F RAIS MAGUFULI AMTEUA PROF. CHIBUNDA KUWA MAKAMU MKUU WA CHUO SUA, AWASILI DODOMA | RobertOkanda

Monday, April 24, 2017

RAIS MAGUFULI AMTEUA PROF. CHIBUNDA KUWA MAKAMU MKUU WA CHUO SUA, AWASILI DODOMA


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULUDescription: Description: Description: Description: Description: Coat of Arms
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz               

Faksi: 255-22-2113425


OFISI YA RAIS,
     IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ikulu, Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Raphael Tihelwa Chibunda kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Ikulu Jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa Uteuzi wa Prof. Raphael Tihelwa Chibunda unaanza leo tarehe 24 Aprili, 2017.
Kabla ya uteuzi huo Prof. Raphael Tihelwa Chibunda alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Sayansi na Teknolojia katika Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia.
Prof. Raphael Tihelwa Chibunda anachukua nafasi ya Prof. Gerald Monela ambaye amemaliza muda wake.
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewasili Mjini Dodoma ambako pamoja na mambo mengine atakuwa mgeni rasmi katika Sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Katika uwanja wa ndege wa Dodoma, Mhe. Rais Magufuli amepokelewa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa,  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Mhe. Jenister Mhagama na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana
Sherehe za Muungano mwaka huu, zitafanyika katika Uwanja wa Jamhuri ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika katika makao makuu ya nchi Mjini Dodoma.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
24 Aprili, 2017.Prof. Raphael Tihelwa Chibunda
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana (kushoto) mara baada ya kuwasili mkoani Dodoma leo. (Picha na Ikulu)


0 comments:

Post a Comment