F TIB CORPORATE BANK PARTNERSHIP WITH TANZANIA REVENUE AUTHORITY (TRA) | RobertOkanda

Tuesday, May 16, 2017

TIB CORPORATE BANK PARTNERSHIP WITH TANZANIA REVENUE AUTHORITY (TRA)

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) Charles Kichere (kushoto) na Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya TIB, Frank Nyabundege wakibadilishana mkataba wa makubaliano ya kufanya biashara pamoja katika Bandari ya Dar es Salaam jijini humo leo. Anayeshuhudia ni Mkuu wa Mahusiano wa Benki ya TIB Corporate, Theresia Soka.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) Charles Kichere (kushoto) na Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya TIB, Frank Nyabundege wakionesha mkataba wa makubaliano walioyokubaliana kufanya biashara katika Bandari ya Dar es Salaam jijini humo leo. Pamoja nao ni Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa mamlaka hiyo, Richard Kayombo na Mkuu wa Mahusiano wa Benki ya TIB Corporate, Theresia Soka.

Baadhi ya waandishi wa habari wakishuhudia kubadilishana kwa mkataba huo.
Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya TIB, Frank Nyabundege akiwa (kushoto) pamoja na wawakilishi wa Benki hiyo, Mkuu wa Mahusiano wa Benki ya TIB Corporate, Theresia Soka, Mkurugenzi wa Biashara, Mwallu Mwachang'a na Mkurugenzi wa Matawi na huduma kwa wateja, Bahati Minja (wa pili kulia) walipohudhuria hafla hiyo.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) Charles Kichere (kushoto) akiwashikisha jambo wana habari baada ya kumaliza hafla ya makabidhiano ya mkataba na Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya TIB, Frank Nyabundege. Pamoja na wawakilishi wa Benki hiyo, Mkuu wa Mahusiano wa Benki ya TIB Corporate, Theresia Soka, Mkurugenzi wa Biashara, Mwallu Mwachang'a na Mkurugenzi wa Matawi na huduma kwa wateja, Bahati Minja (wa pili kulia) walipohudhuria hafla hiyo


TIB CORPORATE BANK PARTNERSHIP WITH TANZANIA REVENUE AUTHORITY (TRA)
The bank has partnered with TRA in tax collection through Taxbank system.
TAXBANK is a collection service provided by Tanzania Revenue Authority (TRA), via integration with Revenue Gateway System (RGS).The tax payers will be able to pay for their Taxes via TIB Corporate Bank Network to TRA account with an instant automatic update to TRA system

TIB Corporate Bank Ltd (TIB- CBL) is a fully fledged commercial bank, 100% owned by the Government of the United Republic of Tanzania.

The Bank has a branch network in main cities of Tanzania 3 in Dar-Es-Salaam namely Samora , Mlimani City and TPA mini branch and 3 branches upcountry namely; Arusha, Mwanza, and Mbeya. The branches are strategically located to serve the Coast, Northern, Lake and Southern zones.
The bank offers customized products including credit facilities, Trade products, cash management products and treasury products. All these embodied with state of the Art Premier banking lounge to our esteemed clients.

The partnership is geared towards supporting government initiative to improve efficiency in TAX collection, thought this initiative Taxi payers will enjoy various benefits including

  • Simplified tax payment, more efficiency and convenience.
  • Minimised human error.
  • Minimised operational cost

TIB Corporate is the main banker for Tanzania Ports Authority-TPA. We already have a mini branch within the Port premises operating 24 hours to facilitate payments for taxes and Port Charges. This is in line with directives of his Excellency president John Pombe Magufuli requiring all institutions responsible with Port activities to offer services for 24 hours a day.
TIB CORPORATE BANK LIMITED YAINGIA UBIA NA MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA (TRA)
Benki ya TIB Corporate imeingia ubia na TRA kwa kuunganisha mifumo yao ya malipo ili kuwezesha kulipa kodi kwa urahisi.
TAXBANK Ni mfumo wa kisasa wa ukusanyaji wa kodi ambao umerahisisha ulipaji  wa kodi kwa wateja wetu. Kwa kupitia utaratibu huu Bank imeunganisha mfumo wake wa malipo moja kwa moja na mfumo wa TRA, hivyo mlipa kodi akilipia katika tawi lolote la bank, taarifa zake zinaonekana mara moja katika mtandao wa TRA hivyo kumuwezesha mlipa kodi kuendelea na taratibu zingine kwa haraka na  kiurahisi zaidi.

TIB Corporate Bank Ltd (TIB CBL) ni benki ya  biashara inayomilikiwa na Serikali kwa 100%. Benki inatoa huduma zote za kibenki za kibishara kwa  mashirika na taasisi za aina mbalimbali za serikali na  binafsi , pia benki inatoa huduma kwa watu binafsi.
Benki ina matawi  6 kwa sasa,  Dar es salaam (3), Mwanza , Arusha na Mbeya.

Benki inatoa huduma mbalimbali  kutokana na mahitaji ya mteja. Baadhi ya  huduma hizo ni pamoja na; akaunti za aina mbalimbali kwa makampuni na watu binafsi, mikopo ya aina mbali mbali ya muda mfupi na wa kati, Dhamana za Kibenki(Guarantees),Uuzaji na ununuaji wa fedha za kigeni, ushauri wa uwezekaji katika hati fungani,ukusanyaji wa fedha na kuwezesha malipo ya jumla kwa makampuni pamoja na ulipaji wa mishahara kwa njia rahisi na ya haraka
Huduma zote hizi hutolewa kwa umahiri na ufanisi mkubwa ili kuhakikisha mteja anafurahia mahusiano yake na benki.

Benki imejiunga na mfumo  huu wa ulipaji kodi, ili kusaidia kufanikisha malengo ya serikali katika kuongeza ufanisi katika kukusanya kodi. Kwa kupitia mfumo huu mlipa kodi anapata huduma bora zaidi pamoja na faida zifuatazo
  • Kumrahisishia mlipa kodi  kufanya muamala wa kulipa kodi kwa haraka na ufanisi.
  • Kupunguza uwezano wa makosa katika ulipaji wa kodi
  • Kupunguza ghrama za uendeshaji na miamala.

TIB Corporate ndio yenye dhamana ya kusimamia sehemu kubwa ya  akaunti za mamlaka ya Bandari-TPA. Tayari tunalo tawi dogo ndani ya bandari ili kuhakikisha kuwa tunawezesha ulipaji wa kodi zote na tozo za bandari kwa ukaribu. Kutoa huduma za kibenki kwa masaa 24 sambamba na agizo la raisi wetu Mhe. John Pombe Magufuli kuzitaka taasisi husika katika bandari kutoa huduma kwa masaa 24.

0 comments:

Post a Comment