BENKI YA NMB YAZINDUWA 'FANIKIWA ACCOUNT' KWA WAFANYABIASHARA WADOGO

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kushoto) pamoja na Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya NMB, Jam...

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kushoto) pamoja na Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya NMB, James Meitaron (wa pili kulia) wakifunua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa NMB FANIKIWA ACCOUNT leo jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Meneja Mwandamizi Kitengo cha Biashara, Donatus Richard akishuhudia.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (katikati) akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa NMB FANIKIWA ACCOUNT uliofanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya NMB, James Meitaron kushoto ni Meneja Mwandamizi Kitengo cha Biashara, Donatus Richard akiwa katika mkutano huo.

Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya NMB, James Meitaron akifafanua jambo katika uzinduzi wa 'NMB FANIKIWA ACCOUNT'. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker na Meneja Mwandamizi Kitengo cha Biashara, Donatus Richard (kushoto).
BENKI ya NMB imezindua akaunti mpya kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati ijulikanayo kama 'NMB FANIKIWA ACCOUNT' ili waweze kukua kibiashara pamoja na kupata maendeleo ya biashara wanazozifanya.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa akaunti hiyo ya wafanyabiashara wadogo na wakati, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Ineke Bussemaker, alisema kuwa akaunti hiyo haina masharti magumu wakati wa kuifungua pamoja na uendeshaji wake hivyo kuwataka wafanyabiashara wote kuitumia.
Alisema kuwa NMB imebuni akaunti hiyo kutokana na kuwepo kwa changamoto ya wafanyabiashara wadogo kukosa mikopo na kukabiliwa na riba kubwa kwenye mikopo. Akifafanua zaidi juu ya bidhaa hiyo, Mkuu wa Idara ya Biashara, James Meitaron alisema Benki ya NMB imeweza kufikia kila kundi katika kuwanufaisha wafanyabiashara wadogo hasa kimikopo ambapo imewanufaisha katika kuendeleza biashara zao.
Alisema Benki ya NMB imekuwa ikifanya kazi kwa ukaribu na serikali pamoja na taasisi zake, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha inawakuza wafanyabiashara wadogo na wakati wakiwemo 'mama lishe'.

Mkutano huo ukiendelea.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kulia) akizungumza na mmoja wa wateja wa Benki ya NMB kushoto.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: BENKI YA NMB YAZINDUWA 'FANIKIWA ACCOUNT' KWA WAFANYABIASHARA WADOGO
BENKI YA NMB YAZINDUWA 'FANIKIWA ACCOUNT' KWA WAFANYABIASHARA WADOGO
http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2017/05/IMG_1127.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/benki-ya-nmb-yazinduwa-fanikiwa-account.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/benki-ya-nmb-yazinduwa-fanikiwa-account.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy