Na Daudi Manongi, MAELEZO DODOMA Serikali kupitia Baraza la Uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC) lililopo chini ya Ofisi ya Wa...
Na Daudi Manongi, MAELEZO DODOMA
Serikali
kupitia Baraza la Uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC) lililopo chini ya
Ofisi ya Waziri Mkuu imewataka wananchi kuitumia vyema mifuko 19 ya
uwezeshaji wananchi kiuchumi ili kujipatia mitaji yenye riba nafuu.
Hayo
yamesemwa leo Bungeni na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira na
Vijana Mhe.Anthony Mavunde wakati akijibu maswali mbalimbali ya wabunge
leo Mjini Dodoma.
“Serikali
inawawezesha wananchi ili waweze kukopesheka kupitia Sera ya uwezeshaji
wananchi kiuchumi ya mwaka 2004 na Sheria ya Uwezeshaji wananchi
kiuchumi Na.6 ya mwaka 2004, Alisema Mhe.Mavunde.
Amesema
Sera hii imeainisha nia ya Serikali ya kuweka mazingira mazuri ya
upatikanaji wa mitaji kwa kuboresha vyanzo vya akiba na kuchukuwa hatua
za kuondoa vikwazo mbalimbali ili kuwezesha mabenki kukopesha kikamilifu
amana zilizopo kwa gharama nafuu,kupitia vikundi vidogo,SACCOS na
Vicoba.
Aidha
kutokana na Sera hii Mipango, Miradi na Mifuko kadhaa imeanzishwa na
Serikali ili kuwezesha wananchi kukopa kwa urahisi ambapo katika mifuko
hiyo 19 baadhi yake ni pamoja na Mfuko wa kuendeleza wajasirimali
wananchi,mfuko wa uwezeshaji wa mwananchi,mfuko wa pembejeo za
kilimo,mfuko wa maendeleo ya vijana, mfuko wa dhamana za mikopo kwa
wajasiriamali wadogo na wa kati,mfuko wa dhamana za mikopo kwa mauzo ya
nje ya nchi ambapo hadi kufikia mwaka 2016 mifuko hii ilikuwa imetoa
mikopo ya trilioni 1.7 kwa wajasiriamali 400,000.
Pamoja na hayo Serikali imeendelea kuweka mazingira mazuri kwa vyombo hivyo kuweza kutoa huduma kwa wananchi.
“Serikali
kupitia Benki kuu ya Tanzania kulingana na mazingira inaendelea
kuangalia viwango vya riba kwa mabenki na Taasisi za fedha ili zimudu
kupata fedha zaidi kwa ajili ya kukopesha wajasiriamali kwa riba
ndogo,ambapo pia imechukua hatua ya kupunguza kiwango cha riba kwa
mikopo yake kutoka asilimia 16 hadi asilimia 12 ”,Alisisitiza Mavunde.
COMMENTS