DC SHINYANGA AFUNGA MAFUNZO YA MAAFISA WATENDAJI ,AWATAKA KUKATAA MIRADI WASIYOITAMBUA

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiongea na maafisa watendaji wa mitaa,vitongoji,vijiji na kata kuwasihi wawe chachu ya ma...



Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiongea na maafisa watendaji wa mitaa,vitongoji,vijiji na kata kuwasihi wawe chachu ya maendeleo kwa kushirikiana kikamilifu na madiwani wao ili kuwaletea maendeleo wananchi huku akiwataka kukataa miradi wasiyoielewa katika maeneo yao.



Matiro ameyazungumza hayo leo May 24,2017 wakati akifunga mafunzo ya siku mbili ya maafisa watendaji wa mitaa,vitongoji,vijiji,kata na maafisa tarafa katika manispaa ya Shinyanga yaliyolenga kuwajengea uwezo katika utendaji wao yaliyofanyika katika ukumbi wa Lewis Kalinjuna katika manispaa hiyo.


Matiro aliwataka maafisa watendaji kuwa makini na miradi inayoanzishwa katika maeneo yao ili kuepuka kwenye lawama na migogoro inayoepukika na kukwamisha maendeleo katika jamii.


“Tunahitaji kuwa na ushirikianona kufanya kazi kwa umoja,nitasikitika sana kuona mradi unapelekwa kwenye kata yako lakini afisa mtendaji hauufahamu,ikitokea hivyo ukatae huo mradi kwani inapotokea mradi huo unaharibika atakayeulizwa ni wewe,kwa hiyo lazima ujue vyema mradi uliopo katika eneo lako ili kuepuka shida”,alieleza Matiro. 

“Nilishawaambia hata wataalamu wa halmashauri zetu kuwa wanapokwenda kwenye kata au vijiji wawashirikishe maafisa watendaji kwa wao ndiyo wasimamizi wakuu wa miradi lakini mnaweza kusimamia miradi hiyo ikiwa mnaitambua na miradi ambayo hamuitambui ikataeni”,aliongeza Matiro. 

Katika hatua nyingine alisema serikali haitasita kuchukua hatua kwa watendaji watakaoisababishia serikali hasara kupitia fedha mbalimbali zinazotolewa na serikali kwa ajili ya maendeleo. 

Aidha Matiro aliwasisitiza maafisa watendaji hao kusimamia vyema suala la ukusanyaji wa mapato na kusimamia vyema suala la ulinzi na usalama katika maeneo yao. 

Matiro alitumia fursa hiyo kuwakumbusha maafisa watendaji kutatua matatizo ya wananchi kwa kuhakikisha kuwa wanatenga siku maalum za kusikiliza kero za wananchi. 

Naye Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi aliwataka maafisa watendaji hao kusimamia vyema utaratibu wa kusoma mapato na matumizi kwa wakati. 

Mwangulumbi pia aliwaagiza maafisa watendaji kutoa ushirikiano kwa maafisa ardhi wakati wa kupima ardhi,kutunza mali za ofisi na kukusanya mapato katika maeneo yote ya biashara.

Nao washiriki wa mafunzo hayo walisema yawasaidia kiutendaji kwani wamejifunza mambo mbalimbali ikiwemo wajibu wao,umuhimu wa kufuata taratibu za kazi,kusimamia miradi,uandishi sahihi wa vitabu na nyaraka za serikali,masuala ya ulinzi,rushwa na tahadhari ya majanga ya moto.


MSIKILIZE HAPA CHINI MKUU WA WILAYA YA SHINYANGA JOSEPHINE MATIRO AKIZUNGUMZA WAKATI WA KUFUNGA MAFUNZO YA MAAFISA WATENDAJI NA MAAFISA TARAFA


ANGALIA PICHA WAKATI WA MAFUNZO YA MAAFISA WATENDAJI NA MAAFISA TARAFA KATIKA UKUMBI WA LEWIS KALINJUNA

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya siku mbili kwa maafisa watendaji wa mitaa,vitongoji,vijiji na kata pamoja maafisa tarafa wa manispaa ya Shinyanga katika ukumbi wa Lewis Kalinjuna leo May 24,2017-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika ukumbi wa Lewis Kalinjuna.Kulia ni mwenyekiti wa mafunzo hayo Simon Mpaname.Wa kwanza kushoto ni Afisa Utumishi wa Manispaa ya Shinyanga Magadi Magezi akifuatiwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo
Washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisisitiza jambo ukumbini
Maafisa mbalimbali wa manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza ukumbini
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini
Afisa Utumishi wa Manispaa ya Shinyanga Magadi Magezi akizungumza ukumbini
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi wakati wa kufunga mafunzo hayo
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi akisisitiza jambo ukumbini
Mwenyekiti wa mafunzo hayo Simon Mpaname akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo.
(Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog)

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: DC SHINYANGA AFUNGA MAFUNZO YA MAAFISA WATENDAJI ,AWATAKA KUKATAA MIRADI WASIYOITAMBUA
DC SHINYANGA AFUNGA MAFUNZO YA MAAFISA WATENDAJI ,AWATAKA KUKATAA MIRADI WASIYOITAMBUA
https://1.bp.blogspot.com/-SPA5a7aMuh0/WSWnKRmb5YI/AAAAAAAAPSE/onn-PNFRHMYO6OMQRkKa-iq51C-fxeyzgCLcB/s640/Malunde%2B%25287%2529.JPG
https://1.bp.blogspot.com/-SPA5a7aMuh0/WSWnKRmb5YI/AAAAAAAAPSE/onn-PNFRHMYO6OMQRkKa-iq51C-fxeyzgCLcB/s72-c/Malunde%2B%25287%2529.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/dc-shinyanga-afunga-mafunzo-ya-maafisa.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/dc-shinyanga-afunga-mafunzo-ya-maafisa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy