WAFANYAKAZI WA KUJITOLEA WA KIMAREKANI WA HAMSINI NA MOJA WA SEKTA ZA AFYA NA KILIMO WAAPISHWA LEO

Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam TANZANIA 19 Aprili, 2017 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI WAFANYAKAZI WA KUJITOLEA WA K...




Ubalozi wa Marekani
Dar es Salaam
TANZANIA
19 Aprili, 2017
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

WAFANYAKAZI WA KUJITOLEA WA KIMAREKANI WA PEACE CORPS HAMSINI NA MOJA (51) WA SEKTA ZA AFYA NA KILIMO WAAPISHWA
Wafanyakazi wa kujitolea wa Kimarekani wa Peace Corps wapatao 51 wamekula kiapo cha utumishi wa miaka miwili nchini Tanzania katika hafla maalum iliyofanyika leo katika ofisi za Peace Corps jijini Dar es Salaam. Wafanyakazi hawa watakaohudumu katika sekta za afya na kilimo watapangiwa kufanya katika wilaya 20 nchini, ikiwa ni pamoja na wilaya za Iringa, Mufindi, Kondoa, Mbinga, Masasi, Ludewa, Lushoto, Songea, Kishapu, Makete na Singida vijijini. Wengine watapangiwa katika wilaya za Same, Njombe, Manyoni, Shinyanga vijijini, Mafinga, Makambako, Wanging’ombe, Mbeya na Lushoto.
Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Vincent Spera aliwaapisha wafanyakazi hao wapya wa kujitolea mbele ya mgeni rasmi, Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Huduma za Afya na Lishe katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dk. Athumani Amir Pembe, na Mkurugenzi Mkazi wa Peace Corps nchini Tanzania Dk. Nelson Cronyn.  Hafla hii ilihudhuriwa pia na waliowahi kuwa wafanyakazi wa kujitolea wa Peace Corps katika maeneo mbalimbali dunia, maafisa kutoka taasisi wabia na familia zilizowahifadhi wafanyakazi wapya wa kujitolea wakati wakiwa mafunzoni.  
Katika hotuba yake, Kaimu Balozi Spera aliieleza hafla hii kama sherehe ya kuthibitisha dhamira ya dhati ya wafanyakazi wa kujitolea kuhudumu na kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani.  “Serikali ya Marekani inafanya kazi katika maeneo yote – kuanzia utawala bora hadi maendeleo ya kiuchumi na usalama wa kikanda – lakini msingi wa kila tunachokifanya ni kuwasaidia watu wa Tanzania.  Tunafanya hivyo vyema zaidi pale panapokuwa na ushirikiano katika ngazi ya mtu na mtu. Dhamira hii hudhihirishwa kila siku na wafanyakazi wa kujitolea wa Peace Corps, wenyeji wao na wafanyakazi wenzao wa Kitanzania,” alisema Kaimu Balozi Spera.
Toka mwaka 1962, zaidi ya wafanyakazi wa kujitolea wa Peace Corps 2,850 wamehudumu nchini Tanzania. Peace Corps hutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa kujitolea wa Kimarekani wanaopangiwa kufanya kazi katika jamii wakihudumu katika nyanja za elimu ya sekondari (wakifundisha hisabati, sayansi na teknolojia ya Mawasiliano), afya na elimu ya mazingira.
Wafanyakazi wa kujitolea husaidia na kutoa mafunzo kuhusu utunzaji wa mazingira ikiwa ni pamoja na kuzuia kuharibika kwa ardhi, kulinda vyanzo vya maji, kuhifadhi ardhi na matumizi ya mbinu bora za kilimo na uhifadhi wa misitu (agro-forestry) wakiweka msisitizo katika kufanya kazi kwa ubia na wanawake na vijana. Pia watatoa mafunzo na kuwezesha kuanzishwa kwa kilimo hai cha bustani (bio-intensive gardens) ili kuongeza upatikanaji wa chakula, na kuboresha lishe ya kaya pamoja na shughuli nyingine za kujiongezea kipato.
Aidha, wafanyakazi hawa wa kujitolea husaidia katika kuimarisha afya ya umma kwa kufanya kazi na vituo, vikundi vya kijamii na vile vilivyomo mashuleni vinavyotoa huduma na elimu ya afya ikiwa ni pamoja na zile zinazohusu kujikinga dhidi ya VVU/UKIMWI, matibabu na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU/UKIMWI,yatima na watoto walio katika mazingira hatarishi. Wafanyakazi wa kujitolea hufanya kazi kwa karibu na kamati za afya vijiji ili kubaini na kuchambua mahitaji na vipaumbele vya jamii na kushiriki katika shughuli zinazohamasisha mabadiliko ya tabia katika maeneo ya afya ya mama na mtoto, lishe, malaria, maradhi yanayosababishwa na maji yasiyo salama, afya ya uzazi na kinga dhidi ya VVU/UKIMWI.
Peace Corps ni taasisi ya Serikali ya Marekani iliyoanzishwa na Rais John F. Kennedy mwaka 1961 ambayo hivi sasa inahudumia zaidi ya wafanyakazi wa kujitolea zaidi ya 8,000 katika zaidi ya nchi 60 duniani. Kwa miaka 56, Peace Corps imekuwa taasisi inayoendesha shughuli za mabadilishano ya kiufundi na kitamaduni zisizoegemea mrengo wowote wa kisiasa na kidini. Zaidi ya wafanyakazi wa kujitolea 189,000 wamehudumu katika nchi 140. Peace Corps ina dhamira ya kukuza amani na urafiki duniani kwa kutekeleza malengo matatu yafuatayo:
  • Kutoa wafanyakazi wa kujitolea wa Kimarekani watakaochangia kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika nchi itakayohitaji wafanyakazi hao;
  • Kukuza uelewa kuhusu Wamarekani miongoni mwa watu katika jamii zinazohudumiwa na Wafanyakazi wa kujitolea;
  • Kuimarisha uelewa wa Wamarekani kuhusu dunia na watu wake.
Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na Ofisi ya Habari ya Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam kwa simu namba: +255 22 229-4000 au kwa barua pepe: DPO@state.gov.

Sehemu ya wafanyakazi wa kujitolea wakicheza na kuimba wimbo wakati wa hafla ya kula kiapo jijini Dar es Salaam leo. Kwa kipindi cha miaka miwili wafanyakazi hao 51 watakuwa wakifanya kazi kwenye sekta za Afya na Kilimo katika wilaya nchini Tanzania.

SOME of the new Peace Corps Volunteers taking their oath of service before the United States Chargé d’Affaires, a.i., Vincent Spera (not pictured) in a swearing-in ceremony held at the Peace Corps office in Dar es Salaam today. The ceremony was graced by Dr Athumani Amir Pembe, Acting Assistant Director of Health Services and Nutrition in the President's Office - Regional Administration and Local Government. For two years, the 51 new  Peace Corps Volunteers will work in the health and agriculture sectors in 20 districts across Tanzania


U.S. Embassy Dar es Salaam
TANZANIA
April 19, 2017
FOR IMMEDIATE RELEASE

U.S. PEACE CORPS SWEARS IN FIFTY-ONE (51)
HEALTH AND AGRICULTURE VOLUNTEERS
Fifty-One Peace Corps Volunteers (PCVs) committed to two years of service in a swearing-in ceremony at the Peace Corps office in Dar es Salaam today.  The volunteers, who will work in the health and agriculture sectors, will be stationed in 20 districts across Tanzania, including Iringa, Mufindi, Kondoa, Mbinga, Masasi, Ludewa, Lushoto, Songea, Kishapu, Makete, Singida Rural, Same, Njombe, Manyoni, Shinyanga Rural, Mafinga, Makambako, Wanging’ombe, Mbeya, and Lushoto.  
Chargé d’Affaires, a.i., Vincent Spera administered the official oath of service to the new volunteers in the presence of the guest of honor, Dr. Athumani Amir Pembe, Acting Assistant Director of Health Services and Nutrition in the President's Office Regional Administration and Local Governments, as well as Tanzania Peace Corps Country Director Dr. Nelson Cronyn.  Former PCVs from around the world, officials from partner volunteer agencies, and families who hosted volunteers also attended the ceremony.  
In his remarks, Chargé Spera described the swearing-in ceremony as a celebration of volunteers’ commitment to service and the durable partnership between Tanzania and the United States.  “The U.S. Government works across all areas – from governance to economic development to regional security – but the core of everything we do is focused on helping the Tanzanian people.  We do that best at the individual, person-to-person level, and Peace Corps Volunteers and their hosts and counterparts make that vision a reality every day,” he told the audience.
More than 2,850 PCVs have served in Tanzania since 1962.  The Peace Corps provides trained American volunteers who work with communities in the fields of secondary education (math, science, and information and communications technology), health promotion, and environmental education.
The volunteers offer assistance and training on environmental education, including land degradation, preserving water catchments, soil conservation and implementation of agro-forestry techniques, and emphasize partnership with women and youth. Volunteers also offer bio-intensive gardens to promote household food security, as well as a variety of income-generating activities.
The volunteers also help strengthen public health by working with youth, health service providers, and community groups to promote healthy behaviors, including HIV/AIDS prevention, and care and support for people living with HIV/AIDS, orphans and vulnerable children. The volunteers work closely with village health committees to analyze community needs and priorities and promote behavior change in areas of maternal and child health, nutrition, malaria, waterborne diseases, sexual and reproductive health, and HIV/AIDS prevention.
Founded in 1961 by President John F. Kennedy, the Peace Corps is a U.S. Government agency that supports about 8,000 volunteers in more than 60 countries. For 56 years, Peace Corps has maintained apolitical and non-sectarian ideals of technical and cultural exchange. More than 189,000 volunteers have served in 140 countries. Peace Corps promotes world peace and friendship by fulfilling three fundamental goals:
  • Providing American volunteers who contribute to the social and economic development of interested countries;
  • Promoting a better understanding of Americans among the people who volunteers serve;
  • Strengthening Americans' understanding of the world and its peoples.
To request more information, please call the U.S. Embassy Dar es Salaam Press Office at Tel: +255 22 229-4000 or email: DPO@state.gov.
******************
 

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAFANYAKAZI WA KUJITOLEA WA KIMAREKANI WA HAMSINI NA MOJA WA SEKTA ZA AFYA NA KILIMO WAAPISHWA LEO
WAFANYAKAZI WA KUJITOLEA WA KIMAREKANI WA HAMSINI NA MOJA WA SEKTA ZA AFYA NA KILIMO WAAPISHWA LEO
https://lh3.googleusercontent.com/O2J1MYxHj0v9NtFgWkkeIezmPlX-Afi6jhbXfdPWpbFnuIWoaPVyI9fg7H4yt6dfycNtAoRo80f-SgWEWliW247oDYk2QlHpmOhgWmy8iz-w5zakfL-MQSsDEkTrfDjNaPgSbaHPsJdbpHvegA
https://lh3.googleusercontent.com/O2J1MYxHj0v9NtFgWkkeIezmPlX-Afi6jhbXfdPWpbFnuIWoaPVyI9fg7H4yt6dfycNtAoRo80f-SgWEWliW247oDYk2QlHpmOhgWmy8iz-w5zakfL-MQSsDEkTrfDjNaPgSbaHPsJdbpHvegA=s72-c
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/wafanyakazi-wa-kujitolea-wa-kimarekani.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/wafanyakazi-wa-kujitolea-wa-kimarekani.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy