WATANZANIA WATAKIWA KUENDELEA KUIAMINI SERIKALI-MAJALIWA

Asisitiza vyombo vya dola vipewe muda wa kufanya uchunguzi wa matukio ya kihalifu. WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania ku...





Asisitiza vyombo vya dola vipewe muda wa kufanya uchunguzi wa matukio ya kihalifu.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kuendelea kuiamini Serikali yao na kuvipa muda vyombo vya dola kuendelea kufanya uchunguzi dhidi ya matukio mbalimbali ya kihalifu yaliyotokea nchini ili kubaini chanzo cha matatizo na wahusika.

Aidha, Waziri Mkuu ametoa wito kwa Watanzania wote kuendelea na utamaduni wa kushirikiana na vyombo vya dola kwa kutoa taarifa pindi vinapotokea vitendo vya kihalifu au viashiria vyake katika maeneo mbalimbali nchini.


Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Aprili 20, 2017) Bungeni mjini Dodoma katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu wakati akijibu swali la Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Freeman Mbowe aliyetaka kupata kauli ya Serikali juu ya hofu iliyotawala nchini kuhusu vitendo vya watu kuuliwa, kupotea na kutekwa.


Waziri mkuu amesema “tukitoa taarifa mapema tunaweza kuharibu upelelezi, tuviachie vyombo vetu vya dola viendelee kufuatilia kuona nani anayesababisha vitendo hivyo na dosari iko wapi na nini chanzo chake alisisitiza,”.


Kadhalika Waziri Mkuu amewasii Watanzania kuendeleza utamaduni mzuri wa watu kuheshimiana, kufuata kanuni na kuviachia vyombo vya dola kutekeleza majukumu yake. “Moja ya majukumu ya Serikali ni kuhakikisha Watanzania wanaishi kwa amani kwa kuwa na ulinzi wa uhakika kwao wenyewe na mali zao wakati wote,”.


Hata hivyo, Mheshimiwa Mbowe aliishauri Serikali kushirikiana na vyombo vya kiuchunguzi vya kimataifa kuchunguza tukio la kupotea kwa msaidizi wake Ben Saanane lililotokea miezi sita iliyopita, ambapo Waziri Mkuu amesema kuwa Taifa lina mahusiano mazuri na mataifa mbalimbali na inashirikiana nayo katika mambo mbalimbali likiwemo suala ya ulinzi ambapo si rahisi kuainisha namna wanavyoshirikiana.


Waziri Mkuu ameongeza kuwa vyombo vyetu vina weledi,vifaa na uwezo wa kutosha kufanya uchunguzi juu mambo yanayotokea nchini hivyo amesisitiza wananchi kuendelea kuiamini kwani matukio haya ya kihalifu likiwemo la mtu kutoweka au kufariki na haina kikomo cha uchunguzi, mara zote uchunguzi unategemeana na aina ya tukio lenyewe au mazingira lilipo tokea


Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali inafanya mapitio kwa vyama vyote vya Ushirika nchini kufuatia baadhi ya vyama hivyo kuwa na mwenendo mbaya hali inayochangia upotevu wa fedha nyingi na kukatisha tamaa wakulima.


Amesema hivi karibuni katika kikao cha wadau wa zao la korosho kilichofanyika wilayani Bagamoyo Bodi ya Korosho ilidaiwa kuhusika na ubadhilifu wa sh. bilioni 30 ambapo Serikali iliunda timu maalumu ya uchunguzi na kubaini upotevu wa sh. bilioni sita na siyo sh. bilioni 30.


Hata hivyo amesema kwamba hasara hiyo ya sh. bilioni sita haikusababishwa na bodi bali vyama vikuu na vya ushirikika vilivyopo kwenye ngazi ya Kata na wilaya, ambavyo vyote vilifanyiwa uchuguzi na hatua zimeanza kuchukuliwa.


Amesema matatizo hayo yako katika vyama vyote vya ushirika hususan vya mazao ya Tumbaku, Kahawa,Pamba, Chai na mazao mengine makuu, ambapo Serikali imeanza kupitia taarifa za ukaguzi kwa kina ili iweze kufanya ukaguzi na sasa wanaendelea na uchunguzi wa chama kikuu cha tumbaku.


Waziri Mkuu amesema wakimaliza kufanya uchunguzi katika chama kikuu cha tumbaku watachunguza vyama vingine vya pamba, kahawa na chai lengo likiwa ni kuwalinda wakulima na kuhakikisha wanapata tija. “Naomba kusisitiza hatua zinaendelea kuchukuliwa na tutaendelea kuimarlisha na ushirika,”.


Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mheshimiwa Mama Salma Kikwete aliyetaka kujua hatua zilizochukuliwa na Serikali kuhusu ubadhirifu wa sh. bilioni 30 uliofanywa na Bodi ya Korosho nchini.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S.L.P 980, DODOMA
ALHAMISI, APRILI 20, 2017.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali bungeni mjini Dodoma, Aprili 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza swali wakati alipoulizwa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, (kulia) bungeni mjini Dodoma, Aprili 20, 2017. 




 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai  akimuapisha Mhe. Dkt Getrude Rwakatare kuwa Mbunge.
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai  akimkabidhi Mhe. Dkt Getrude Rwakatare vifaa vya kazi mara baada ya kumuapisha kuwa Mbunge leo Aprili 20, 2017 Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai  akiongoza kikao cha kumi cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 20, 2017.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akijibu maswali ya wabunge katika kikao cha kumi cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 20, 2017. 
 Naibu Waziri wa Afya maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt Hamisi Kigwangalla akijibu maswali ya wabunge katika kikao cha kumi cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 20, 2017.
 Mbunge wa Kuteuliwa Mhe. Salma Kikwete akiuliza swali  katika kikao cha tisa  cha Mkutano wa kumi wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 20, 2017.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  Mhe. Suzan Kolimba akijibu maswali ya wabunge mbalimbali  katika kikao cha kumi cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 20,2017. 
 Mbunge wa Mafinga Mjini (CCM) Mhe Cosata David Chumi  akiuliza swali  katika kikao cha kumi cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 20, 2017.
 Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Stella Manyanya akijibu maswali ya wabunge mbalimbali  katika kikao cha kumi cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 20,2017. 
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Isack Kamwele akijibu maswali ya wabunge mbalimbali  katika kikao cha kumi cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 20,2017. 
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Ashatu Kijaji akijibu maswali ya wabunge mbalimbali katika kikao cha kumi cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 20, 2017.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akimsikiliza Mbunge wa Igunga Mhe. Dalali Kafumo wakati wakijadiliana jambo katika kikao cha kumi cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 20, 2017. 
Wabunge wakifuatilia hoja mbalimbali katika kikao cha kumi cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 20, 2017. (Picha na Raymond Mushumbusi Dodoma MAELEZO)

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WATANZANIA WATAKIWA KUENDELEA KUIAMINI SERIKALI-MAJALIWA
WATANZANIA WATAKIWA KUENDELEA KUIAMINI SERIKALI-MAJALIWA
https://i.ytimg.com/vi/N2sqSOxuyos/hqdefault.jpg
https://i.ytimg.com/vi/N2sqSOxuyos/default.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/watanzania-watakiwa-kuendelea-kuiamini.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/watanzania-watakiwa-kuendelea-kuiamini.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy