RAIS MAGUFULI AMTAKA PROFESA MUHONGO KUJITATHMINI. NI KUHUSIANA NA KASHFA YA MCHANGA WA MADINI

Rais John Magufuli,leo Jumatano Mei 24, 2017, amepokea ripoti ya kamati ya kuchunguza mchanga wa madini wa kampun...




Rais John Magufuli,leo Jumatano Mei 24, 2017, amepokea ripoti ya kamati ya kuchunguza mchanga wa madini wa kampuni ya ACACIa, na kumtaka Waziri wa Nishati na Madini, Profes Sospeter Muhongo, kujitathmini tena kwa haraka, kama bado anafaa kuongoza wizara hiyo
"Kutokana na ripoti hii ambayo imeonyesha udhaifu mkubwa wa wizara kushindwa kuzuia upotevu mkubwa wa mapato ya serikali kwa kutosimamia ipasavyo usafirishaji wa mchanga wa Madini njema yanchi, ni vema waziri Muhongo ambaye ninamuheshimu sana, lakini kwa swalahili hana budi kupima na kujitathmini kwaharaka ni kwanini asijiuzulu." Alisema Rais Magufuli katika hotuba take Ikulu jijini Dar es Salaam, mara baada ya kupokea taarifa hiyo. HOTUBA FUPI YA, NA HATUA ALIZOCHUKUA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI MARA BAADA YA KUPOKEA RIPOTI YA KAMATI YA KUCHUNGUZA MAKONTENA YA MCHANGA WA DHAHABU (MAKINIKIA YA DHAHABU)
..Endelea....Tulitumia vifaa vyote katika ulinzi lakini wapo waliojitokeza kutaka kuingilia uchunguzi huu na bahati nzuri majina yote tunayo, wapo wengine mnawajua wenyewe wakibwatuka wengine kwenye mitandao, wamepewa fedha.
Ndugu zangu tuko kwenye vita na vita ya uchumi ni mbaya sana, mabilioni ya fedha haya ambayo nchi yetu imepoteza, dhahabu tani tani 7.8 hadi 13.16 kwa kontena 277. Tani 15.5 ni malori mawili na land rover moja. Malori mawili ya tani 7 yanaleta tani 14, labda na pick up zote umezipaki pale na hio ni kwa makontena 277.
Kuna tume inayotaka kujua ni makontenayanasafirishwa mangapi, haraka haraka ni makontena 250 na 300 kwa mwezi, kwa mwaka zaidi ya makontena 3600.
Ni kitu cha kuumiza mno na kwa hili watanzania wote tushikamane, hospitali watu wanakosa madawa, mashuka, shule watu wanakosa madawati, hela za treni mpaka tukope kumbe kuna hela zinamwagika hapa.
Nilimfukuza katibu mkuu wa nishati na madini alipoulizwa na kamati ya wabunge kiasi cha dhahabu kilichopo, ni aibu kwa mtu aliesomeshwa na watanzania.
Bilioni 676 hadi trilioni 1.5 tunzazipoteza watanzania, madini mengine hawakujali hata kuyarekodi(Nipe ile document). Tunaweza tukaona kwa miaka kwa 17, tulipaswa kuwa donor country kwa vitu tulivyopewa na Mungu.
Hauwezi ukashangaa katika wizara hizi ndio nilichagua watu waziri wa kuziendesha, kuna tume iliundwa miaka ya nyuma, walidanganya kuna smelter ziko nchi fulani, walipoenda wakaishia hotelini. Smelter sio tatizo kwenye ripoti, inaonyesha kampuni nyingi zinazoweza kuuza smelter, viongozi hawakuchukua juhudi za kununua smelter.
Sera ya taifa ya madini ya mwaka 2009 inasema haja ya kununua smelter, viongozi wa hizo wizara hawakufanya juhudi, kwanini TMAA wapime kidogo halafu wanakuja kuweka tu seal wakati hujui kilichowekwa ndani, kwanini?
Kwanini wasimamizi wasimamizi wa TMAA ambao ni wizara hawakushtukia? Kwanini bodi ya TMAA haiwakushtukia? Inawezekana nikajiuliza maswali mengi majibu yasipatikane. Inawezekana yakaletwa na tume nyingine, nilienda na wenzangu kuteta kidogo, Haiwezi kupita hivi hivi.
Ripoti hii ikipita hivi hivi tutakuwa watu wa ajabu sana, tutafanya kitu, tunasubiri ile ripoti nyingine.
Mapendekezo yote ya tume nimeyakubali Bodi ya TMAA nimeivunja Rasmi Namsimamisha kazi mkurugenzi mkuu wa TMAA na wafanyakazi waanze kuchunguzwa na vyombo vya dola Shughuli zote zinazohusu madini, vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vianze kutumika sawasawa. Wizara wameshindwa kusimamia TMAA, ujenzi wa Smelter pia imeshindwa kuweka utaratibu wa kufatili haya makenikia, mbona huwa wanaenda Ulaya? Kamishna madini anafanya nini? Waziri anafanya nini?
Vyombo viwachunguze watendaji wa wizara ya madini wanaoshughulia

Nampenda sana Prof Mhongo na ni rafiki yangu, kwa hili ajitathmini na nilitaka aachie madaraka.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RAIS MAGUFULI AMTAKA PROFESA MUHONGO KUJITATHMINI. NI KUHUSIANA NA KASHFA YA MCHANGA WA MADINI
RAIS MAGUFULI AMTAKA PROFESA MUHONGO KUJITATHMINI. NI KUHUSIANA NA KASHFA YA MCHANGA WA MADINI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEixblE82Gt_aDQ_UZlp8nJ0hXPXKLKtg3MMCzEMOFCmsfxLOnAGh3PGn9O5gbmeD-HDNMJf5WvH3yYD3LfsYvViSyWwaJJxlWMGVKc46_ofQyDf_JIRAY6pHq1E_9qhTd-Ef0YXzPttpQ0/s640/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEixblE82Gt_aDQ_UZlp8nJ0hXPXKLKtg3MMCzEMOFCmsfxLOnAGh3PGn9O5gbmeD-HDNMJf5WvH3yYD3LfsYvViSyWwaJJxlWMGVKc46_ofQyDf_JIRAY6pHq1E_9qhTd-Ef0YXzPttpQ0/s72-c/1.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/rais-magufuli-amtaka-profesa-muhongo.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/rais-magufuli-amtaka-profesa-muhongo.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy