Wazalishaji wadogo wadogo wa bidhaa nchini wameshauriwa kutumia fursa ya bure ya ukaguzi wa bidhaa zao inayotolewa na Shirika la Viwan...
Wazalishaji wadogo wadogo wa bidhaa nchini wameshauriwa kutumia fursa ya bure ya ukaguzi wa bidhaa zao inayotolewa na Shirika la Viwango Tanzania TBS.
Hayo yamesemwa na Afisa Masoko Mwandamizi kutoka katika shirika hilo, Gladnes
Kaseka pichani kushoto juu wakati akiongea na waandishi wa habari
kwenye maonyesho ya tano ya biashara ya Mkoa wa Tanga.
Kaseka pichani kushoto juu wakati akiongea na waandishi wa habari
kwenye maonyesho ya tano ya biashara ya Mkoa wa Tanga.
Alisema kuwa licha ya TBS kutoa fursa hiyo lakini bado wazalishaji wadogo na
wakati wameshindwa kuitumia fursa hiyo kwa ukamilifu wake na kusababisha
kuendelea kuwepo kwa bidhaa ambazo hazina nembo ya ubora.
wakati wameshindwa kuitumia fursa hiyo kwa ukamilifu wake na kusababisha
kuendelea kuwepo kwa bidhaa ambazo hazina nembo ya ubora.
"Bado wazalishaji wetu wengi hawajaweza kuifikia fursa hiyo ambayo itaweza
kuwasaidia kuhakikisha wanazalisha bidhaa zenye ubora lakini wataweza
kuingiza bidhaa zao kwa urahisi katika masoko ya ushindani tofauti na
sasa" alisema Kaseka.
kuwasaidia kuhakikisha wanazalisha bidhaa zenye ubora lakini wataweza
kuingiza bidhaa zao kwa urahisi katika masoko ya ushindani tofauti na
sasa" alisema Kaseka.
Aidha alisema kuwa bado wanaendelea na jitihada za kuhakikisha wanaziondosha
katika soko bidhaa ambazo ni hafifu kwa kufanya ukaguzi wa Mara kwa Mara
katika masoko na maeneo yote yanayohusika na shughuli za uuzaji wa bidhaa.
katika soko bidhaa ambazo ni hafifu kwa kufanya ukaguzi wa Mara kwa Mara
katika masoko na maeneo yote yanayohusika na shughuli za uuzaji wa bidhaa.
Naye Mfanyabiashara Aisha Kisoki alisema kuwa changamoto kubwa ni muingiliano
wa bidhaa kutoka nje ambazo kwa hapa nchini zinauzwa kwa bei rahisi
tofauti na wanazozizalisha.
wa bidhaa kutoka nje ambazo kwa hapa nchini zinauzwa kwa bei rahisi
tofauti na wanazozizalisha.
Alisema kuwa iwapo TBS wataweza kudhibiti uingiaji usio rasmi wa bidhaa kutoka
nje utasaidia sana wafanyabiashara wa ndani ya nchi kuona umuhimu wa
kuweka nembo bidhaa zao.
nje utasaidia sana wafanyabiashara wa ndani ya nchi kuona umuhimu wa
kuweka nembo bidhaa zao.
(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
COMMENTS