MWALIMU COMMERCIAL BANK PLC (MCB), YAZINDUA KAMPENI YA WEKA AKIBA NA USHINDE, WATEJA KUONDOKA NA IPADS

  Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank PLC, Bw. Ronald Manongi, (katikati), akiwa na Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko...




 Afisa
Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank PLC, Bw. Ronald Manongi, (katikati), akiwa na Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko, Bw. Valence Luteganya, (kulia) na Meneja Masoko, Bi. Rahma Ngassa, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mei 18, 2017.







NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MWALIMU Commercial Bank PLC imezindua kampeni  ya
“Weka Akiba na Ushinde” kwa Wateja wake na wananchi kwa ujumla.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam leo Mei 18, 2017 wakati akizindua kampeni hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank PLC, Ronald Manongi alisema, “Draw
hiyo ipo wazi kwa wateja wote waliopo na watakaojiunga na sifa kubwa ya kuingia kwenye draw hiyo ni kwa mteja aliyepo au anayejiunga, kuweka akiba ya Shilingi
50, 000 au zaidi.” Alisema Bw. Manongi.
Akifafanua zaidi Afisa huyo Mtendaji Mkuu wa benki hiyo alisema, kampeni hiyo ambayo itawawezesha wateja kupata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali kila mwezi
kwa kipindi cha miezi miwili.
“Mteja anapoweka akiba (fedha), kiasi cha Shilingi 50,000 au zaidi, atapata alama, (Point) moja itakayomuwezesha kushiriki kwenye draw.” Alisema.
Alisema, kadiri Mteja anapoweka akiba zaidi ndivyo Anavyojiwekea nafasi nzuri ya kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo IPADS na vocha za manunuzi zenye thamani ya
Shilingi 100,000 na kwamba kila itakapochezeshwa draw hiyo, washindi wanane (4)
na kujishindia zawadi mbalimbali.
Akielezea hudma za benki hiyo, Manongi alifafanua
kuwa  Mwalimu Commercial Bank inatoa gharama nafuu na rafiki za kibenki na ni suluhisho la kifedha kwa walimu,
watumishi wa serikali na wananchi kwa ujumla na kutoa wito kwa Wateja wapya kuja kufungua Akaunti na kuweka akiba ili wapate nafasi ya kuingia kwenye draw hiyo.
Naye Mkuu wa kitengo cha Biashara na Masoko wa Benki
hiyo, Valence Luteganya alisema, “Huduma za kibenki za MCB ni bora na  nafuu, tunawahakikishia wateja wetu waje
kufanya maamuzi ya kifedha yaliyo sahihi kwani tunatoa huduma mbalimbali za kibenki zilizo nafuu.” Alisema na kuongeza kuwa MCB pia inatoa huduma za ATM
zilizounganishwa na mtandao wa Umoja switch ambao una ATM zaidi ya 200 nchi
nzima.
“Lakini si hivyo tu pia huduma bora za kibenki kupitia
simu za mkononi (Mobile Banking), huduma ya bure ya ujumbe wa SMS ukiwa na usalama na kuwawezesha wateja kupata taarifa za mara kwa mara kuhusiana na
Akaunti zao. Hivyo natoa wito kwa wananchi kwa ujumla kuja na kujiunga na Benki yetu kwa huduma bora na za uhakika.” Alisema.
   




 Bw. Manongi akizungumzia kampeni hiyo
 Mkuu wa kitengo cha Biashara na Masoko wa Benki hiyo, Valence Luteganya, akifafanua jinsi kampeni hiyo itakavyofanyika

 Meneja Masoko wa benki hiyo, Bi. Rahma Ngassa,(kushoto), akizungumzia ubora wa huduma za kibenki kwenye benki hiyo. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa MCB, Bw. Manongi
 Mkutano ukiendelea
 Waandishi wa habari wakiwa kazini
 Bw. Manongi akisikiliza maswali ya waandishi
 Bw. Manongi (kushoto), akiwa na Luteganya.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MWALIMU COMMERCIAL BANK PLC (MCB), YAZINDUA KAMPENI YA WEKA AKIBA NA USHINDE, WATEJA KUONDOKA NA IPADS
MWALIMU COMMERCIAL BANK PLC (MCB), YAZINDUA KAMPENI YA WEKA AKIBA NA USHINDE, WATEJA KUONDOKA NA IPADS
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiioOkIdgDglzj2xSFpGPRaebZ4E41EDW7DKDdpeuv0kbbnV5nfhx-9DYVZdKMhOh-n_uV0gJfME4IuyJoo4AQh2GKN6VqHsDpNFdYd8o4LpNxiyoMp6MYCzhXl-VfbxLBHPWYltOlOE30/s640/5R5A1930.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiioOkIdgDglzj2xSFpGPRaebZ4E41EDW7DKDdpeuv0kbbnV5nfhx-9DYVZdKMhOh-n_uV0gJfME4IuyJoo4AQh2GKN6VqHsDpNFdYd8o4LpNxiyoMp6MYCzhXl-VfbxLBHPWYltOlOE30/s72-c/5R5A1930.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/mwalimu-commercial-bank-plc-mcb.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/mwalimu-commercial-bank-plc-mcb.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy