RAIS DKT. MAGUFULI PAMOJA NA MKEWE MAMA JANETH WATEMBELEA KUWAJULIA HALI WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI DAR ES SALAAM

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU Simu: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz ...

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULUDescription: Description: Description: Description: Description: Coat of Arms
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz               

Faksi: 255-22-2113425



OFISI YA RAIS,
     IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 28 Mei, 2017 amewajulia hali wagonjwa waliolazwa katika wodi ya Mwaisela iliyopo katika hospitali ya Taifa Muhimbili na kuwashukuru Madaktari na Wauguzi kwa juhudi kubwa wanazofanya kunusuru maisha ya watu.
Mhe. Rais Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli wamewatembelea wagonjwa hao majira ya saa moja ya asubuhi wakitokea katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam ambako wamehudhuria ibada ya Jumapili.
Miongoni mwa wagonjwa waliojuliwa hali na Mhe. Rais Magufuli na mkewe ni Mzee Francis Maige Kanyasu (Ngosha) aliyelazwa katika chumba namba 310 na Mtoto Shukuru Musa Kisonga aliyelazwa katika chumba namba 312 ambaye hivi karibuni aliripotiwa kuugua ugonjwa usiofahamika uliosababisha aishi kwa kunywa mafuta ya kula, sukari na Maziwa.
Pamoja na kuwapa pole wagonjwa waliolazwa katika wodi ya Mwaisela na kuwashukuru Madaktari na Wauguzi, Mhe. Rais Magufuli amesema Serikali itaendelea kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili hospitali hiyo na changamoto zinazowakabili madaktari na wauguzi.
“Jamani, Madaktari tunawashukuru sana, mnafanya kazi nzuri, Madaktari wote nchini pokeeni pongezi zangu, sisi Serikali tutaendelea kuzikabili changamoto hizo na siku moja zitakwisha, kikubwa ni kumtanguliza Mungu mnapofanya kazi ya kuokoa maisha ya watu kwa juhudi kubwa, mnafanya kazi ya Mungu” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuwatembelea wagonjwa katika hospitali hiyo na amemhakikishia kuwa Madaktari tayari wamegundua magonjwa yanayowakabili Mzee Francis Maige Kanyasu (Ngosha) na Mtoto Shukuru Musa Kisonga na kwamba wanaendelea vizuri na matibabu.
Aidha, Prof. Museru amesema hospitali hiyo imepiga hatua kubwa ya kujenga uwezo wa kutibu magonjwa ambayo wagonjwa walilazimika kwenda kutibiwa nje ya nchi na hivyo kuokoa fedha nyingi za Serikali.
“Mhe. Rais hospitali yetu sasa imeanza kufanya upasuaji na kutoa tiba ya magonjwa ambayo yalilazimu wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi, mfano hivi sasa tunatoa huduma ya kusafisha figo kwa wagonjwa takribani 250, na kuanzia mwezi Julai mwaka huu tutaanza kupandikiza figo.
“Huduma hii hugharimu kati ya Shilingi Milioni 60 na Shilingi Milioni 70 kwa mgonjwa mmoja anayekwenda kutibiwa nje ya nchi, lakini hapa nchini gharama zinashuka hadi Shilingi Milioni 21” amesema Prof. Museru.
Prof. Museru ameongeza kuwa Hospitali ya Taifa Muhimbili pia inajipanga kuanza kutoa huduma ya matibabu kwa watoto wenye matatizo ya usikivu ambao wapo hatarini kuwa viziwi na hivyo kuokoa fedha nyingi zinazotumika kuwatibu nje ya nchi, kutoka Shilingi Milioni 90 hadi Shilingi Milioni 30.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
28 Mei, 2017


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakimjulia hali Mzee Francis Maige Kanyasu(Ngosha) aliyelazwa Wodi ya Mwaisela katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya Matibabu. Wakwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Profesa Lawrence Museru pamoja na Dkt. Juma Mfinanga Daktari Bingwa wa magonjwa ya Dharura na Ajali katika hospitali hiyo. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mzee Francis Maige Kanyasu(Ngosha) aliyelazwa Wodi ya Mwaisela katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya Matibabu 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakimjulia hali mtoto Shukuru Kisonga aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Mtoto Shukuru alikuwa akidaiwa kuishi kwa kula Sukari, Maziwa na mafuta ya kula lakini hali yake imeimarika zaidi na kuanza kula vyakula vya kawaida. Katikakati ni Mama yake Shukuru Mwanahabibi Mohamed Mtei. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakimtakia heri mtoto Shukuru Kisonga aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili pamoja na Mama yake Mwanahabibi Mohamed Mtei. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwajulia hali wagonjwa wengine waliolazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwajulia hali wagonjwa wengine waliolazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkurugenzi wa Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwajulia hali wagonjwa wengine waliolazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini. (Picha na Ikulu)

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RAIS DKT. MAGUFULI PAMOJA NA MKEWE MAMA JANETH WATEMBELEA KUWAJULIA HALI WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI DAR ES SALAAM
RAIS DKT. MAGUFULI PAMOJA NA MKEWE MAMA JANETH WATEMBELEA KUWAJULIA HALI WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI DAR ES SALAAM
https://lh3.googleusercontent.com/0TANDmqj7kQ5DfNaRiAMhRdwqEi7LXgv7c2wpJFu6r-XduhwDrPiMaSRuWlPvxzZOrUk60ypp8X6lFjurrsptR4ZRJPqPDKiNWRnZAa5CJYbkLvDbbF1aVWvTdVGPqf9RCq_ylN2SzP7wB_z-g
https://lh3.googleusercontent.com/0TANDmqj7kQ5DfNaRiAMhRdwqEi7LXgv7c2wpJFu6r-XduhwDrPiMaSRuWlPvxzZOrUk60ypp8X6lFjurrsptR4ZRJPqPDKiNWRnZAa5CJYbkLvDbbF1aVWvTdVGPqf9RCq_ylN2SzP7wB_z-g=s72-c
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/rais-dkt-magufuli-pamoja-na-mkewe-mama.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/rais-dkt-magufuli-pamoja-na-mkewe-mama.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy