Ofisa wa Benki ya NMB Tawi la Temeke, Latifa Ayoub Dadah (kushoto) akimkabidhi mpira wa miguu mmoja wa viongozi wa michezo wa Shul...
BENKI
ya NMB imetoa elimu ya masuala ya kibenki na umuhimu wa kujijengea
utamaduni wa uwekaji akiba kwa wanafunzi na baadhi ya wazazi wa Shule ya
Msingi Wailes iliyopo Temeke jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na wanafunzi wa Shule ya Msingi Wailes walioshiriki mafunzo hayo ya
kifedha, Ofisa wa Benki ya NMB Tawi la Temeke, Latifa Ayoub Dadah
alisema NMB inaendelea kutoa elimu ya masuala ya kifedha ikiwa ni pamoja
na kujifunza mbinu za kuweka akiba kwa ajili ya maisha ya baadae.
Alisema
elimu hiyo inatolewa kupitia Programu maalum ya Wajibu ambayo hutoa
fursa kwa watoto, vijana na wazazi kujifunza masuala ya kifedha ili
kumjengea mtoto utamaduni wa kujiwekea akiba, elimu ambayo watoto wengi
hawapati fursa ya kujifunza.
Akizungumza
katika mafunzo hayo, alisema vijana wengi wamekuwa hawana utaratibu wa
kujiweka akiba tangu wadogo hivyo NMB kupitia programu ya Wajibu
inaendelea kutoa elimu kwa watoto, vijana pamoja na wazazi wao kuelewa
umuhimu wa kujiwekea akiba ya fedha kupitia akaunti mbali mbali za benki
hiyo, kama vile Mtoto Account, Chipukizi Account na Mwanachuo Account.
NMB
katika ziara hiyo ambapo ilikuwa imeongozana na wachezaji wa Timu ya
Mpira wa Miguu ya Azam kupitia kituo chao cha michezo, mbali na anafunzi
na wazazi kupata elimu ya masuala ya kifedha na uwekaji akiba kwa
manufaa ya baadaye, wachezaji wa Azam walicheza mpira na wanafunzi hao
pamoja na kugawa zawadi mbalimbali toka NMB na kampuni ya Azam.
Picha ya pamoja ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Wailes na wageni wao
baada ya mafunzo ya programu ya wajibu iliyotolewa na Benki ya NMB.
Ofisa
wa Benki ya NMB Tawi la Temeke, Latifa Ayoub Dadah (kushoto)
akimkabidhi zawadi mmoja wa wazazi wa wanafunzi walioshiriki mafunzo ya
programu ya wajibu ya NMB.
Ofisa wa Benki ya NMB Tawi la Temeke, Latifa Ayoub Dadah (kulia)
akimkabidhi moja ya zawadi mwanafunzi wa Shule ya Msingi Wailes baada ya
kujibu vizuri swali kwenye mafunzo ya programu ya wajibu.
Akifafanua
zaidi, Bi. Latifa alisema elimu hiyo ni mwendelezo wa programu ya
wajibu ambapo NMB imekuwa akizunguka katika shule mbalimbali za msingi
na sekondari nchi nzima huku ikitoa elimu ya kifedha na masuala mazima
ya uwekaji akiba.
Alisema
elimu hiyo itawasaidia watoto na vijana kufanya matumizi mazuri ya
fedha kwa sasa na baadae, elimu ambayo wengi wameikosa. Alisema elimu
hiyo ambayo imepokelewa vizuri kwa wanafunzi na wazazi ambao wameshiriki
itaendelea kutolewa na benki hiyo hivyo kuwashauri wazazi na vijana
kufungua akaunti mbalimbali ya NMB kulingana na maitaji yao ili waweze
kunufaika.
"...Mwitikio
kwa waliopata fursa ya kushiriki katika mafunzo haya ni mzuri kwa kwli
hasa katika wilaya yetu ya Temeke, tumekuwa tukipokea watoto mbalimbali
wakija kufungua akaunti jambo ambalo linaonesha wamevutiwa na elimu
hii," alisema ofisa huyo wa Benki ya NMB Tawi la Temeke.
Naye
Mwalimu wa Taaluma wa Shule ya Msingi Wailes, Zabibu Wasia aliishukuru
Benki ya NMB kwa kutoa mafunzo hayo kwa wanafunzi pamoja na baadhi ya
wazazi/walezi wa shule hiyo na kuahidi kuendelea kuwa mabalozi kueneza
elimu hiyo kwa wengine kutokana na umuhimu wake.
"..Tunaishukuru
sana NMB kwa kuamua kuleta elimu hiyo kwa wanafunzi na wazazi wa Wailes
tunaamini hii ni fursa ya kipekee kwetu maana shule za msingi Dar es
Salaam zipo nyingi lakini umeona muanze na sisi...tunashukuru sana kwa
kutupendelea," alisema Bi. Wasia.
Mbali
na elimu hiyo NMB ilitoa mipira miwili kama zawadi kwa wanafunzi wa
Shule ya Msingi Wailes, yaani mpira wa miguu kwa wanafunzi wa kiume na
mpira wa pete kwa wanafunzi wa kike.
Mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Wailes akijibu swali kwenye
mafunzo ya programu ya wajibu iliyotolewa na Benki ya NMB shuleni hapo.
Baadhi ya wachezaji vijana wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Azam kupitia
kituo chao cha michezo wakiwa na wanafunzi wa Shule ya Msingi Wailes.
Ofisa wa Benki ya NMB Tawi la Temeke, Latifa Ayoub Dadah (kulia) akitoa
elimu ya masuala ya kifedha na akiba kwa wazazi na wanafunzi
walioshiriki mafunzo ya programu ya wajibu ya NMB katika Shule ya Msingi
Wailes ya jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wachezaji vijana (kulia) wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Azam
akipiga mpira alipokuwa akicheza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Wailes
ya jijini Dar es Salaam.
COMMENTS