RAIS MAGUFULI AAGIZA UONGOZI WA DODOMA KUUNDA KAMATI KUSHUGHULIKIA SUALA LA KUBADILI HATI ZA UMILIKI ARDHI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU Simu: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz T...


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz

Faksi: 255-22-2113425OFISI YA RAIS,
     IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 29 Aprili 2017, ameuagiza Uongozi wa Mkoa wa Dodoma kuunda kamati itakayoshughulikia suala la kubadilisha hati ya umiliki wa ardhi katika mkoa huo kutoka miaka 33 hadi miaka 99.
Rais Magufuli ametoa agizo hilo katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma wakati alipokutana na viongozi mbalimbali wa mkoa huo wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa.
Kamati hiyo itahusisha wajumbe kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Ofisi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Dodoma na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma - CDA.
Rais Magufuli amesema mji wa Dodoma pekee ndio wenye matatizo makubwa  ya umiliki wa ardhi kutokana na hati zake kutolewa kwa miaka 33 badala ya miaka 99 kama ilivyo miji mingine nchini kitu kunachorudisha nyuma maendeleo ya mji huo ikiwa ni pamoja na uwekezaji.
'' Dodoma bado kuna tatizo moja kubwa, katika viwanja vyote vinavyotolewa hapa hati zake ni za miaka 33, huwezi ukajenga nchi ya viwanda,huwezi ukamvutia muwekezaji ambaye hati yake ni miaka 33 na wakati anataka kwenda kukopa benki umpe garantii ya miaka 33,nafikiri hii sheria tulikosea sana na nafikiri hii ni moja ya sheria ambayo ilifanya hata viwanda vingi visijengwe hapa Dodoma'' amesema Rais Magufuli.
Katika hatua nyingine, Rais Magufuli ameridhia ombi la Chuo Kikuu cha Dodoma kusamehewa kulipa kodi ya ardhi ya zaidi ya shilingi Bilioni Mbili iliyokuwa inadaiwa na CDA na kuagiza kutodaiwa tena kwa kuwa chuo hicho hakifanyi biashara bali hutoa huduma kwa jamii.
''Chuo kikuu cha Dodoma hakifanyi biashara ,kipo pale kwa ajili ya kutoa elimu kwa watanzania na wengi wao ni watoto wa masikini ,ardhi zote kwa mujibu wa sheria namba nne na namba tano ya mwaka 1999 na sheria nyingine zote za ardhi zikiwemo zile za mabadiliko za mwaka 2007 mwenye Mamlaka makubwa ya kusimamia ardhi ni Rais,kulingana na misingi hiyo ili mradi tu hili lisichukuliwe kwa kila Taaasisi lakini nimetoa special offer kwa Chuo Kikuu cha Dodoma lile deni lisamehewe , wasidaiwe na wala wasiwadai tena'' amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli pia ameagiza Ujenzi wa Uwanja wa mkubwa wa michezo mkoani humo unaofadhiliwa na Mfalme wa Morocco ujengwe karibu na eneo la Nane Nane mkoani Dodoma.
Aidha, Rais Dkt. Magufuli amesema kuwa anataka uwanja huo  uwe mkubwa na wa kisasa utakaokidhi mahitaji ya kimataifa katika kipindi  cha zaidi ya  miaka 100 ijayo na hivyo atasimamia mwenyewe ujenzi huo.
Kwa upande wa ujenzi wa Uwanja wa ndege wa Dodoma,  Rais Magufuli ameagiza kufanywa tathmini ya nyumba zitakazo bomolewa kwa ajili ya upanuzi wa  Uwanja huo ili kulipwa fedha zao mara moja  hali itakayopelekea Uwanja huo ukidhi mahitaji ya kutua ndege za kimataifa.
Katika hatua nyingine Rais Magufuli amewashukuru Wananchi wa Mkoa wa Dodoma kwa ukarimu na makaribisho makubwa hususan katika sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika tarehe 26 Aprili mkoani humo.
Amesema Wananchi wa Dodoma wameonyesha ukarimu na uvumilivu wa hali ya juu hata pale mvua ilipokuwa inanyesha waliendelea kushuhudia sherehe hizo ni kitu ambacho cha kuigwa na wananchi wa mikoa mingine nchini.
Rais Magufuli ameondoka mkoani Dodoma kuelekea mkoa wa Kilimanjaro, ambapo pamoja na mambo mengine atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za sikukuu ya wafanyakazi Duniani, Mei Mosi.

Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Chamwino, Dodoma
29 Aprili, 2017

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RAIS MAGUFULI AAGIZA UONGOZI WA DODOMA KUUNDA KAMATI KUSHUGHULIKIA SUALA LA KUBADILI HATI ZA UMILIKI ARDHI
RAIS MAGUFULI AAGIZA UONGOZI WA DODOMA KUUNDA KAMATI KUSHUGHULIKIA SUALA LA KUBADILI HATI ZA UMILIKI ARDHI
https://lh6.googleusercontent.com/E-vK17bXQzf5TP3-W2pKbcOLewSpvZucD72TIOaHXpBqHKRshk6ETWF6ymZ526bHaURU6pmVPKnzlfdpmqBs5FgRhtUqb81ggdt2Pzc-ep7TiXbKA0rtLMqUaU50Q8z3gqQJnuIinVpnFvXvow
https://lh6.googleusercontent.com/E-vK17bXQzf5TP3-W2pKbcOLewSpvZucD72TIOaHXpBqHKRshk6ETWF6ymZ526bHaURU6pmVPKnzlfdpmqBs5FgRhtUqb81ggdt2Pzc-ep7TiXbKA0rtLMqUaU50Q8z3gqQJnuIinVpnFvXvow=s72-c
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/rais-magufuli-aagiza-uongozi-wa-dodoma.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/rais-magufuli-aagiza-uongozi-wa-dodoma.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy