F RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM | Okandablogs

Saturday, May 27, 2017

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Rajab Omar Luhwavi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Benard Mtandi Makali kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa, Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Clifford Katondo Tandari kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro, Ikulu jijini Dar es Salaam


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ndugu Geoffrey Idelphonce Mwambe kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Ikulu jijini Dar es Salaam.


Viongozi waliopishwa wakila Kiapo cha Uadilifu Ikulu Dar es Salaam. Kutoka (kulia) ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Tixon Tuyangine Nzunda, Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji Rajab Omar Luhwavi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa, Benard Mtandi Makali,  Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro, Clifford Katondo Tandari pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Geoffrey Idelphonce Mwambe.


Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji Rajab Omar Luhwavi mara baada ya kupiga picha ya pamoja Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ikulu)

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULUDescription: Description: Description: Description: Description: Coat of Arms
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz               

Faksi: 255-22-2113425OFISI YA RAIS,
     IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 27 Mei, 2017 amemuapisha Bw. Tixon Tuyangine Nzunda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) - anayeshughulikia Elimu.
Viongozi wengine walioapishwa na Mhe.Rais Dkt. Magufuli ni Bwa. Rajab Omar Luhwavi ambaye anakuwa Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji.
Bw. Bernard Mtandi Makali ameapishwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa na Bw. Clifford Katondo Tandari, kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro.
Pia Rais Magufuli amemuapisha Bw. Geoffrey Idelphonce Mwambe kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).
Viongozi wote walioapishwa wameahidi kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi wa hali ya juu katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Hafla ya kuapishwa viongozi hao imehudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  Mhe. Dkt. Augustine Mahiga na viongozi mbalimbali wa Serikali.


Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
27 Mei, 2017

 

0 comments:

Post a Comment