RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA ZOEZI LA UHAKIKI WA VYETI KWA WATUMISHI WA UMMA MJINI DODOMA

  Na Nuru Juma na Beatrice Lyimo-MAELEZO . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka watumishi 9932 wal... 

Na Nuru Juma na Beatrice Lyimo-MAELEZO .

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka watumishi 9932 waliogushi vyeti, kuondoka maeneo yao ya kazi haraka iwezekanavyo kabla hawajadhibiwa kwa mujibu wa sheria.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo mjini Dodoma alipokuwa akikabidhiwa taarifa ya uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma sambamba na uzinduzi wa maadhimisho ya miaka kumi ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

“Watumishi 9932 wenye vyeti vya kugushi na feki mishahara yao ya mwezi huu ikatwe na waondoke kazini mara moja na hizo nafasi zitangwazwe ili wasomi waweze kuziomba na majina yao yawekwe kwenye magazeti ili wajulikane” amesema Rais Magufuli

Aidha amesema kuwa hadi kufika tarehe 15 Mei, 2017 kila mkuu wa Idara mahali pake pa kazi ahakikishe watumishi hao wameondoka na watakao kaidi agizo hilo amevitaka vyombo vya usalama kuwashughulikia.
Hata hivyo Rais Magufuli ameongeza kuwa watumisi 1538 wanaotumia cheti zaidi ya mtu mmoja kutopewa mshahara hadi pale itakapojulikana nani mwenye cheti halali na kuwataka watumishi 11,769 kuwasilisha vyeti vilivyopungua.

Mbali na hayo Rais Magufuli amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii na kuachana na masuala ya siasa kwa lengo la kujenga nchi kwani watanzania wanahitaji maendeleo.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Angela Kairuki amesema kuwa mpaka sasa vyeti vilivyohakikiwa ni 435,000 ambapo imefanyika kwa awamu tatu iliyojumuisha Serikali za Mitaa, Taasisi na Mashirika ya Umma, Tume na Ofisi ya Menejimenti ya Utumishi na Wakala wa Serikali pamoja na Serikali Kuu.

“Leo tunakabidhi taarifa ya awamu mbili iliyohusisha Serikali za Mitaa, Taasisi na Mashirika ya Umma, Tume na Ofisi ya Menejimenti ya Utumishi na Wakala wa Serikali ambapo imejumuisha uhakiki wa vyeti vya Kidato cha Nne, Sita, vyeti vya ualimu kwa ngazi ya cheti na stashahada” amesema Waziri Kairuki.

Amesema kuwa matokeo ya uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma yapo ya aina nne ambapo watumishi 376,969 sawa na asilimia 94.23 wanavyeti halali, watumishi 9932 asilimia 2.4 wanavyeti vya kugushi, watumishi 1538 asilimia 0.3 vyeti vyao vinatumika kwa zaidi ya mtu mmoja na watumishi 11,769 asilimia 2.8 wanavyeti pungufu.

Nae Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako alisema wizara yake inakumbana na changamoto ya watumishi wa umma kugushi vyeti hivyo aliwataka wanafunzi kusoma kwa bidii kwani serikali imeziba njia zote za mkato za kuajiriwa na Serikali.

“Leo tunaandika historia ya kipekee kwani suala la uhakiki wa yveti limefanyika kwa mara ya kwanza nchini ambapo Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ndio yenye jukumu la kuhakiki uhalali wa vyeti hivyo” amesema Prof. Ndalichako.

Zoezi la uhakiki wa vyeti kwa Watumishi wa Umma limeendeshwa na Serikali ya Awamu ya Tano kuanzia Mwezi Oktoba, 2016 likiwa na lengo la kubaini uhalali wa vyeti kwa watumishi wake. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akinyanyua juu Taarifa na vitabu vye majina 9,932 ya watumishi wenye vyeti vya kugushi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akihutubia viongozi mbalimbali, wanafunzi wa UDOM, pamoja na watumishi wa Umma mara baada ya kupokea Taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti  kwa watumishi wa umma kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Angela Kairuki katika Ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisoma moja ya  vitabu vya Taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti  kwa watumishi wa umma awamu ya kwanza alivyopokea kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angela Kairuki, (kulia) katika Ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma leo Aprili 28, 2017. Katikati ni Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti  kwa Watumishi wa umma kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Angela Kairuki katika Ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe na kufungua boksi kubwa lenye majina ya watumishi zaidi ya 9,932 waliobainika kuwa na vyeti vya kugushi mara baada ya kupokea Taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti  kwa watumishi wa umma kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Angela Kairuki katika Ukumbi wa Chimwaga mjini DodomaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa , Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako, Spika wa Bunge Job Ndugai, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Angela Kairuki wakiminya kitufe kuashiria maadhimisho ya miaka 10 ya Chuo Kikuu cha Dodoma UDOM katika ukumbi wa Chimwaga mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na watumishi mbalimbali wa umma, viongozi pamoja wanafunzi wa UDOM mara baada ya kumaliza kuhutubia katika Ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma.


Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia katika Ukumbi wa Chimwaga.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia katika hadhara hiyo katika Chuo kikuu cha Dodoma UDOM.Baadhi ya viongozi mbalimbali wakifatilia kwa makini Hotuba iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika maadhimisho ya miaka 10 ya Chuo cha UDOM toka kuanzishwa kwake.


Baadhi ya Makatibu wakuu pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali, wanafunzi pamoja na walimu wa  UDOM wakipiga makofi wakati wakimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akiwasili katika ukumbi wa Chimwaga mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya miaka 10 ya Chuo kikuu cha Dodoma UDOM kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Idris Kikula, katika ukumbi wa Chimwaga mkoani Dodoma. (PICHA NA IKULU)

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA ZOEZI LA UHAKIKI WA VYETI KWA WATUMISHI WA UMMA MJINI DODOMA
RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA ZOEZI LA UHAKIKI WA VYETI KWA WATUMISHI WA UMMA MJINI DODOMA
https://1.bp.blogspot.com/-Z5EHCvFhshM/WQNEpERqyUI/AAAAAAADfrs/fpgLD-E3Il07LSH7i9Fs-S9QdzjioYqiwCLcB/s640/unnamed.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-Z5EHCvFhshM/WQNEpERqyUI/AAAAAAADfrs/fpgLD-E3Il07LSH7i9Fs-S9QdzjioYqiwCLcB/s72-c/unnamed.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/rais-dkt-magufuli-apokea-taarifa-ya.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/rais-dkt-magufuli-apokea-taarifa-ya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy