PPF YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA MOROGORO

Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele (kulia) akimkabidhi msaada wa mashuka Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala ...


Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele (kulia) akimkabidhi msaada wa mashuka Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa Bi. Zainab Chaula (kushoto) kwa ajili ya hospitali ya Rufaa ya Morogoro. Msaada huo ni sehemu ya vifaa tiba vilivyotolewa na Mfuko huo ambapo katika mwaka wa fedha 2016/2017 jumla ya shilingi milioni 99,983,700 zimetolewa kununulia vifaa tiba vinavyogawiwa katika hospitali na vituo vya afya 16 vya serikali nchini. (Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog)
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali ya mitaa Bi. Zainab Chaula (kushoto) akimkabidhi mashuka ambayo ni sehemu ya vifaa tiba kwa Meya wa Manispaa ya Morogoro, Paschal Mahanga (kulia) kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Morogoro. Wengine wanaoshuhudia ni Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Lulu Mengele (wa kwanza kushoto) na Meneja wa PPF Kanda ya Mashariki na Kati, Bw. Michael Christian.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za mkoa na Serikali ya Mitaa Bi. Zainab Chaula akitoa shukrani kwa PPF kwa kuweza kurudisha sehemu ya mapato yake kwa jamii kwa kutoa vifaa tiba.

Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Lulu Mengele akizungumza mbele ya wageni waliofika katika hafla ya kutoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi mil. 6,077,800 kwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ambapo PPF imetoa sehemu ya mapato yake kwa jamii kulingana na sera ya uchangiaji na udhamini ya Mfuko huo.
Mganga mkuu wa hospitali ya rufaa ya Morogoro, Frank Jacob akitoa shukrani wa PPF.

Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF kanda ya Kaskazini na Kati na wafanyakazi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro.

Meya wa Manispaa ya Morogoro, Paschal Mahanga akitoa ufafanuzi mchache jinsi alivyokuwa anaufahamu Mfuko wa Pensheni PPF.

Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF kanda ya Kaskazini na Kati na wafanyakazi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro wakielekea wodini.
Wagonjwa wakitumia mashuka na vitanda vilivyotolewa na PPF.
---
Serikali imefurahishwa na na juhudi za Mfuko wa Pensheni PPF kwa kutoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya milioni 99,983,700 kwa hospitali 16 hapa nchini ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya afya hapa nchini.

Akielezea furaha hiyo wakati akipokea sehemu ya msaada huo wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 6 kwa hospitali ya mkoa wa Morogoro, Naibu Katibu Mkuu ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dkt. Zainab Chaula amesema kumekua na chanagamoto mbalimbali za vifaa tiba katika hospitali mbalimbali hapa nchini.

Kwa upande wake meneja wa uhusiano wa PPF, Lulu Mengele amesema pamoja na kutoa mafao ya pensheni na mafao mengine yanayoendana na hayo kwa wanachama wake kutoka kwenye sekta rasmi na isiyokuwa rasmi. Mfuko wa Pensheni wa PPF katika sera yake ya uchangiaji na udhamini ambapo moja kati ya sehemu wanayochangia ni upande wa sekta ya afya ambapo katika mwaka wa fedha 2016/2017 jumla ya shilingi milioni 99,983,700 zimetolewa kununulia vifaa tiba vinavyogawiwa katika hospitali na vituo vya afya 16 vya serikali nchini. Sehemu ya vifaa hivyo vilivyotolewa ni muendelezo wa zoezi la kukabidhi vifaa tiba lilizinduliwa na waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa mkutano wa 26 wa wanachama na wadau wa PPF uliofanyika machi 2017 jijini Arusha.

Naye meneja wa PPF kanda ya mashariki na kati, Bw. Michael Christian alisema kuwa PPF wanao mfumo wa uchangiaji wa hiari 'WOTE SCHEME' ambapo aliwakaribisha wananchi waliokatika sekta isiyo rasmi kujiunga ili kunufaika na mafao ya uzeeni, huduma za bima za afya pamoja na mikopo ya elimu na mikopo ya maendeleo. Vile vile wale walio sekta rasmi wanakaribishwa kujiunga kama mfumo wa hiari ili kuweza kujiwekea akiba na kunufaika na mikopo ya elimu na mikopo ya maendeleo.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: PPF YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA MOROGORO
PPF YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA MOROGORO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhNf6XbJXKFz8jJcdS9vkOLMOKC6KzIY88169TUW_Js2LiJTq7JrRW6MeiVLyQ_RDiSwWXelW2Jjme6BKY3z7Fa_TxCZOlBn0-5zCC4xmyrxDtpXoeToEEBPSDOGKiEBU5CKbe1969AiXI/s640/IMG_0639.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhNf6XbJXKFz8jJcdS9vkOLMOKC6KzIY88169TUW_Js2LiJTq7JrRW6MeiVLyQ_RDiSwWXelW2Jjme6BKY3z7Fa_TxCZOlBn0-5zCC4xmyrxDtpXoeToEEBPSDOGKiEBU5CKbe1969AiXI/s72-c/IMG_0639.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/ppf-yatoa-msaada-wa-vifaa-tiba-katika.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/ppf-yatoa-msaada-wa-vifaa-tiba-katika.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy