F RAIS MAGUFULI AKUTANA NA MAKAMU MWENYEKITI WA SHIRIKISHO LA VIWANDA CHINA NA MABALOZI | RobertOkanda

Tuesday, May 23, 2017

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA MAKAMU MWENYEKITI WA SHIRIKISHO LA VIWANDA CHINA NA MABALOZI


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na  Bw. Zhang Xin, Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya China National Machinery Industry Federation (CBMIF) na mjumbe wa National Congress ya China Bw. Zhang Xin aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam Mei 23, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akizungumza na  Bw. Zhang Xin, Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya China National Machinery Industry Federation (CBMIF) na mjumbe wa National.
Congress ya China Bw. Zhang Xin aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam Mei 23, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa tayari kumsindikiza na  Bw. Zhang Xin, Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya China National Machinery Industry Federation (CBMIF) na mjumbe wa National Congress ya China Bw. Zhang Xin aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam Mei 23, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja  na  Bw. Zhang Xin, Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya China National Machinery Industry Federation (CBMIF) na mjumbe wa National Congress ya China Bw. Zhang Xin na ujumbe wake na maafisa wa serikali aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam Mei 23, 2017

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkaribisha Kaimu Balozi wa Korea Kusini nchini Mhe. Songwon Shin aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam Mei 23, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Kaimu Balozi wa Korea Kusini nchini Mhe. Songwon Shin aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam Mei 23, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimsindikiza Kaimu Balozi wa Korea Kusini nchini Mhe. Songwon Shin aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam Mei 23, 2017

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimlaki Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Malika Berak aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam Mei, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Malika Berak aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam Mei 23, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimsindikiza baada ya mazungumzo  Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Kaimu Balozi wa Uturuki nchini Mhe. Yunus Belei aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam Mei 23, 2017

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Kaimu Balozi wa Uturuki nchini Mhe. Yunus Belei aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam Mei 23, 2017
(PICHA NA IKULU)

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULUDescription: Description: Description: Description: Description: Coat of Arms
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz               

Faksi: 255-22-2113425OFISI YA RAIS,
     IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewahakikishia wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Shirikisho la Taifa la Utengenezaji wa Mitambo ya Viwanda la China (China National Machinery Industry Federation - CNMIF) kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itawapa ushirikiano wa kutosha katika mpango wao wa kuwekeza katika uzalishaji wa nishati ya umeme, viwanda na kilimo hapa nchini.
Mhe. Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo tarehe 23 Mei, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa CNMIF na Mbunge wa Bunge la Wananchi wa China Bw. Zhan Xin.
Mhe. Dkt. Magufuli amesema Tanzania imejiwekea malengo ya kuongeza uzalishaji wa umeme kutoka Megawatts kati ya 1,500 na 1,800 zinazozalishwa hivi sasa hadi kufikia Megawatts 10,000 na kwamba ili kufikia malengo hayo wawekezaji wanakaribishwa kuzalisha umeme kwa kutumia vyanzo vilivyopo kama vile gesi, makaa ya mawe na jua.
“Kwa hiyo Ndg. Zhang Xin kawaambie wawekezaji wenzako wa China waje Tanzania, nchini zetu ni ndugu na marafiki wa miaka mingi, itakuwa jambo jema wakija kuunga mkono juhudi zetu za kujenga viwanda kwa kuzalisha umeme mwingi na pia kushiriki katika miradi mingine ikiwemo ya ujenzi wa miundombinu ya reli na barabara” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amekutana na Balozi wa Ufaransa hapa nchini Mhe. Malika Berak ambapo viongozi hao wamezungumzia utekelezaji wa mambo mbalimbali ya ushirikiano pamoja na miradi ya maendeleo iliyotokana na makubaliano ya Mkutano wa wafanyabishara wa Tanzania na Ufaransa uliofanyika hivi karibuni.
Viongozi wengine ambao leo wamekutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Rais Magufuli ni Kaimu Balozi wa Uturuki hapa nchini Bw. Yunus Belet na Kaimu Balozi wa Jamhuri ya Korea Bw. Songwon Shin.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
23 Mei, 2017

0 comments:

Post a Comment