F TIB CORPORATE BANK WORKING WORKING 24 HOURS -ABIDING TO PRESIDENT JPM DIRECTIVES | RobertOkanda

Wednesday, May 24, 2017

TIB CORPORATE BANK WORKING WORKING 24 HOURS -ABIDING TO PRESIDENT JPM DIRECTIVES

Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya TIB Corporate, Frank Nyabundege akiongea na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu benki hiyo kuanza kutoa huduma za Kibenki kwa siku zote kwa saa 24 katika tawi lao lililopo Bandarini. Hii ni sanjari na agizo la Rais John Magufuli kuzitaka taasisi zinazotoa huduma Bandarini kufanya kazi kwa saa 24. Pamoja naye ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya TIB Corporate Theresia Soka na Mkurugenzi wa Biashara Mwallu Mwachang’a.

Baadhi ya wakurugenzi wa benki hiyo wakiwa katika mkutano huo.

Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.

Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya TIB Corporate Theresia Soka akiwataarifu waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu benki hiyo kuanza kutoa huduma za Kibenki kwa siku zote kwa saa 24 katika tawi lao lililopo Bandarini. Hii ni sanjari na agizo la Rais John Magufuli kuzitaka taasisi zinazotoa huduma Bandarini kufanya kazi kwa saa 24. Pamoja naye (katikati) ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo, Frank Nyabundege na Mkurugenzi wa Biashara Mwallu Mwachang’a.
TIB CORPORATE BANK WORKING TPA BRANCH WORKING 24 HOURS -ABIDING TO PRESIDENT JPM DIRECTIVES.
The Bank has already commenced to offer 24 hours banking services through the TPA Mini Branch located within the Port Premises. This is in line with directives of his Excellency president John Pombe Magufuli requiring all institutions responsible with Port activities to offer services for 24 hours every day.
The bank facilitates payments of all types of taxes as well as payments for all port charges.
The bank is well prepared and equipped following the recent initiative to embark on TAXBANK , a collection system whereby the tax payers are able to pay for their Taxes via TIB Corporate Bank Network to TRA account with an instant automatic update to TRA system.
Further, TIB Corporate Bank being main banker for Tanzania Port Authority (TPA) means that all port charges paid through the bank are instantly updated to TPA records enabling quick progress on other following processes.

TIB Corporate Bank Ltd (TIB- CBL) is a fully fledged commercial bank, 100% owned by the Government of the United Republic of Tanzania.

The Bank has a branch network in main cities of Tanzania 3 in Dar-Es-Salaam namely Samora , Mlimani City and TPA mini branch and 3 branches upcountry namely; Arusha, Mwanza, and Mbeya. The branches are strategically located to serve the Coast, Northern, Lake and Southern zones.
The bank offers customized products including credit facilities, Trade products, cash management products and treasury products. All these embodied with state of the Art Premier banking lounge to our esteemed clients.KUITIKIA AGIZO LA RAIS JPM -TIB CORPORATE BANK YATOA HUDUMA ZA KIBENKI KWA MASAA 24 KUPITIA TAWI DOGO LA TPA.
Benki ya TIB Corporate tayari imeanza kutoa huduma za kibenki kwa siku zote kwa masaa 24 katika tawi dogo la TPA lililopo ndani ya eneo la Bandari.
Hii ni sambamba na agizo la raisi wetu Mhe. John Pombe Magufuli kuzitaka taasisi husika katika bandari kutoa huduma siku zote kwa masaa 24.

Benki ya TIB Corporate inawezesha wananchi wote kulipia kodi za aina mbalimbali pamoja na tozo zote za bandari. Benki imejipanga vyema ili kuhakikisha huduma hii inaleta ufanisi na urahisi zaidi kwa mlipaji.

Hivi karibuni benki ilingia mkataba na Mamlaka ya Mapato Tanzania - TRA kwa kuunganisha mfumo wa Malipo ya Kodi ujulikanao kama TAXBANK. Kwa kupitia mfumo huu, mlipa kodi akilipia katika tawi lolote la benki, taarifa zake zinaonekana mara moja katika mtandao wa TRA hivyo kumuwezesha mlipa kodi kuendelea na taratibu zingine kwa haraka na  ufanisi zaidi.
Sambamba na hili TIB Corporate ndio yenye dhamana ya kusimamia sehemu kubwa ya  akaunti za mamlaka ya Bandari-TPA hivyo basi mwanachi anapolipia tozo yoyote ya bandari taarifa zake huonekana mara moja katika mtandao wa TPA hivyo kurahisisha na kuwezesha kuendelea na taratibu zingine kwa haraka zaidi.

TIB Corporate Bank Ltd (TIB CBL) ni benki ya  biashara inayomilikiwa na Serikali kwa 100%. Benki inatoa huduma zote za kibenki za kibishara kwa  mashirika na taasisi za aina mbalimbali za serikali na  binafsi , pia benki inatoa huduma kwa watu binafsi.
Benki ina matawi  6 kwa sasa,  Dar es salaam (3), Mwanza , Arusha na Mbeya.

Benki inatoa huduma mbalimbali  kutokana na mahitaji ya mteja. Baadhi ya  huduma hizo ni pamoja na; akaunti za aina mbalimbali kwa makampuni na watu binafsi, mikopo ya aina mbali mbali ya muda mfupi na wa kati, Dhamana za Kibenki(Guarantees),Uuzaji na ununuaji wa fedha za kigeni, ushauri wa uwezekaji katika hati fungani, ukusanyaji wa fedha na kuwezesha malipo ya jumla kwa makampuni pamoja na ulipaji wa mishahara kwa njia rahisi na ya haraka
Huduma zote hizi hutolewa kwa umahiri na ufanisi mkubwa ili kuhakikisha mteja anafurahia mahusiano yake na benki.


0 comments:

Post a Comment