TBL GROUP YASHIRIKI KAMPENI YA KUWAJENGEA WASICHANA UWEZO

 Meneja wa Mawasiliano wa TBL Group, Zena Tenga, akiongea na wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Premier iliyopo Bagamoyo k...


 Meneja wa Mawasiliano wa TBL Group, Zena Tenga, akiongea na wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Premier iliyopo Bagamoyo katika semina ya kuwajengea  uwezo wa kujiamini na kukabiliana na  changamoto mbalimbali chini ya mpango unaojulikana kama HerAfrica.
Wanafunzi  wasichana wa shule ya sekondari  ya Premier iliyopo Bagamoyo katika picha ya pamoja wakati  wa semina ya kuwajengea uwezo iliyoandaliwa na mpango wa HerAfrica.
---
Kampuni ya TBL Group imeelezea dhamira yake ya kuunga mkono serikali na taasisi mbalimbali zinazotekeleza mpango wa kuwajengea uwezo watoto wa kike na kuwasaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili na kusababisha wabaki nyuma.

Mkurugenzi wa Uhusiano na Masuala yanayohusiana na kampuni wa TBL Group, Georgia Mutagahywa,aliyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akieleza jinsi kampuni ilivyoshiriki katika semina ya mpango wa kuzungumza na wasichana kuhusiana kupambana na changamoto mbalimbali zinazowakabili ujulikanao kama HerAfrica.

“Mtazamo wetu ndani ya kampuni suala la jinsia tunalipa umuhimu mkubwa kwa kuwa tunaamini kuwa wanawake wanao uwezo wa kufanya vizuri wakipata fursa na kuondokana na changamoto zinazosababisha wabaki nyuma na tutaendelea kuunga mkono jitihada za serikali na taasisi mbalimbali zinazopambana na usawa wa kijinsia na kuondokana na mila potofu zinakwamisha wanawake na kusababisha wabaki nyuma” alisema Mutagahywa.

Katika semina ya taasisi ya HerAfrica iliyofanyika katika sekondari ya wasichana ya Premier iliyopo Bagamoyo, Meneja wa Mawasiliano wa TBL Group, Zena Tenga, aliungana na wanawake wengine kutoa mada za kuwajengea uwezo wa kujiamini wasichana wanaosoma katika shule hiyo.

Mbali na mada za kuwajengea uwezo wa kuamini pia wanafunzi hao wasichana walielezwa changamoto mbalimbali wanazoweza kukutana nazo katika ujana wao zinazoweza kupelekea kushindwa kutimiza ndoto zao na walipewa mbinu na mikakati ya kuzikabili ili waweze kutumiza ndoto zao pia walielezwa umuhimu wa kujibidiisha na masomo yao kwa kuwa elimu ni silaha pekee itakayoweza kuwakomboa.

Mratibu wa programu hiyo nchini,Lilian Matari,kutoka kampuni ya Ushauri wa kitaalamu ya LAS alisema kuwa hii ni semina ya pili ya kuongea na wasichana kufanyika na mkakati wa kampuni ni kuendesha semina nyingi nchini kote ili kuwafikia wasichana wengi hususani waliopo mashuleni.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TBL GROUP YASHIRIKI KAMPENI YA KUWAJENGEA WASICHANA UWEZO
TBL GROUP YASHIRIKI KAMPENI YA KUWAJENGEA WASICHANA UWEZO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjvgf06glPm4U6t6bLqh27CLvwaLorZnHMyreZQcJB1k7uPe20REeXl_kqwnMbVUzU3Wd7J03sQgZMeS_8pYngVBO-oaODqkrGh43yRfkuCTyHqbx166b7VTAIg2Oc609HxN_O7dL022gQ/s640/ZENA-PHOTO+1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjvgf06glPm4U6t6bLqh27CLvwaLorZnHMyreZQcJB1k7uPe20REeXl_kqwnMbVUzU3Wd7J03sQgZMeS_8pYngVBO-oaODqkrGh43yRfkuCTyHqbx166b7VTAIg2Oc609HxN_O7dL022gQ/s72-c/ZENA-PHOTO+1.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/tbl-group-yashiriki-kampeni-ya.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/tbl-group-yashiriki-kampeni-ya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy