PAMBANO LA EL CLASICO; BARCA YAIFUNGA MADRID IKIWA PUNGUFU

NA K-VA BLOG NA MASHIRIKA YA HABARI LILE pambano la watani wa jadi nchini Hispania, (El Clasico), baina ya Real Madrid ...
NA K-VA BLOG NA MASHIRIKA YA HABARI
LILE pambano la watani wa jadi nchini Hispania, (El Clasico), baina ya Real Madrid na Barcelona la ligi kuu ya soka nchi humo maarufu kama Laliga, lilimalizika usiku wa kuamkia leo Aprili 24, 2017 kwa Barca kushinda mabao 3-2.
Hata hivyo Barca imeshinda Madridi ikiwa pungufu kufuatia mlinzi wake na nahodha wa timu hiyo, Sergio Ramos, kutolewa nje ka kadi nyekundu kufuatia rafu aliyomchezea mshambuliaji hatari wa Barca, Leonel Messi, zikiwa zimesalia si zaidi ya dakika 20 mpira kumalizika.
Pambano hilo lililokuwa la marudiano na kuchezwa kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu, Madrid ilikuwa ya kwanza kujipatia bao katika kipindi cha kwanza kupitia kwa kiungo wa kati wa timu hiyo Cacemiro, kufuatia mpira wa krosi uliopigwa na Marcello kutoka wingi ya kushoto.
Hata hivyo Barca ilisawazisha bao hilo dakika chache kabla ya mpira kwenda mapumziko kupitia kwa winga wake Ra
BAO la 500 la Lionel Messi limeipeleka Barcelona kwenye uongozi wa ligi kuu ya Hispania Laliga katika muda wa majeruhi dhidi ya wachezaji pungufu wa Real Madrid kwenye uwanja wa ugenini wa Santiago Bernabeu nchini Hispania usiku wa kuamkia leo Aprili 24, 2017
Ushindi wa mabao 3-2 wa El Clasico dhidi ya hasimu wake Madrid, unaifanya Barca kuwa na pointi sawa na Madrid lakini kwa rekodi nzuri ya kukabana koo kileleni.
Casemiro alifunga bao la kwanza na la kuongoza kabla ya Messi kusawazisha na Ivan Rakitic kuiweka Barcelona mbele huku Nahodha wa Madrid, Sergio Ramos, akionyeshwa kadi nyekundu kutokana na kumchezea vibaya Messi.
Kocha Mkuu wa Madrid, Zenadine Zidane, “Zizu” alifanya mabadiliko kwa kumuingiza James Rodriguez ambaye alifunga bao la kusawazisha, kabla ya Messi kufunga bao la ushindi kwenye muda wa majeruhi.
Licha ya kufungwa katika pambano hilo, bado ina faida mchezo mmoja mkononi ukilinganisha na Barca ambayo sasa imesaliwa na michezo mitano.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: PAMBANO LA EL CLASICO; BARCA YAIFUNGA MADRID IKIWA PUNGUFU
PAMBANO LA EL CLASICO; BARCA YAIFUNGA MADRID IKIWA PUNGUFU
https://4.bp.blogspot.com/-heet2tJoMbY/WP2KMP9wNXI/AAAAAAAA054/mEK5yo6U_hUmGd4Xg0iafclyKLqUKgKDwCLcB/s320/_95757372_messi_getty.jpg
https://4.bp.blogspot.com/-heet2tJoMbY/WP2KMP9wNXI/AAAAAAAA054/mEK5yo6U_hUmGd4Xg0iafclyKLqUKgKDwCLcB/s72-c/_95757372_messi_getty.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/pambano-la-el-clasico-barca-yaifunga.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/pambano-la-el-clasico-barca-yaifunga.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy