Napenda kuungana na mamilioni ya Watanzania kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Joseph Magufuli...
Napenda
kuungana na mamilioni ya Watanzania kumpongeza Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Joseph Magufuli kwa uzalendo na
mapenzi ya dhati anayoonyesha kivitendo kwa Wananchi na Taifa kwa ujumla
kwa kuhakikisha analinda rasilimali, Mali, haki na maslahi.
Hivi
karibuni Rais Magufuli alizuia makontena 277 yenye mchanga wa madini
kusafirishwa kwenda nje ya nchi na kuunda kamati kuchunguza hasara au
faida tuliyokuwa tukiipata Watanzania kutokana na kusafirisha mchanga
huo ambapo kamati imewasilisha taarifa ya awali imeonyesha thamani ya
makontena hayo 277 ni Tsh. Bilioni 112.1 kumbe thamani halisi ni Tsh.
Trilioni 1.44. Taarifa hiyo imeonyesha hayo makontena tu tulikuwa
tumepoteza zaidi ya Tsh. Bilioni 829.4 ambapo kwa mwaka mmoja tu
tulikuwa tukipoteza Trilioni 25 ambayo Serikali ilikuwa haipati hata
senti moja.
Kupitia
mchanga huo tu tulikuwa tukiibiwa hivyo kwa takribani miaka 18 huku
tukipoteza Tsh. Trilioni 829.4 sawa na bajeti ya miaka 26 ya Tsh
Trilioni 32 kwa kila mwaka.
Tunapoteza
pesa hizo huku tukiangalia mahospitali hayana madawa, miundombinu
mibovu, mishahara haikidhi, tunakopa kukamilisha bajeti ya nchi maumivu
ambayo hatukustahili kabisa kuyapata sisi Watanzania.
Ahsante
sana Rais Magufuli kwa kuonyesha uzalendo wa kuzuia unyonyaji na
uhujumu uchumi huu wa kikatili uliokuwa ukiendelea nchini. Ni viongozi
wachache sana Afrika waliosalia wenye kariba ya uzalendo kama alionao
Rais Magufuli.
Huu
ni mwendelezo wa uzalendo wa kivitendo unaoonyesha na Rais Magufuli.
Tukumbuke ni Rais Magufuli huyu huyu anasimamia vyema upotevu wa mapato
bandarini, kuzuia matumizi ya ovyo Serikalini ya kodi za Wananchi kwa
kufuta safari za nje, kulipana posho zisizo na tija na kupunguza
matumizi ya kawaida kwa kuongeza fedha zaidi kwenye matumizi ya
kimaendeleo.
Kiukweli
ninaiona Tanzania mpya ikijengwa na uzalendo alionao Rais Magufuli kwa
Watanzania na Taifa kwa ujumla. Watendaji, viongozi na Wananchi yatupasa
tuige Uzalendo wa Rais wetu mpendwa Dk. John Pombe Magufuli kwa
kuungana nae kupambana na wahujumu uchumi wa nchi yetu.
Rais
Magufuli fanya uliyotumwa na wanyonge usiogope wanaojiita wachambuzi
ambao kila kitu hukuchambua kinyume, hao ni changamoto ya wewe kusonga
mbele!
Tunakuombea Rais Magufuli ulinzi, Baraka, hekima na busara zaidi toka kwa Mwenyezi Mungu.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu mbariki Rais wetu Dk. Magufuli.
Na Emmanuel J. Shilatu
25/05/2017
0767488622
COMMENTS