MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI (WCF) WATOA ELIMU KWA WAAJIRI NCHI

Na Benjamin Sawe.     Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), umeendesha semina ya siku moja kwa waajiri nchini ili kutoa elimu juu ya sh...

Na Benjamin Sawe.
   
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), umeendesha semina ya siku moja kwa waajiri nchini ili kutoa elimu juu ya shughuli za Mfuko na wajibu wa waajiri kwa wafanyakazi wao katika kujisajili na kuwalipa michango kwa niaba ya waajiriwa wao.

Akizungumza katika semina hiyo Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko huo Radhimana Mbilinyi amesema kuanzishwa kwa mfuko huo kumekuja wakati muafaka ambapo Tanzania inaelekea katika uchumi wa viwanda hivyo kupelekea ongezeko la wafanyakazi ambapo chombo hicho ndio mkombozi wa majanga yatokanayo na kazi.                 

“Ni muda muafaka kwa waajiri kutambua wajibu wenu katika Mfuko huu na pia kutambua madhara ya kutotekeleza wajibu wenu” Alisema Radhimina Mbilinyi.

Katika hotuba yake, Bi Mbilinyi alieleza umuhimu wa waajiri kuwalipia michango wafanyakazi wake kama sheria inavyotaka, ili kuwawekea akiba pindi wapatapo na majanga wakiwa kazini.

Akizungumza wakati akitoa mada Afisa Matekelezo Bi. Amina Likungwala amesema, Mfuko umeamua kuandaa semina hiyo ili kutoa elimu zaidi kwa waajiri  kwa kutambua kuwa waajiri ndio wadau wakuu wa Mfuko huo na semina hiyo itawasaidia kujua kazi za Mfuko lakini pia wajibu wa waajiri kwa wafanyakazi katika kutoa michango ya kila mwezi.

Naye, Afisa Madai wa Mfuko huo, Grace Tarimo, alisema, Mfuko huo upo kisheria ili kutoa fidia kwa wafanyakazi watakaoumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi.

Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi ni Taasisi ya Serikali chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na umeundwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi Sura ya 263 iliyorejewa Disemba, Mwaka 2015.
Makamu Mwenyekiti  kutoka Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi  (WCF)  Radhimina Mbilinyi akifungua Semina ya uelimishaji kwa Waajiri kuhusu haki na wajibu wa mwajiri na mfanyakazi jijini Dar es Salaam Mei 29 2017.
Afisa Matekelezo Mwandamizi  kutoka Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) akitoa mada katika semina ya uelimishaji kwa Waajiri kuhusu haki na wajibu wa mwajiri na mfanyakazi jijini Dar es Salaam jana.

Mkurugenzi  wa Huduma za Tiba na Tathmini kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt. Abdullssadaam Omary akitoa mada katika semina ya uelimishaji kwa waajiri kuhusu haki na wajibu wa mwajiri na mfanyakazi jijini Dar es Salaam jana.

Baadhi ya washiriki wa semina ya uelimishaji kwa waajiri wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi wa semina hiyo ambaye ni Makamu Mwenyekiti  wa Bodi ya  Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Radhimina Mbilinyi jijini Dar es Salaam jana.



 

 


COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI (WCF) WATOA ELIMU KWA WAAJIRI NCHI
MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI (WCF) WATOA ELIMU KWA WAAJIRI NCHI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEizGpBCyQb20hQMYOB9RRiMjQkPwCdWuQ0LnjKFQcuPj0reKCUcZ8elAh0V9SLZQ5ssjn4dWGdV2YavDvGawd84g4x9xpFR3T6GlJNi3qTMBml-4zYW8w4XYHSGwmJer5KkFH82dJHoehk/s640/WCF+1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEizGpBCyQb20hQMYOB9RRiMjQkPwCdWuQ0LnjKFQcuPj0reKCUcZ8elAh0V9SLZQ5ssjn4dWGdV2YavDvGawd84g4x9xpFR3T6GlJNi3qTMBml-4zYW8w4XYHSGwmJer5KkFH82dJHoehk/s72-c/WCF+1.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/mfuko-wa-fidia-kwa-wafanyakazi-wcf.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/mfuko-wa-fidia-kwa-wafanyakazi-wcf.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy