WANAWAKE KANISA LA PENTEKOSTE WAOMBA AMANI ILIYOPO NCHINI IDUMISHWE

  Mwenyekiti wa Muungano wa Wanawake wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (MMPT) Misheni ya Kijitonyama,  Maines Mhama (kulia), akimkab...




 Mwenyekiti wa Muungano wa Wanawake wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (MMPT) Misheni ya Kijitonyama,  Maines Mhama (kulia), akimkabidhi maua mgeni rasmi wa maadhimisho ya siku ya wanawake wa kanisa hilo, Anitha Mshighati (katikati), mara baada ya kuwasili kwenye sherehe hiyo iliyofanyika Kanisa la Pentekoste la Kituo cha Tabata Kisiwani Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mchungaji Ibrahim Mshighati mume wa mgeni rasmi.



Hapa ni furaha tupu wakati mgeni rasmi akisindikizwa kuingia kanisani
 Mgeni rasmi Anitha Mshighati akizungumza katika maadhimisho hayo.
  Mwenyekiti wa Muungano wa Wanawake wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (MMPT) Misheni ya Kijitonyama,  Maines Mhama akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
 Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Pentekoste Kituo cha Tabata Kisiwani, John Shusho akiwa kwenye maombi wakati wa maadhimisho hayo.
 Kwaya ya Kanisa hilo Kituo cha Tabata Kisiwani ikitumbuiza
 Nyimbo za kusifu zikiendelea.


 Kwaya ya Tabata Kisiwani ikiimba. 


Kwaya ya Kijitonyama ikiimba.
 Kwaya ya Gongo la Mboto ikifanya vitu vyake
 Kwaya ya Kipawa haikuwa nyuma kutoa burudani
 Mwimbaji wa nyimbo za injili wa kujitegemea, Joyce Agato akiwajibika
 Mwenyekiti wa Muungano wa Wanawake wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (MMPT) Misheni ya Kijitonyama,  Maines Mhama (kushoto), akiwa na wageni wake mgeni rasmi na mumewe.
 Ibada ikiendelea.
 Ni kuimba nyimbo za kusifu na kucheza.
 Mwenyekiti wa Wanawake Maines Mhama akitoa neno la maadhimisho hayo.
 Katibu Msaidizi wa Wanawake wa Kanisla hilo, Joyce Agato akimkabidhi risala mgeni rasmi.


Na Dotto Mwaibale

WANAWAKE  wametakiwa kuwa chachu ya kujenga  amani nchini badala ya kusubiri iharibike.

Mwito huo umetolewa Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na Mwenyekiti wa Muungano wa Wanawake wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (MMPT) Misheni ya Kijitonyama,  Maines Mhama wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake kwa kanisa hilo.

"Wanawake tunapaswa kuwa wa kwanza kujenga amani ya nchi kuanzia kwenye familia zetu kwani inapokosekana waathirika wakubwa ni sisi na watoto wetu" alisema Mhama.

Alisema amani inapokoseka shughuli zote haziwezi kufanyika nchini ikiwa pamoja na kuabudu hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuitunza kwani inapopotea gharama ya kuirudisha inakuwa kubwa.

Akiongelea matukio yanayotokea nchini ya watu kuuana kama yaliyotokea Kibiti mkoani Pwani kwa askari nane kuuana alisema wanadamu wanapaswa kumrudia mungu bila kujali itikadi za dini.

"Matukio ya kuuana yaliyoibuka hivi karibuni yatakwisha kwa watu kuwa na hofu ya mungu na si vinginevyo" alisema Mhama.

Mgeni rasmi kwenye sherehe hizo,  Anitha Mshighati aliwataka wanawake kuungana katika masuala mbalimbali na kuanzisha shughuli za ujasiriamali ili waweze kujikomboa kiuchumi.

"Wanawake serikali imetuwekea miundombinu mizuri ya kufanya shughuli zetu tutumie fursa hiyo kujianzishia miradi mbalimbali ili tuweze kufanya mambo makubwa ya kiuchumi" alisema  Mshighati.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni kuitafuta amani na kuidumisha.

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WANAWAKE KANISA LA PENTEKOSTE WAOMBA AMANI ILIYOPO NCHINI IDUMISHWE
WANAWAKE KANISA LA PENTEKOSTE WAOMBA AMANI ILIYOPO NCHINI IDUMISHWE
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhLP3KEQDbyjZi0Xu0LHiNi1OmChXtqrBRFewBx9NoZPHAqZR88tiGkuP36v3n8-tKHNMxfRMqo6VvnoHQ4tB-KcnqbyirED9pVaGzycIvtQVJNUWlYnzPvMwr2u_prdnyJjwf7S_Y8aANy/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhLP3KEQDbyjZi0Xu0LHiNi1OmChXtqrBRFewBx9NoZPHAqZR88tiGkuP36v3n8-tKHNMxfRMqo6VvnoHQ4tB-KcnqbyirED9pVaGzycIvtQVJNUWlYnzPvMwr2u_prdnyJjwf7S_Y8aANy/s72-c/1.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/wanawake-kanisa-la-pentekoste-waomba.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/wanawake-kanisa-la-pentekoste-waomba.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy