tunawaombe ushindi mkubwa na tunategemea watakuja na ubingwa,” alisema Mpungwe. Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke akitoa pongezi kwa timu ya Azania kupata nafasi ya kwenda Uingereza wakati wa hafla ya kukabidhi bendera kwa timu hiyo inayokwea pipa kesho 18 Mei. Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe.[/caption] Kwa upande wa Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke aliipongeza timu ya Azania kwa kupata nafasi ya kwenda Uingereza kucheza kwenye moja ya kiwanja maarufu cha Anfield lakini pia kuipongeza benki ya Standard Chartered kwa kufikisha miaka 100 tangu kuanza kutoa huduma nchini. “Hii ndiyo nguvu ya michezo inauwezo wa kuwaunganisha watu pamoja, mnakwenda Uingereza tunaijua ni timu kubwa nawapongeza Azania kwa kupata nafasi, hongereni sana nawatakia kila la kheri najua mtafurahi kwa kipindi ambacho mtakuwa kule, “Mnakwenda kwenye moja ya uwanja maarufu nchini Uingereza, Liverpool ni timu yenye historia na wachezaji wakubwa kama Steven Gerarld, Kenny Dalglish na wengine wengi, pia niwapongeze Standard Chartered kwa kufikisha miaka 100 tangu kuanza kufanya kazi Tanzania,” alisema Cooke. Mkuu wa idara ya Fedha wa Benki ya Standard Chartered, Abdulrahman Said akizungumzia safari ya timu ya Azania katika hafla ya kukabidhi bendera kwa timu hiyo inayokwea pipa kesho 18 Mei kuelekea nchini Uingereza.[/caption] Nae nahodha wa timu hiyo, Khalid Sultan Said aliahidi kuwa timu hiyo inajiamini kuwa inauwepo wa kupambana na timu zingine na kuahidi kuwa itahakikisha kikombe kinakuja nchini. Timu hiyo itaondoka nchini Mei, 18 watafika Mei, 19 wakiwa huko watakutana na timu zingine, Mei, 20 watatembelea uwanja wa Anfield, Mei, 21 watashuhudia mchezo wa Liverpool na Middlesbrough na baada ya hapo wataingia uwanjani kwa ajili ya mashindano na watarejea nchini Mei, 22. Mjumbe wa Bodi ya Standard Chartered Tanzania, Ami Mpungwe (kushoto) akizungumzia wakati wa halfa ya kukabidhi bendera timu ya Azania inayotarajia kukwea pipa kesho Mei 18 kuelekea nchini Uingereza. Kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe. Nahodha wa timu ya Azania, Khalid Sultan Said akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kukabidhiwa bendera kuelekea nchini Uingereza kesho Mei 18. Kikosi cha Timu ya Azania katika hafla ya kukabidhiwa bendera kuelekea nchini Uingereza kesho Mei 18. Picha juu na chini ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akiabidhi hati za kusafiria kwa wachezaji wa timu ya Azania wanaotarajia kukwea pipa kesho Mei 18 kuelekea nchini Uingereza.Katikati ni Mkuu wa Mahusiano wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba. Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke akikabidhi hati ya kusafiria kwa mwandishi wa TV1 atakayeambatana na msafara wa timu hiyo kuelekea nchini Uingereza.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (wa pili kulia) akikabidhi rasmi bendera kwa Nahodha wa timu ya Azania, Khalid Sultan Said. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mjumbe wa Bodi ya Standard Chartered Tanzania, Ami Mpungwe (suti nyeusi) na Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke (kulia). Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akimkabidhi jezi Nahodha wa timu ya Azania, Khalid Sultan Said wakati wa hafla ya kukabidhi bendera timu hiyo. Katikati ni Mjumbe wa Bodi ya Standard Chartered Tanzania, Ami Mpungwe.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TIMU YA AZANIA KUIWAKILISHA TANZANIA KWENYE MASHINDANO YA STANDARD CHARTERED UINGEREZA
TIMU YA AZANIA KUIWAKILISHA TANZANIA KWENYE MASHINDANO YA STANDARD CHARTERED UINGEREZA
http://www.thebeauty.co.tz/wp-content/uploads/2017/05/waziri.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/timu-ya-azania-kuiwakilisha-tanzania.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/timu-ya-azania-kuiwakilisha-tanzania.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy