F RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI TAMISEMI | Okandablogs

Wednesday, May 24, 2017

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI TAMISEMI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULUDescription: Description: Description: Description: Description: Coat of Arms
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz               

Faksi: 255-22-2113425



OFISI YA RAIS,
     IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ikulu, Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 24 Mei, 2017 amemteua Bw. Tixon Tuliangine Nzunda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) -  anayeshughulikia Elimu.
Kabla ya uteuzi huo Bw. Tixon Tuliangine Nzunda alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa.
Bw. Tixon Tuliangine Nzunda anachukuwa nafasi ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) -  akishughulikia Elimu Bw. Bernard Makali ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa.
Uteuzi huu unaanza mara moja.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
24 Mei, 2017

0 comments:

Post a Comment