SERIKALI KUHAMASISHA HALMASHAURI NCHINI KUNUNUA VIUADUDU VYA KUUA VILUILUI VYA MBU WAENEZAO MALARIA

Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA. Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema kuwa itaendel...

Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema kuwa itaendelea kuhamasisha Halmshauri  zote nchini kununua viuadudu vya kibailojia kwa ajili ya kuua viluilui vya mbu waenezao Malaria vinavyotengenezwa na kiwanda cha Biotec product cha Kibaha.

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Dk Hamis Kigwangala  wakati akijibu swali la Mbunge wa Gando Mhe.Othman Omar Haji.


Hayo yamesemwa leo Bungeni na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Dk Hamis Kigwangala  wakati akijibu swali la Mbunge wa Gando Mhe.Othman Omar Haji.
“Viuadudu hivi bimeanza kutengenezwa kuanzia mwezi Desemba 2016 na kwa sasa uhamasishaji huu unaendelea  na endapo viuadudu ivi vitatumiwa vizuri vitasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza kiwango cha maambukizi ya Malaria nchini”,Alisema Mhe.Kigwangalla.
Aidha amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Ushirikiano na Serikali ya Cuba imeendelea kushirikiana katika mambo mengi ikiwemo pamoja na Sekta ya Afya tangu mwaka 1986 mkataba uliposainiwa kati ya Serikali hizi mbili.
Kupitia mkataba huo Serikali ya Tanzania imekuwa ikipokea madaktari bingwa kutoka Cuba ambao wamekuwa wakifanya kazi katika Hospitali za Muhimbili,Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya , Hospitali Tumbi na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma.
Mbali na hayo amesema kuwa Madaktari hao wamekuwa wakitoa huduma mbalimbali za kibingwa kwa wananchi na kuwajengea uwezo madaktari wanaofanya nao kazi katika Hospitali hizo.
Aidha kwa kushirikiana na kampuni ya Labiofarm ya Cuba,Serikali imeweza kujenga kiwanda cha kutengeneza viuadudu ivyo na Serikali ya Cuba imeleta wataalamu.
Kiwanda icho cha Biotec cha kibaha kina uwezo wa kuzalisha lita milioni 2.5 za viuatilifu vya  kuua viluilui vya mbu waenezao Malaria  kwa mwaka.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: SERIKALI KUHAMASISHA HALMASHAURI NCHINI KUNUNUA VIUADUDU VYA KUUA VILUILUI VYA MBU WAENEZAO MALARIA
SERIKALI KUHAMASISHA HALMASHAURI NCHINI KUNUNUA VIUADUDU VYA KUUA VILUILUI VYA MBU WAENEZAO MALARIA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi4yBrEN_DPpUoYy4alQCzxo0yVdKs2b6ctXeHznRut9qk3l7AuT3x6DgoSSBxmtKwGReqzAoYCBJQkOt7BrjjzwMY49oPappwii7d537Kr22hZaLCbJqGv5fga7bo3_bz3Et3MbP3jWNI/s640/9234-Mhe.Kigwangala.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi4yBrEN_DPpUoYy4alQCzxo0yVdKs2b6ctXeHznRut9qk3l7AuT3x6DgoSSBxmtKwGReqzAoYCBJQkOt7BrjjzwMY49oPappwii7d537Kr22hZaLCbJqGv5fga7bo3_bz3Et3MbP3jWNI/s72-c/9234-Mhe.Kigwangala.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/serikali-kuhamasisha-halmashauri-nchini.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/serikali-kuhamasisha-halmashauri-nchini.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy