WAAJIRI TEKELEZENI SHERIA YA KAZI ILI KULINDA HAKI ZA WAFANYAKAZI-NAIBU WAZIRI MAVUNDE.

Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA. Waajiri wote nchini yakiwemo makampuni ya Madini wametakiwa kutekeleza matakwa ya Sheria ya ...


Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.


Waajiri wote nchini yakiwemo makampuni ya Madini wametakiwa kutekeleza matakwa ya Sheria ya kazi kwa lengo la kulinda haki za wafanyakazi.


Hayo yamesemwa na Naibu Waziri  Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Ajira Kazi na watu wenye Ulemavu  Mhe. Anthony Mavunde wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge leo Mjini Dodoma.


“Makampuni haya yana wajibu mkubwa wa kulinda haki za wafanyakazi,kupunguza migogoro isiyo ya lazima sehemu za kazi na kuongeza tija na uzalishaji mahala pa kazi.”Aliongeza Mhe.Mavunde.


Aidha amesema Ofisi yake imeendelea kutekeleza majukumu yake ya usimamizi wa Sheria kwa kufanya kaguzi sehemu za kazi kwa lengo la kuhakikisha kuwa waajiri wanazingatia matakwa ya Sheria,elimu ya Sheria za kazi inatolewa kwa waajiri,wafanyakazi na vyama vyao ili kuongeza uelewa wao katika kutekeleza Sheria.


Kuhusu ukaguzi wa mikataba kwa kampuni zinazofanya kazi migodini amesema  Serikali iliunda kikosi ambacho kilishirikisha Maafisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, NSSF, SSRA,OSHA ,Mamlaka ya Mapato Tanzania na Wakala wa Ukaguzi wa Madini.


Amesema kikosi kazi hiki kilipewa jukumu la kufanya ukaguzi wa kina kwenye migodi iliyopo kanda ya ziwa na kaskazini kwa lengo la kuangalia hali halisi ya utekelezaji wa Sheria za kazi,afya na usalama mahali pa kazi,masuala ya hifadhi ya jamii,fedha na kodi.


Pamoja na hayo amesema kuwa Serikali inatambua umhimu wa uwekezaji katika kukuza fursa za ajira kwa watanzania na kuchangia kukua uchumi kwa ujumla.


“Serikali itaendelea kusimamia sheria za kazi ili kuhakikisha kuwa waajiri wote nchini wanatimiza wajibu wao na wawekezaji wamepata nafasi ya kuwekeza na kuchangia kukua kwa uchumi wa nchi yetu kwa kufuata sheria zilizoko nchini”Alisisitiza Mhe. Mavunde.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAAJIRI TEKELEZENI SHERIA YA KAZI ILI KULINDA HAKI ZA WAFANYAKAZI-NAIBU WAZIRI MAVUNDE.
WAAJIRI TEKELEZENI SHERIA YA KAZI ILI KULINDA HAKI ZA WAFANYAKAZI-NAIBU WAZIRI MAVUNDE.
https://3.bp.blogspot.com/-GCQvr__68bk/WQHj2qGEkYI/AAAAAAADfnE/1NTR2bt9JQ8bc_rRhcIcN9KJIpVRxQ8oACLcB/s400/unnamed.jpg
https://3.bp.blogspot.com/-GCQvr__68bk/WQHj2qGEkYI/AAAAAAADfnE/1NTR2bt9JQ8bc_rRhcIcN9KJIpVRxQ8oACLcB/s72-c/unnamed.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/waajiri-tekelezeni-sheria-ya-kazi-ili.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/waajiri-tekelezeni-sheria-ya-kazi-ili.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy