TAMKO LA SERIKALI; KUHUSU KUONGEZA MUDA WA KUBADILISHA CHETI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO TAARIFA KWA UMMA KUONGEZA MUDA WA KUBAD...

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
Tanzania Coat of Arms

TAARIFA KWA UMMA
KUONGEZA MUDA WA KUBADILISHA CHETI CHA CHANJO YA HOMA YA MANJANO
Tarehe 24 Novemba 2016 Wizara ilizindua Cheti kipya cha Chanjo za Kimataifa kijulikanacho kama Cheti cha Chanjo ya Homa ya Manjano ili kuendana na maboresho ya kipengele cha 7 cha Kanuni za Afya za Kimataifa za mwaka 2005. Lakini pia, zoezi hili lililenga kukabiliana na kusambaa kwa vyeti vya kugushi (feki) ambavyo  watu wamekuwa wakivipata bila kupata chanjo, hali ambayo ilitishia Afya ya Jamii dhidi ya ugonjwa huo. Kwasababu hizo, Wizara iliona ni vema kufanya mabadiliko ya cheti hicho, ambapo wenye vyeti vya zamani wanabadilishiwa na wale  wanaopata chanjo wanapewa cheti kipya.
Wizara inapenda kutoa taarifa ya utekelezaji wa zoezi hilo kama ifuatavyo. Kabla ya kuanza matumizi ya vyeti vipya, wastani wa wasafiri 800 walikuwa wanapatiwa chanjo kwa mwezi kupitia vituo vilivyoruhusiwa na Wizara. Baada ya kuzindua vyeti vipya na kuongeza udhibiti wa vyeti feki idadi ya wanaopata chanjo imeongeza kutoka 800 hadi 2,445 kwa mwezi ikiwa ni ongezeko la mara 3 ya waliokuwa wanachanja hapo awali. Ongezeko hili limesababishwa na wasafiri zaidi ya 1,644 kusalimisha vyeti feki kwa mwezi na kuchanjwa na kupewa vyeti halali.
Kwa ujumla tangu matumizi ya vyeti vipya vianze mwezi wa Agosti mwaka 2016 mpaka mwezi Machi 2017, jumla ya wasafiri 19,557 wamepatiwa chanjo ambapo kati yao 13,157 wamesalimisha vyeti feki na kupatiwa chanjo, hii ni sawa na asilimia 67.2. Halikadhalika, watu 11,644 wamebadilisha vyeti vyao halali vya zamani.
Kupata cheti bila kupata chanjo ni kosa na kunahatarisha afya yako na Afya ya Jamii, kwani ukienda katika nchi zenye hatari ya ugonjwa wa homa ya manjano, unaweza kuambukizwa kwasababu huna kinga na hatimaye kuleta ugonjwa huo nchini. Vile vile zoezi hili limebaini uwepo wa vituo vinavyotoa chanjo hii bila kuwa na kibali cha Wizara, hili ni kosa na hivyo ni marafuku kituo chochote kutoa chanjo hiyo hadi hapo vituo hivyo vitakapopata kibali. Aidha, kwa wale ambao wananunua au kutoa vyeti bila kupata chanjo nao wanatenda kosa hivyo, waache mara moja kwani mkono wa sheria utachukua mkondo wake.
Tarehe 16 Februari 2017 Wizara ilikumbusha kubadili vyeti vya zamani katika muda uliopangwa yaani Januari 1 hadi Machi 31, 2017. Kutokana na tathmini tuliyoifanya imeonekana kuwa watu wengi bado hawajabadili vyeti vya zamani na kutokana na umuhimu wa zoezi hilo kwa afya ya jamii, tumeamua kuongeza muda wa mwezi mmoja ili watu wapate nafasi ya kubadili vyeti vyao, hivyo zoezi hili litaendelea na litaitimishwa tarehe 30.04.2017. Wizara inatoa wito kwa watu ambao bado wana vyeti vya zamani kufika katika vituo vya kutolea huduma na kuvibadilisha. Baada ya muda huo kupita hakutakuwa na muda mwingine wa nyongeza.

Wizara inawakumbusha tena kuwa ugonjwa wa homa ya manjano haupo nchini ila kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, Tanzania ipo katika ukanda wa nchi zenye kiwango kidogo cha maambukizi ya ugonjwa huo (low risk country). Hata hivyo, tupo katika hatari ya kuupata ugonjwa huo kutokana na kuzungukwa na nchi zilizopo kwenye ukanda wa kiwango cha juu cha hatari ya ugonjwa huo (High risk countries). Hivyo ni jukumu la kila mtu kuhakikisha tunajilinda dhidi ya ugonjwa huo kuingia nchini.
Ugonjwa huu husambazwa na mbu jike aina ya Aedes aliye na virusi vya ugonjwa huo. Mpaka sasa duniani hakuna dawa ya kutibu ugonjwa huo na mgonjwa hupatiwa matibabu ya kupunguza maumivu au kutibu dalili zinazojitokeza. Njia pekee ya kujikinga na ugonjwa huu ni kupata chanjo dhidi ya ugonjwa huo. Chanjo hiyo huanza kufanya kazi kiufasaha siku kumi baada ya mtu kupata chanjo hiyo. Hivyo, nawasihi wanaosafiri kupata chanjo hiyo angalau siku kumi au zaidi kabla ya kusafiri kwenda kwenye nchi zenye maambukizi.  Aidha, kwa watu wasio na safari hawahitajiki kupata chanjo hiyo.
Vile vile, kwa wale ambao hawastahili kupata chanjo kwa sababu za umri (miaka 60 na kuendelea), wajawazito na watu wenye sababu za kiafya zilizothibitishwa na Daktari, watapatiwa cheti maalaumu kijulikanacho kama “International Vaccination Exemption certificate” pamoja na kupewa ushauri wa hatua za kiafya za kuchukua dhidi ya kujikinga na ugonjwa huo.
Mwisho, Wizara inapenda kuwashukuru wale wote walioitikia wito wa zoezi hili la kubadili vyeti kwani wamefanya hivyo kwa manufaa yao na ya Taifa. Halikadhalika, wale ambao hawajabadili vyeti vyao watumie muda huu wa nyongeza kufanya hivyo.

Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Afya
21-04-2017.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TAMKO LA SERIKALI; KUHUSU KUONGEZA MUDA WA KUBADILISHA CHETI
TAMKO LA SERIKALI; KUHUSU KUONGEZA MUDA WA KUBADILISHA CHETI
https://lh3.googleusercontent.com/CRclLFsmUXNF8vtcwoXu1ya7CCPXfUdSUjFZdgUuDKINliQ5WB9_Q66zeicD6Tr-52U50ntPGErjGKx18ifD5rSrpCVzl7U-RRprxFpP0q5VfWZH8GPaoMyNEIIgc5uCpqEeEF_w1SpYvh7qNg
https://lh3.googleusercontent.com/CRclLFsmUXNF8vtcwoXu1ya7CCPXfUdSUjFZdgUuDKINliQ5WB9_Q66zeicD6Tr-52U50ntPGErjGKx18ifD5rSrpCVzl7U-RRprxFpP0q5VfWZH8GPaoMyNEIIgc5uCpqEeEF_w1SpYvh7qNg=s72-c
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/tamko-la-serikali-kuhusu-kuongeza-muda.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/tamko-la-serikali-kuhusu-kuongeza-muda.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy