TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

- Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Kitalu Na. 8, Mtaa wa Luthuli S.L.P 2643, DAR ES SALAAM Simu: +255 22 2135747/8; 2137...


-
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
Kitalu Na. 8, Mtaa wa Luthuli
S.L.P 2643, DAR ES SALAAM
Simu: +255 22 2135747/8; 2137125; 2135222
Faksi: +255 22 2111281
Tovuti: www.chragg.go.tz

Aprili 14, 2017
   
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

THBUB yalaani mauaji ya Askari Polisi 8 Mkoani Pwani

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imepokea kwa masikitiko taarifa ya kuuwawa kwa askari wanane (8) wa Jeshi la Polisi, katika tukio lililotekelezwa na watu wasiofahamika jioni ya Aprili 13, 2017 katika kijiji cha Jaribu Mpakani, Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inalaani vikali mauaji haya ya kikatili ya askari polisi waliokuwa kazini na wasiokuwa na hatia. Aidha, tunaungana na Watanzania wengine kuwapa pole familia za wafiwa na Jeshi la Polisi kwa ujumla.

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa matukio ya mauaji ya askari polisi na wananchi wengine maeneo tofauti Mkoani Pwani tangu mwaka 2015 yamekuwa yakiongezeka na kusababisha uvunjifu wa haki za binadamu, hususan haki ya uhai inayolindwa na Katiba ya nchi, na madhara mengine kwa familia za wahanga, kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Haki ya kuishi kama zilivyo haki nyingine, inalindwa kisheria, na pia inalindwa na mikataba mbalimbali ya kimataifa na kikanda ambayo Tanzania imeridhia. Hakuna mtu anayepaswa kuporwa haki hii ya msingi kiholela. Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) Ibara ya 14, kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata kutoka katika jamii hifadhi ya maisha yake, kwa mujibu wa sheria.

Ikumbukwe kwamba askari polisi wanapokuwa kazini wanatekeleza majukumu muhimu ya kulinda raia na mali zao, kwa hiyo usalama wao unategemewa na Watanzania wote. Yeyote yule anayewaua askari polisi siyo tu anataka kuwachonganisha askari polisi na raia, bali  pia anawaweka raia hao katika hofu kubwa ya usalama wao na mali zao.

Hivyo basi, kwa mara nyingine, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inashauri kwamba:
  1. Katika kuhakikisha kuwa haki ya kuishi ya askari polisi na wananchi wote inalindwa, Jeshi la Polisi na Serikali kwa ujumla wafanye uchunguzi wa kina ili kubaini sababu za mauaji haya kutokea kwa kujirudia Mkoani Pwani, na kuhakikisha wahusika wote wanapatikana na wanafikishwa kwenye vyombo vya sheria, ili sheria ichukue mkondo wake.

  1. Tume inawakumbusha wananchi kuwa vitendo vya ukatili, mauaji, na matendo yote yanayokiuka Sheria yanayofanywa na raia wasio wema ni ukiukwaji wa Sheria, haki za binadamu na misingi ya utawala wa sheira; Hivyo Tume inakemea matendo haya na kutaka yapigwe vita.

  1. Aidha, inawataka wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuhakikisha upelelezi wa matukio hayo unakamilika ili hatua za kisheria zichukuliwe kwa watakaobainika kuhusika na matukio haya.

Imetolewa na:
(SIGNED)
Bahame Tom Nyanduga
Mwenyekiti

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Aprili 14, 2017

Bahame Tom Nyanduga Mwenyekiti wa THBUB

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA
https://lh6.googleusercontent.com/7Bz-7zyukGRqnD2QLWLAMhmM-qwOTGXH9pt00MKglcNFGY1figAE5s8nxxSh8IEnorLgCh_inchi-gI69zLpqx3Y_oMKA7S8kFM3MKJAQXCpJjxIdP1ToUZbpY1u6g6Y70h-f6hxtSvBQXw7ZA
https://lh6.googleusercontent.com/7Bz-7zyukGRqnD2QLWLAMhmM-qwOTGXH9pt00MKglcNFGY1figAE5s8nxxSh8IEnorLgCh_inchi-gI69zLpqx3Y_oMKA7S8kFM3MKJAQXCpJjxIdP1ToUZbpY1u6g6Y70h-f6hxtSvBQXw7ZA=s72-c
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/tume-ya-haki-za-binadamu-na-utawala-bora.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/tume-ya-haki-za-binadamu-na-utawala-bora.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy