MAREKANI YAAHIDI KUWAJENGEA UWEZO WANAWAKE NA VIJANA WA ZANZIBAR

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.  Abdalla Juma  Saadala ” Mabodi” akizungumza na Mkurugenzi wa taasisi ya Kimarekani i...

MABOD
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.  Abdalla Juma  Saadala ” Mabodi” akizungumza na Mkurugenzi wa taasisi ya Kimarekani inayoshughulikia masuala ya Demokrasia duniani (NDI), Dkt. Keith Jenningspamoja na ujumbe wake
……………………………………………………………..
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM  Zanzibar, Dkt. Abdalla Juma Sadala  amefanya  mazungumzo na Mkurugenzi wa Taasisi ya kimarekani inayoshughulikia masuala ya Demokrasia Duniani (NDI), kanda ya mashariki na kusini mwa afrika, Dkt. Keith Jennings, huko Afisi kuu ya CCM   Kisiwandui Zanzibar.
Katika mazungumzo hayo Naibu Katibu Mkuu huyo alieleza kwamba CCM imekuwa mdau mkubwa wa kutekeleza dhana ya demokrasia kwa vitendo, sambamba na kutoa fursa za uongozi kwa makundi yote ya kijamii.
Alisema ujio wa taasisi hiyo Zanzibar utafungua fursa mbali mbali kwa vijana na wanawake kupata ujuzi wa kukabiliana na changamoto za kisiasa na kiuchumi.
Pia  Dkt. Mabodi aliishauri  Taasisi hiyo kufungua Ofisi hapa nchini kwa lengo la kuratibu masuala mbali mbali yakiwemo kuwapatia Vijana fursa za kimasomo nchini marekani ili waweze kujifunza na kupata ujuzi wa fani zinazokubalika katika soko la ajira hapa nchini.
“Vijana na Wanawake wa Zanzibar wanakabiliwa na changamoto ya upungufu wa ajira, hivyo taasisi yenu ikitoa fursa za mafunzo ya ujasiria mali itasaidia kukabili tatizo hilo.”, alisema Dkt. Mabodi.
Naye Mkurugenzi wa taasisi ya kimarekani inayoshughulikia masuala ya Demokrasia duniani (NDI), kanda ya mashariki na kusini mwa afrika, Dkt. Keith Jennings alieleza kuwa taasisi hiyo inajishughulisha na masuala ya Demokrasia na kutoa mafunzo ya  ujasiria mali kwa vijana na wanawake duniani.
Dkt. Keith alisema kuwa lengo la ziara hiyo ni taasisi hiyo kujitambulisha kwa CCM Zanzibar na kubadilishana mawazo yatakayosaidia kufanya kazi za kisiasa kwa pamoja.
” Taasisi yetu imekuwa ikitoa mafunzo ya ujasiriamali pamoja na mbinu za kutumia fursa zinazopatikana katika mifumo ya Kidemokrasia  kwa vijana na wanawake, hivyo tunatarajia hata kwa Zanzibar makundi hayo yatanufaika na mpango huo.”, alieleza Dkt. Keith.
Dkt. Keith alisema  Zanzibar ina historia kubwa  ya kisiasa hivyo taasisi hiyo ina dhamira ya kuwajengea uwezo vijana mbali mbali hapa nchini ili waweze kutumia vizuri fursa zilizopo katika michakato ya kidemokrasia.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAREKANI YAAHIDI KUWAJENGEA UWEZO WANAWAKE NA VIJANA WA ZANZIBAR
MAREKANI YAAHIDI KUWAJENGEA UWEZO WANAWAKE NA VIJANA WA ZANZIBAR
http://fullshangweblog.com/home/wp-content/uploads/2017/05/MABOD.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/marekani-yaahidi-kuwajengea-uwezo.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/marekani-yaahidi-kuwajengea-uwezo.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy