Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa tatu kulia) akielezea mpango wa Serikali wa kuboresha kil...
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa tatu kulia)
akielezea mpango wa Serikali wa kuboresha kilimo ili kukuza uchumi wa
viwanda alipofanya Mkutano na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha
la Kimataifa (IMF), Tao Zhang (wa tatu kushoto), katika ukumbi wa Wizara
ya Fedha na Mipango jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto)
akielezea kuhusu ujenzi wa Reli kwa kiwango cha Kimataifa (Standard
Gauge) ambapo alisema itasaidia kuchochea maendeleo si tu kwa Tanzania
bali na nchi jirani, wakati wa Mkutano na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang (hayupo pichani) katika
ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam. Kulia ni
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Benno Ndulu.
Naibu
Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang (kushoto)
akizungumza na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango
(Mb), (hayupo pichani) kuhusu nia ya Shirika hilo kufungua fursa zaidi
za mikopo kwa Tanzania, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango
jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa nne
kushoto) na Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF),
Tao Zhang (wa nne kulia) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya
kumalizika kwa Mkutano kati yao katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na
Mipango jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) na
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang
(kushoto) wakiagana baada ya kumaliza mkutano kati yao, katika Mkutano
huo Zhang aliipongeza Serikali kwa hatua nzuri za ukuaji wa Uchumi.
Gavana
wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu (kulia) akipeana mkono na
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF)
anaeziwakilisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba (kushoto)
baada ya kumalizika kwa Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang katika Ofisi za Wizara ya Fedha na
Mipango Jijini Dar es Salaam. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)
……………………………………………………………………………….
Na Benny Mwaipaja, WFM
Naibu
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang
ameahidi kufungua madirisha ya mikopo kwa nchi ya Tanzania kutokana na
jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali za kukuza uchumi.
Bw.
Zhang aliyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa
Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), katika ofisi za
Wizara hiyo Jijini Dar es Salaam.
“Shirika
la Fedha la Kimataifa limeziona jitihada za kukuza uchumi wa nchi
ambapo mpaka sasa Tanzania inaongoza katika nchi za Afrika Mashariki na
ipo juu ya wastani wa ukuaji wa uchumi Barani Afrika” Alisema Bw. Zhang.
Ameishauri
Serikali kuendelea kushirikiana na Sekta binafsi katika ukuaji wa
Uchumi ili uchumi huo uwe endelevu. Aidha ameitaka Serikali kuwa na
mfumo shirikishi wa kifedha utakao wanufaisha wananchi wengi.
Naye
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), amesema
kuwa juhudi za Tanzania kwa sasa ni kuchochea ukuaji wa Kilimo na
kuongeza uzalishaji wenye tija.
“Umasikini
haujatatuliwa kwa kiwango ambacho Serikali ingependa kukiona, kwa kuwa
mpaka sasa watu walio katika umasikini na ukosefu wa huduma za lazima
ni takribani asilimia 34.4 “, aliongeza Dkt. Mpango
Kama
nchi imeamua kwenda kwenye uchumi wa kati na jambo ambalo linatiliwa
mkazo ni upatikanaji wa umeme wa kutosha na wenye bei nafuu .
Amesema
kuwa Serikali imefanya juhudi za kupeleka umeme mpaka vijijini lakini
bado kazi hiyo haijakamilika. Pia suala la miundombinu ya ya
usafirishaji ni changamoto, ukiwemo usafiri wa reli kutoka Mashariki
hadi Magharibi mwa nchi ambao ni wazamani na umeharibika.
“Serikali
imeamua kujenga Reli yenye kiwango cha Kimataifa (Standard gauge)
ambayo ni ya gharama, na kwa makadirio ya awali zinahitajika Dola
Bilioni 7.6, lakini umechukuliwa uamuzi huo ili kuharakisha
Maendeleo”aliongeza Dkt. Mpango.
“Tayari
tumeanza ujenzi wa reli hiyo kwa fedha za ndani kwa takribani Kilometa
200 kutoka Dar es salaam mpaka Morogoro na tutaendelea na ujenzi kadri
fedha zinavyo patikana” alifafanua Waziri Mpango .
Amesema
kuwa, kumekuwa na tatizo la ahadi za Wahisani kutotekelezwa kwa wakati
jambo linalofanya baadhi ya shughuli za maendeleo kutotekelezwa kwa
wakati.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF)
anaeziwakilisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba, alisema ni
vema Serikali ikaendelea kuangalia vipaumbele katika ujenzi wa
miundombinu ili iweze kuchochea uchumi.
“Suala
la ajira hasa kwa vijana linatakiwa kufanyiwa kazi na pia kuweka
mazingira mazuri ya uwekezaji na ufanyaji biashara kwa Sekta Binafsi kwa
kuwa Sekta Binafsi imekuwa na mchango mkubwa katika Maendeleo kwa nchi
nyingi Duniani” Alishauri Bw. Mkwezalamba.
Ameishauri
Tanzania kuendelea kuwekeza kikamilifu katika Sekta ya Elimu kwa kuwa
ni moja ya eneo ambalo kama likifanyiwa kazi kikamilifu litaleta Matokeo
chanya na ya haraka katika ukuaji wa Uchumi.
Akitoa
ufafanuzi wa hoja hizo, Waziri Mpango, amesema Serikali imeendelea
kuhakikisha kunakuwa na viwanda vingi ili vijana wengi waweze kupata
ajira. Aidha tayari Tanzania imeanza kutekeleza Elimu bure kuanzia
darasa la kwanza hadi kidato cha nne ili kutoa fursa kwa watu wengi
zaidi kupata elimu.
COMMENTS