Mjumbe wa Bodi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt. Francis Michael akifungua Semina ya uelimishaji kwa Waajiri kuhusu...
Mjumbe
wa Bodi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt. Francis Michael
akifungua Semina ya uelimishaji kwa Waajiri kuhusu haki na wajibu wa
mwajiri na mfanyakazi jijini Morogoro leo. Kulia ni Mwanasheria
Mwandamizi Irine Mungu.
Mwanasheria
Mwandamizi, Irine Mungu kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF)
akitoa mada kwa waajiri kuhusu haki na wajibu wa mwajiri na mfanyakazi
jijini Morogoro leo.
Afisa
Uhusuano Mwandamizi kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) akitoa
mada katika semina ya uelimishaji kwa waajiri kuhusu haki na wajibu wa
mwajiri na mfanyakazi mkoani Morogoro leo.
Fabian Felician akichangia mada katika semina ya uelimishaji kwa
waajiri kuhusu haki na wajibu wa mwajiri na mfanyakazi iliofanika mkoani
Morogoro leo.
Afisa
Kazi Mfawidhi mkoa wa Morogoro, Simbo Swai akichangia mada katika
semina ya uelimishaji kwa waajiri kuhusu haki na wajibu wa mwajiri na
mfanyakazi iliyofanyika mkoani Morogoro leo.
Hilda Msemo kutoka Mzinga Corporation akichangia mada katika semina ya
uelimishaji kwa waajiri kuhusu haki na wajibu wa mwajiri na mfanyakazi
iliyofanika mkoani Morogoro leo.
Baadhi
ya washiriki wa semina ya uelimishaji kwa waajiri wakiwa katika picha
ya pamoja na mgeni rasmi wa semina hiyo ambaye ni Mjumbe wa Bodi wa
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt. Francis Michael mkoani
Morogoro leo.
Mfuko
wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), umeendesha semina ya siku moja kwa
waajiri nchini katika mikoa minne, ili kutoa elimu juu ya shughuli za
Mfuko na wajibu wa waajiri kwa wafanyakazi wao katika kujisajili na
kuwalipa michango kwa niaba ya waajiriwa wao.
Akizungumza katika semina hiyo mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko Dkt. Francis Michael.
Amesema
kuanzishwa kwa mfuko huo kumekuja wakati muafaka ambapo Tanzania
inaelekea katika uchumi wa viwanda hivyo kupelekea ongezeko la
wafanyakazi ambapo chombo hicho ndio mkombozi wa majanga yatokanayo na
kazi.
“Ni
muda muafaka kwa waajiri kutambua wajibu wenu katika Mfuko huu na pia
kutambua madhara ya kutotekeleza wajibu wenu” Alisema Dkt. Michael.
Katika
hotuba yake, Dkt. Michael alieleza umuhimu wa waajiri kuwalipia
michango wafanyakazi wake kama sheria inavyotaka, ili kuwawekea akiba
pindi wapatapo na majanga wakiwa kazini.
Mfuko
wa Fidia kwa wafanyakazi ni Taasisi ya Serikali chini ya Ofisi ya
Waziri Mkuu na umeundwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia
kwa wafanyakazi Sura ya 263 iliyorejewa Desemba, Mwaka 2015.
Dkt.
Michael amesema, Mfuko umeamua kuandaa semina hiyo ili kutoa elimu
zaidi kwa waajiri kwa kutambua kuwa waajiri ndio wadau wakuu wa Mfuko
huo na semina hiyo itawasaidia kujua kazi za Mfuko lakini pia wajibu wa
waajiri kwa wafanyakazi katika kutoa michango ya kila mwezi.
Akitoa
mada juu ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, Afisa Uhusiano Mwandamizi
wa Mfuko huo, Sebera Fulgence, alisema, Mfuko huo upo kisheria ili kutoa
fidia kwa wafanyakazi watakaoumia, kuugua ama kufariki kutokana na
kazi.
Naye
Mwanasheria Mwandamizi wa Mfuko huo Bi.Irene Mungure amesema, ni muda
mwafaka kwa waajiri kutambua wajibu wao katika mfuko ikiwa ni pamoja na
kutambua madhara ya kutokutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa Sheria.
Katika
uzinduzi wa semina hizo jana Makao Makuu ya Nchi Dodoma, Mwenyekiti wa
Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Emmanuel
Humba, alifafanua zaidi juu ya haja ya waajiri kuufahamu vizuri Mfuko
namna unavyoendeshwa ikiwa ni pamoja na kulipa fidia kwa wafanyakazi
watakaoumia, kuugua ama kufariki. Aidha, alisema kuwa waajiri ni wadau
wakuu wa uendelezaji Mfuko.
Bw.
Humba aliwaasa waajiri kutokufanya udanganyifu na ubadhilifu hasa
katika uwasilishwaji wa michango kwani itakuwa ni kuudidimiza Mfuko na
ni kosa kisheria na waajiri watakaojihusisha watachukuliwa hatua za
kisheria kwa mujibu wa Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi Sura ya 263
iliyorejewa Desemba, Mwaka 2015.
Semina hiyo imefanyika katika mikoa ya Dodoma,Kilimanjaro, Morogoro na Arusha.
COMMENTS