RAIS DKT MAGUFULI AHUDHURIA IBADA YA JUMAPILI MAKANISA MAWILI TOFAUTI MJINI MOSHI

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitakiana amani na mmoja wa mapadre katika Kanisa la Kuu la Katoli...




 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitakiana amani na mmoja wa mapadre katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi Mjini alikohudhuria ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea Ekaristi Takatifu toka kwa Askofu Isaac Aman katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini alikohudhuria ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiungana na waumini  katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini katika ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
 Waumini wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli aliposalimia waumini katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini katika ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
 Waumini wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimia waumini katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini katika ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
 Waumini wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimia waumini katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini katika ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
 Waumini wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli aliposalimia waumini katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini katika ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiombewa na Askofu Isaac Aman katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini alikohudhuria ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiombewa na Askofu Isaac Aman katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini alikohudhuria ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiombewa na Askofu Isaac Aman katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini alikohudhuria ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na watawa katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini baada ya  ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na waumini katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini baada ya  ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
 Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Frederick Shoo akitoa mahubiri wakati wa ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo  Aprili 30, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na waumini wengine wakimsikiliza Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Frederick Shoo akitoa mahubiri wakati wa ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo  Aprili 30, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akikaribishwa na Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Frederick Shoo kuongea na wananchi baada ya  ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo  Aprili 30, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akikaribishwa na Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Frederick Shoo kuongea na wananchi baada ya  ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo  Aprili 30, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiongea na waumini na wananchi baada ya  ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo  Aprili 30, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiongea na waumini na wananchi baada ya  ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo  Aprili 30, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiombewa sala maalumu na Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Frederick Shoo kuongea na wananchi baada ya  ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo  Aprili 30, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  na Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Frederick Shoo pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meck Sadick wakati wa kuhitimisha ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo  Aprili 30, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiongozana na Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Frederick Shoo baada ya  ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo  Aprili 30, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Frederick Shoo, Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Muhagama, Askofu Mstaafu Evarist Kweka wakipata picha ya pamoja  baada ya  ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo  Aprili 30, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Frederick Shoo na Askofu Mstaafu Evarist Kweka baada ya  ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo  Aprili 30, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Frederick Shoo na Askofu Mstaafu Evarist Kweka na kiongozi mwingine baada ya  ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo  Aprili 30, 2017. (PICHA NA IKULU)
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz

Faksi: 255-22-2113425


OFISI YA RAIS,
     IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 30 Aprili 2017, ameungana na waumini wa dini ya Kikristo kusali ibada ya Jumapili katika Kanisa la Kiaskofu, Jimbo Katoliki la Moshi  ,Parokia ya Kristo Mfalme na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Moshi Mjini, Dayosisi ya Kaskazini mkoani Kilimanjaro na kuwataka waumini wa makanisa hayo na Watanzania kwa ujumla kuendeleza amani iliyopo nchini kwa kuwa ndio chachu ya Maendeleo.
Rais Magufuli amesema hatua zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya Tano zina lengo la kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli ya taifa linalomuamini MUNGU.
'' Napenda muniamini kuwa mimi nipo kwa niaba yenu, najua huu Urais si wangu, Urais mnao ninyi mlioamuwa nitumike kama mtumishi kwa wakati huu, nawaomba sana muendelee kuniweka katika sala zenu ili kazi hii ya Urais isinipe kiburi, nikawe mtumishi wa watu'' Amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli amewashukuru waumini wa makanisa hayo mawili na watanzania kwa ujumla kwa kusimama pamoja kuliombea Taifa amani iliyowezesha wananchi kupiga kura kwa amani katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na kutokana na sala zao Mwenyezi MUNGU akamuwezesha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha, Rais Magufuli ametoa msaada wa mifuko 100 ya Saruji kusaidia maendeleo ya kanisa Katoliki na Shilingi Milioni Moja kwa Kwaya ya Kanisa hilo ili irekodi nyimbo zake, halikadhalka katika Kanisa la KKKT, Mheshimiwa Rais ametoa mifuko 150 ya Saruji kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya Kanisa hilo na Shilingi milioni Moja kwa Kwaya ya Kanisa hilo.
Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama amemuunga mkono Rais Magufuli kwa Kuchangia Mifuko hamsini ya Saruji ambapo Mkuu wa Mkoa wa kilimanjaro Mhe. Said Meck Sadick amechangia mifuko hamsini ya Saruji na Shilingi laki Tano.
Kwa upande wake Askofu wa Jimbo Katoliki la Moshi ,Parokia ya Kristo Mfalme Askofu Isaac Amani amemshukuru Rais Magufuli kwa uwamuzi wa kusali kanisani hapo na kuwataka waumini wa kanisa hilo na Tanzania kwa ujumla kuendelea kumuombea yeye pamoja na Serikali yake ili iweze kuwatumikia Watanzania katika kuwaletea maendeleo na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya mfano kwa Bara la Afrika.
Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania - KKKT, Askofu Dr Fredrick Shoo amewataka waamini wa kanisa hilo na watanzania kwa ujumla kutokuwa na hofu kwa mambo yanayofanywa na Rais hususani katika kupambana na maovu, dhuluma na ufisadi vikiwemo na badala yake Watanzania wabadilike na kujijengea mazoea ya kufanya kazi halali na kuwa waaminifu na kuwa wazalendo kwa Taifa lao.
Aidha, Askofu Shoo amemuomba Dkt Magufuli kuangalia uwezekano wa kupunguza kodi hususani kwa taasisi za kidini zinzotoa huduma za kijamii zikiwemo zile za Elimu na Afya.
Akijibu Maombi hayo Rais Dkt Magufuli amewaeleza waamini na watanzania kwa ujumla kuwa Serikali inathamini michango ya huduma za kijamii zinazotolewa na Taasisi za dini na kuahidi kuliangalia suala hilo.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU.
Moshi, Kilimanjaro.
30 Aprili, 2017.


COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RAIS DKT MAGUFULI AHUDHURIA IBADA YA JUMAPILI MAKANISA MAWILI TOFAUTI MJINI MOSHI
RAIS DKT MAGUFULI AHUDHURIA IBADA YA JUMAPILI MAKANISA MAWILI TOFAUTI MJINI MOSHI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgzEsGvCexgzBvVee098S1jy9bqDvmzedJ6xYZt0KgdHwaUEuSz2iuX48V2YThnTiTcJXbBgdfoc_IA2luBahgozFPXMXXBV0-GbAH4REIlnkH2J8ICd5IcKrZXYgVMAlxrDnVURps6Btw/s640/m1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgzEsGvCexgzBvVee098S1jy9bqDvmzedJ6xYZt0KgdHwaUEuSz2iuX48V2YThnTiTcJXbBgdfoc_IA2luBahgozFPXMXXBV0-GbAH4REIlnkH2J8ICd5IcKrZXYgVMAlxrDnVURps6Btw/s72-c/m1.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/rais-dkt-magufuli-ahudhuria-ibada-ya.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/rais-dkt-magufuli-ahudhuria-ibada-ya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy