TIGO YAZINDUA KAMPENI YA ‘JAZA UJAZWE’ KUWASHUKURU WATEJA KWA UAMINIFU WAO

 Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga akifafanua jambo  kwa waandishi wa habari  kuhusu kifurushi cha Jaza Ujazwe mapema leo  katika uz...



 Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga akifafanua jambo  kwa waandishi wa habari  kuhusu kifurushi cha Jaza Ujazwe mapema leo  katika uzinduzi rasmi wa kifurushi hicho "JazaUjazwe’ ambapo mteja  atapata bonus kwa njia ya SMS, Muda wa maongezi, MBs kwa ajili ya kuperuzi internet, Whatsapp na You Tube Kulia kwake ni Mtaalamu wa kubuni Ofa kutoka kampuni ya simu za mkononi ya TIGO Jacqueline Nnunduma na kushoto ni   Meneja Mawasiliano ya Umma wa Tigo Woinde Shisael.

Mtaalamu wa kubuni Ofa kutoka kampuni ya simu za mkononi ya TIGO Jacqueline Nnunduma  akijibu maswali kwa waandishi wakati wa uzinduzi wa kifurushi cha Jaza Ujazwe (katikati)  Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga  na mwishoni ni  Meneja Mawasiliano ya Umma wa Tigo Woinde Shisael .

 Dar es Salaam, Jumatano  Mei 17, 2017- Kampuni inayoongoza mfumo wa maisha ya kidijitali, Tigo Tanzania  imezindua kampeni nyingine mpya ya kuvutia inayofahamika kama, ‘JazaUjazwe’ ambapo mteja  atapata bonus kwa njia ya SMS, Muda wa maongezi, MBs kwa ajili ya kuperuzi internet, Whatsapp na You Tube pindi anapoongeza muda wa maongezi iwe ni kupitia vocha ya kukwangua, Tigo Pesa au Tigo Rusha.
Kwa mujibu wa Tigo kampeni ya ‘Jaza Ujazwe’ imekuja kama  shukrani kwa wateja wa kampuni hiyo ya simu kutokana na uaminifu wao mkubwa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo,  Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga alisema, “Tigo inathamini kuungwa mkono kulikotukuka kunakoonyeshwa na wateja wake kwa kipindi cha miaka mingi, na ndio maana tunaamini wanastahili kupewa shukrani kwa kuendelea kutuamini. Kama kampuni, tunayofuraha  kwa mara nyingine tena  kuwapatia wateja wetu bonus ili waweze kuendelea kufurahia huduma zetu za kiwango cha juu duniani.”
Mpinga alibainisha kuwa  kampeni hiyo mpya inadhihirisha nafasi ya kampuni katika kutoa huduma na bidhaa bora zinazokidhi mahitaji ya wateja  wake na wakati huo huo  kuimarisha mchango wake katika soko kama kampuni ya simu za mkononi iliyo na ubunifu wa hali ya juu.
Alisisitiza  kujikita kwa Tigo katika kuendelea  kuwapatia wateja wake bidhaa na huduma bora zaidi na kuongeza, “Bidhaa na huduma zetu zimeundwa baada ya kufanya tafiti  zinazolenga kuhakikisha wateja wetu wanaridhishwa na wanapata thamani kwa kila shilingi wanayotumia kwa mawasiliano. Hivyo ‘Jaza Ujazwe’ ni kuitikia hitaji la mteja na pia kuwapa wateja uzoefu  wa kusisimua kila wakati wanapotumia bidhaa zetu. Tunaamini kwamba wateja wetu watafurahia dakika za ziada, ujumbe mfupi wa maneno (SMS) au data za bonus na hatimaye kuboresha mwenendo wao wa mawasialiano. 
Wateja wote wa Tigo wanastahili kupata bonus hizi kwa kuwa hakuna masharti yoyote.  

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TIGO YAZINDUA KAMPENI YA ‘JAZA UJAZWE’ KUWASHUKURU WATEJA KWA UAMINIFU WAO
TIGO YAZINDUA KAMPENI YA ‘JAZA UJAZWE’ KUWASHUKURU WATEJA KWA UAMINIFU WAO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg7pmLK5Q-afUTME0gu686QoYkwoZxLkkS1QIRqr5kwtcpixZsegmNllVb75y_0F8BSBo-56M-owSJ7B4eAi5v-cwBJt9mijBzXz6fI1Uwl41GAY0NP6FDiBXPzmSG_Gv242eMzWUg6kZs/s640/_MG_5550.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg7pmLK5Q-afUTME0gu686QoYkwoZxLkkS1QIRqr5kwtcpixZsegmNllVb75y_0F8BSBo-56M-owSJ7B4eAi5v-cwBJt9mijBzXz6fI1Uwl41GAY0NP6FDiBXPzmSG_Gv242eMzWUg6kZs/s72-c/_MG_5550.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/tigo-yazindua-kampeni-ya-jaza-ujazwe.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/tigo-yazindua-kampeni-ya-jaza-ujazwe.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy