BALOZI SEIF ALI IDD AONGOZA MAZISHI YA MAMA MZAZI WA VUAI ALI VUAI

NA IS-HAKA OMAR,  ZANZIBAR. MAMIA ya Wananchi wameudhuria mazishi ya Mama mzazi wa Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM Zanzibar.Vuai Al...

NA IS-HAKA OMAR,  ZANZIBAR.


MAMIA ya Wananchi wameudhuria mazishi ya Mama mzazi wa Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM Zanzibar.Vuai Ali Vuai, Marehemu Bi.Mwanaisha Hassan Vuai huko Kijijini kwao Bwejuu, Mkoa wa Kusini Unguja.


Mazishi hayo yameongozwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, aliyeambatana na viongozi mbali mbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  pamoja na  jamhuri ya muungano Tanzania.


Bi. Mwanaisha amefariki jana wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Tasakhtaa  iliyopo  Vuga  Mjini  Zanzibar.


Akizungumza mara baada ya mazishi hayo, Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM Zanzibar, Nd. Vuai Ali Vuai alisema kifo cha Mama yake mzazi kimeacha pengo kubwa katika  familia hiyo  kwani marehemu huyo alikuwa akitegemewa na jamii kutokana na busara zake.


Aidha  Vuai amewashukru wananchi mbali mbali waliojitokeza kumuunga mkono katika mazishi hayo na kuwasihi waendelee kuwa na umoja wa kushirikiana katika mambo mbali mbali ya kijamii.


“  Mama yetu tulimpenda sana lakini ndio hivcyo amefariki sasa kilichobaki kwetu sisi tuliobaki ni kumuombea dua yeye pamoja na wazee wetu wengine waliofariki kabla yake.”, alisema  Naibu Katibu Mkuu huyo.


Mbali na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Balozi Seif Ali Idd pia  Mazishi hayo yameudhuriwa na Viongozi  mbali mbali  wakiwemo Katibu Mkuu wa CCM   Abdulrahman Omar Kinana, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar   Dkt. Abdalla Juma Saadala “ Mabodi”,Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Tanzania Shaka Hamdu Shaka,  Mkuu wa Mkoa kusini Unguja    Dk.Idrissa  Muslim Hija, Katibu  wa Kamati Maalum  ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi Zanzibar, Waride Bakari  Jabu.


Viongozi wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja, Idrissa  Kitwana  Mustafa, Mnadhimu wa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi  wa CCM, Ali Salum Haji pamoja na baadhi ya Mawaziri, Manaibu Mawaziri  na Makatibu wakuu wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


 Bi.Mwanaisha Hassan Vuai amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 85 ameacha watoto tisa (9) pamoja na wajukuu kadhaa.


Mungu ailaze roho ya marehemu pahali pema peponi-Amin.




 Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balosi Seif  Ali Idd akipokelewa na viongozi mbali mbali wa Chama na Serikali mara baada ya kuwasili katika mazishi ya Mama mzazi wa Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Zanzibar  Vuai Ali Vuai, huko kijijini kwao Bwejuu.
 Viongozi  mbali mbali wa Chama na serikali pamoja na wananchi wakiiombea Dua  Maiti ya Bi. Mwanaisha Hassan Vuai ambaye ni Mama mzazi wa Naibu Katibu Mkuu Msitaafu wa CCM Zanzibar  Vuai Ali Vuai katika msikiti wa kijiji cha Bwejuu.
 Viongozi  mbali mbali wa Chama na serikali pamoja na wananchi wakiiombea wakiwa msikitini kabla ya kuanza kuiswalia Maiti ya Bi. Mwanaisha Hassan.
 Baadhi ya Viongozi na wananchi kwa upande wa wanawake wakiomba dua katika mazishi ya Marehemu Bi. Mwanaisha Hassan Vuai ambaye ni Mama mzazi wa Naibu Katibu Mkuu Msitaafu wa CCM Zanzibar  Vuai Ali Vuai katika msikiti wa kijiji cha Bwejuu.
 Matukio tofauti ya kubebwa kwa maiti inapotolewa msikiti hadi sehemu ya kaburi ilipofanyiwa mazishi.
Viongozi mbali mbali wa Chama na serikali wakiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Nd. Abdulrahman Omar Kinana wakimfariji Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM  Zanzibar  katika mazishi ya Mama yake mzazi yaliyofanyika huko kijijini kwao Bwejuu, Mkoa wa Kusini Unguja. (Picha na Ofisi ya CCM Zanzibar)

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: BALOZI SEIF ALI IDD AONGOZA MAZISHI YA MAMA MZAZI WA VUAI ALI VUAI
BALOZI SEIF ALI IDD AONGOZA MAZISHI YA MAMA MZAZI WA VUAI ALI VUAI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh-mw-s40qAuaGDPT1vH3xTO_zjBoxIS3zxReiOi0fjf8zUV90ZuLcN-o-_LBdFP6ooFKNg_sdghDVxKJpYyyoO0pLrJ-7jfSJ4StbwL3fn2bO4v60_7B460euUstqFT3vn8xzTfyF1tmrw/s640/01.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh-mw-s40qAuaGDPT1vH3xTO_zjBoxIS3zxReiOi0fjf8zUV90ZuLcN-o-_LBdFP6ooFKNg_sdghDVxKJpYyyoO0pLrJ-7jfSJ4StbwL3fn2bO4v60_7B460euUstqFT3vn8xzTfyF1tmrw/s72-c/01.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/balozi-seif-ali-idd-aongoza-mazishi-ya.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/balozi-seif-ali-idd-aongoza-mazishi-ya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy