WATUMISHI SEKTA YA UJENZI WAPEWA SOMO

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (Wa pili kulia), akizungumza na wafanyak...




Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (Wa pili kulia), akizungumza na wafanyakazi wa Wizara hiyo pamoja na wawakilishi kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi, Mkoani Morogoro. 



Katibu wa Baraza la Wafanyakazi (Sekta ya Ujenzi), Bw. Ramadhani Msafiri(Wa pili kushoto), akifafanua jambo kwa wafanyakazi wa Wizara hiyo pamoja na Wawakilishi kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi, Mkoani Morogoro.

Mmoja wa wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Bw. Shukuru Sikunjema, akitoa maoni yake kwa Mwenyekiti Wa Baraza la Wafanyakazi Eng. Joseph Nyamhanga katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi, Mkoani Morogoro.

Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) wakifuatilia maelekezo ya Baraza la Wafanyakazi wakati wa kikao hicho kilichofanyika Mkoani Morogoro.

Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Wakiimba nyimbo ya ‘Solidarity forever’ kuonyesha mshikamano katika utendaji kazi wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi, Mkoani Morogoro.

Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunga kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika Mkoani Morogoro.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng.Joseph Nyamhanga, amewataka watumishi wa Wizara hiyo kutekeleza majukumu yao kwa weledi na uadilifu ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya Serikali ya Awamu ya Tano.


Akisoma hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Profesa Makame Mbarawa, katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi leo, mkoani Morogoro, Eng. Nyamhanga, ametoa wito kwa watumishi wote kushirikiana kwa pamoja katika kutekeleza majukumu yao ili kuleta tija kwa Serikali na Taifa kwa ujumla.


"Naliomba baraza hili la wafanyakazi kuhakikisha linahamasisha watumishi wote wa Wizara kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili, weledi na ushirikiano ili kuleta ufanisi", amesema Eng.Nyamhanga.


Aidha, Eng. Nyamhanga amelisisitiza Baraza hilo kuandaa mkataba wa kupima utendaji kazi wa watumishi katika majukumu yao ya kila siku ili kupima ufanisi wa watumishi hao kuanzia ngazi ya juu hadi ya chini.


Katibu Mkuu Nyamhanga , amelitaka Baraza hilo kuweka mazingira maalum kwa watumishi ikiwemo kuandaa mpango wa mafunzo ya ndani na nje ya nchi ili kuongeza ujuzi kwa watumishi wa Wizara hiyo.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Tawi la Ujenzi, Samuel Mticco, amemhakikishia Katibu Mkuu huyo kutekeleza maagizo yote yaliyosemwa katika Baraza hilo ikiwemo la uandaaji wa mkataba wa utendaji kazi kwa watumishi.


Kikao hicho cha siku moja cha Baraza la wafanyakazi la Sekta ya Ujenzi pamoja na mambo mengine kimekubaliana kupunguza matumizi ya fedha za Serikali yasiyo ya lazima pamoja na kupambana na vitendo vya ufisadi na rushwa.


(Imetolewa na kitengo cha mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano)

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WATUMISHI SEKTA YA UJENZI WAPEWA SOMO
WATUMISHI SEKTA YA UJENZI WAPEWA SOMO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjd6SrPzkGDzbEtI6Y0TlFW72ko_VQ73ZpT0BAP84QA73nEfDWkQQYVhFOSx9wSF3zxRvIR_QY3f_KTGSnVDxQVYpeXbUOq0wnfu3hrjasV1Mqu6dkwyT2euNjm1dFiiLc9JY841LB0UrKd/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjd6SrPzkGDzbEtI6Y0TlFW72ko_VQ73ZpT0BAP84QA73nEfDWkQQYVhFOSx9wSF3zxRvIR_QY3f_KTGSnVDxQVYpeXbUOq0wnfu3hrjasV1Mqu6dkwyT2euNjm1dFiiLc9JY841LB0UrKd/s72-c/1.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/watumishi-sekta-ya-ujenzi-wapewa-somo.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/watumishi-sekta-ya-ujenzi-wapewa-somo.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy