TADB YAASWA KUWAFIKIA WAKULIMA WADOGO NCHI NZIMA

Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa William Tate Ole Nasha (MB) (mwenye tai) akikaribishwa katika Banda la Benki y...


Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa William Tate Ole Nasha (MB) (mwenye tai) akikaribishwa katika Banda la Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) mara baada ya kufungua Maadhimisho ya Kampeni ya Wiki ya Maziwa inayofanyika Kitaifa mjini Bukoba, mkoani Kagera kuanzia tarehe 28 Mei had Juni 01.

Wito umetolewa kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) kuwafikia wakulima, wafugaji na wavuvi wadogo nchi nzima ili kuweza kuwakwamua katika changamoto zinazorudisha nyuma juhudi zao za kujiongezea kipato kwa kukosa mitaji ya uhakika katika kuongeza tija ya kilimo nchini.

Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa William Tate Ole Nasha (MB) wakati akifungua rasmi Maadhimisho ya Kampeni ya Wiki ya Maziwa inayofanyika Kitaifa mjini Bukoba, mkoani Kagera.

Mhe. Ole Nasha amesema kuwa dhima ya kuanzishwa kwa TADB ni kutoa suluhisho la ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha na mikopo kwa wakulima wadogo nchini ili kuchagiza maendeleo ya kilimo nchini hivyo Benki ina wajibu wa kuwafikia wakulima wote wadogo wenye uhitaji wa mikopo.

“Nawaomba mujielekeze kutoka mikopo yenu ya gharama nafuu kwa wakulima wadogo ambao hawawezi kupata mikopo kwenye benki za biashara ili kutekeleza lengo la Serikali la kuwainua wakulima kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini,” Mhe. Ole Nasha alisema.

Aliongeza kuwa anafahamu kuwa Serikali ikishirikiana na TADB ilifanya mazungumzo na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na kupelekea Bodi ya Benki ya Maendeleo Afrika kutoa kibali cha kuipatia TADB fedha za kukopesha kwenye sekta ya kilimo, na kuitaka Benki hiyo kutumia fedha hizo kwa kuwapatia wakulima wadogo ambao ni wahitaji zaidi wa miko hiyo.

“Naomba muwakopeshe wakulima hizo fedha ya zaidi  Bilioni 200 ili kuwaongezea tija katika shughuli zao,” aliongeza.

Kwa mujibu wa mpango kazi wa TADB hadi kufikia miaka mitano ijayo itakuwa imefungua ofisi sita za kikanda zenye lengo la kuwahudumia wakulima wote nchini. Ambapo katika hatua za awali Benki hiyo inaendelea kuwajengea uwezo wakulima wa nchi nzima ili kuwaandaa kupata mikopo kutoka Benki hiyo.

Mpango kazi huo unaweka bayana malengo mengine yanayojumuisha utafutaji wa fedha toka vyanzo mbalimbali zenye gharama nafuu kwa minajili ya kuwakopesha Wakulima katika hatua zote za mnyororo wa ongezeko la thamani kwenye mazao ya Kilimo na kupanua wigo wa utaoji mikopo toka Minyororo Kumi na Minne (14) ya mwanzo na kuhusisha pia mazao mengine ya Kilimo na pia kuwaunganisha wakulima na masoko ya ndani na nje ya nchi.

TADB ni taasisi ya serikali ambayo ilianzishwa kwa ajili ya kutatua ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha mikopo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo nchini ambao ulikuwa unachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa; riba kubwa kwenye mikopo ya kilimo; mikopo ya muda mfupi; masharti magumu ya kukopa bila kuzingatia hali halisi ya sekta ya kilimo  na mazao ambayo inaathiriwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya hali ya hewa.
Afisa Mahusiano na Masoko Mkuu wa TADB, Bw. Saidi Mkabakuli (kushoto) akizungumza wakati Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa William Tate Ole Nasha (MB) (mwenye tai) alipotembelea Banda la TADB.
Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa William Tate Ole Nasha (MB) (mwenye tai) akizungumza na maafisa wa TADB (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa Benki hiyo kuwafikia wakulima wote nchini.
Afisa Tathmini wa Mikopo Mwandamizi wa TADB, Bw. Mubezi Buberwa (kulia) na Afisa Mahusiano na Masoko Mkuu wa TADB, Bw. Saidi Mkabakuli (wapili kulia) wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa William Tate Ole Nasha (MB) (mwenye tai) wakati alipotembelea Banda la TADB.
Afisa Tathmini wa Mikopo Mwandamizi wa TADB, Bw. Mubezi Buberwa (kulia) akifafanua hoja mbali mbali kuhusiana na mikopo inayotolewa na Benki hiyo.
Afisa Mahusiano na Masoko Mkuu wa TADB, Bw. Saidi Mkabakuli (kulia) akimuelezea Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa William Tate Ole Nasha (MB) (mwenye tai) mpango wa TADB kuwafikia wakulima nchi nzima.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TADB YAASWA KUWAFIKIA WAKULIMA WADOGO NCHI NZIMA
TADB YAASWA KUWAFIKIA WAKULIMA WADOGO NCHI NZIMA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgTyiLpH8vkyw5QwwJpL-1nc_RCrWfph2hhz0xowbJa4-o5KPcFeplBVWTzt7TQqoguMDZHoirHijr9lEEYunfBpPgH5AcSJ0b6YeNO4xIThufe7R3YUZzFT6lcuU3regpCZqwgA5h2na8/s640/IMG_7291.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgTyiLpH8vkyw5QwwJpL-1nc_RCrWfph2hhz0xowbJa4-o5KPcFeplBVWTzt7TQqoguMDZHoirHijr9lEEYunfBpPgH5AcSJ0b6YeNO4xIThufe7R3YUZzFT6lcuU3regpCZqwgA5h2na8/s72-c/IMG_7291.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/tadb-yaaswa-kuwafikia-wakulima-wadogo.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/tadb-yaaswa-kuwafikia-wakulima-wadogo.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy