Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA. Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) imekusanya shilingi bilioni 63,015...
Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.
Serikali
kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) imekusanya shilingi
bilioni 63,015,450,230 kwa kipindi cha Octoba 2013 mpaka Februari 2017
tangu kuanzishwa kwa mtambo wa kuhakiki na kusimamia Huduma za
Mawasiliano(TTMS) nchini.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Edwin
Ngonyani wakati akijibu swali la Mbunge wa Kigamboni Mhe. Dkt Faustine
Engelbert leo Bungeni.
“Mtambo
huu umesaidia Mamlaka ya Mawasiliano nchini kuongeza ufanisi katika
kusimamia Sekta ya Mawasiliano pamoja na kwenda sambamba na kasi ya
mabadiliko yanayotokea katika Sekta ya Mawasiliano Duniani
kote”,Aliongeza Mhe.Ngonyani.
Aidha
kati ya pesa izo bilioni 56,987,368,631 zimewasilishwa hazina na
shilingi bilioni 6,028,081,599 zimewasilishwa Tume ya Sayansi na
Teknolojia(COSTECH) kwa ajili ya kugharamia tafiti mbalimbali zenye
manufaa kwa nchi yetu ambapo kabla ya hapo kahukuwa na mapato hayo.
Amesema
mtambo huu umeiwezesha TCRA kuwa na uwezo wa kusimamia mawasiliano ya
simu za Kimataifa na zile za mwingiliano,pia mtambo huo umesaidia
kudhibiti mawasiliano ya Simu za ulaghai za kimataifa na kusimamia ubora
wa mitandao katika kutoa huduma bora kwa wananchi,kudhibiti namba
tambulishi za vifaa vya mawasiliano nchini pamoja na usimamiaji wa
miamala ya fedha inayopita katika mitandao ya simu hapa nchini.
“Aidha
pamoja na mafanikio hayo jitihada za kuboresha zaidi mfumo huu ili
kuweza kubaini na kujiridhisha juu ya mapato yote yatokanayo na huduma
za mawasiliano na yanayokidhi mahitaji ya Mamlaka ya Mapato
Tanzania,Benki kuu ya Tanzania na TCRA zinaendelea”Aliongeza
Mhe. Ngonyani.
Aidha
Serikali itaendelea kuwajengea uwezo wataalamu wa TCRA ili waweze
kuendana na kasi ya ukuaji wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
hususani katika eneo hili la kuchakata taarifa mbalimbali za huduma za
mawasiliano zinazopatikana kutoka kwa watoa huduma ili kuweza na
kujiridhisha juu ya mapato yote.
COMMENTS