MKUU WA MKOA WA TANGA AKOLEZA VITA YA MADAWA YA KULEVYA

Tanga , MKUU wa Mkoa wa Tanga, Martin Shighela, amesema vita ya madawaya kulevya inaendelea hivyo kuviagiza vikosi vya ulinzi na usal...




Tanga, MKUU wa Mkoa wa Tanga, Martin Shighela, amesema vita ya madawaya kulevya inaendelea hivyo kuviagiza vikosi vya ulinzi na usalama kuhakikisha inawakamata vinara wa wasafirishaji na wauzaji.
Akizungumza katika hafla ya fupi ya makabidhiano ya jengo la Afya ya Akili Hospitali ya Rufaa ya Bombo lililokarabatiwa na Kituo cha Tanga International Comperence Centre (TICC), Shighela alisema vita ya madawa itakuwa endelevu.
Alisema vijana wengi wamekuwa wakiathirika na matumizi ya madawa ya kulevya na Taifa kukosa nguvu kazi ya kuleta maendeleo na kuviagiza vyombo vya  ulinzi na usalama kuhakikisha Tanga hakuna njia ya upitishaji.
“Kuna wagonjwa wa akili kutokana na maumbile yao lakini kuna wagonjwa wengine wa akili wa kujitakia ambao sababu zake ni matumizi ya madawa ya kulevya” alisema Shighela na kuongeza
“Ili kuwaokoa vijana wetu na kupunguza nguvu kazi naviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuongeza nguvu ya mapambano ya madawa ya kulevya” alisema Kwa upande
wake Balozi wa Norway hapa nchini, Hanne-Marie Karstand, amewataka watumishi wa hospitali ya Bombo kulitunza jengo hilo kama ilivyo matumizi yake.
Alisema Serikali ya Norway itaisaidia Tanzania katika Nyanja mbalimbali za kijamii ikiwemo Afya, elimu, Mazingira pamoja na
wagonjwa wa Afya ya  Akili.
“Niuombe uongozi wa hospitali ya Bombo kulitunza jengo hili kwa kutumika matumizi yake
kama ilivyokusudiwa, Norway itaisaidia Tanzania kila ambapo kunahitajika msaada” alisema
Nae Mganga Mkuu wa Mkoa, Asha Mahita, alisema awali wamekuwa wakikumbana na changamoto
mbalimbali ikiwemo kukosa uwezo wa kuwasafirisha wagonjwa kwenda vituovinavyotoa huduma za Afya ya akili.
Aliwataka wafadhili wengine kuiga mfano wa Norway kuisadia hospitali hiyo kutokana na changamoto ambazo imekuwa ikabiliana nazo.
                                                 








Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shighela (katikati), Balozi wa Norway wa kwanza kulia, Hanne-Marie Karstand na Mganga Mkuu wa Mkoa, Asha Mahita (kushoto) wakifungua jengo la Afya
ya Akili hospitali ya Rufaa ya Bombo lililokarabatiwa na kituo cha Tanga International Comperence Centre Tanga




Habari kwa hisani ya blog ya kijamii ya tangakumekucha 0655 902929

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MKUU WA MKOA WA TANGA AKOLEZA VITA YA MADAWA YA KULEVYA
MKUU WA MKOA WA TANGA AKOLEZA VITA YA MADAWA YA KULEVYA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh1svX65_UQlbXmFz4m7g98biP4ZHlsY9pABowilgRi5Arr4yGXLDPT1p6YJq97uN1OOC88myxI5QdcHeO_aa6pz5cZ1StBhb9MkzEr8OqD-7pDmpnb-YO8AkGiVqat6tYLEdXIMZhh3S3C/s640/DSCN8083.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh1svX65_UQlbXmFz4m7g98biP4ZHlsY9pABowilgRi5Arr4yGXLDPT1p6YJq97uN1OOC88myxI5QdcHeO_aa6pz5cZ1StBhb9MkzEr8OqD-7pDmpnb-YO8AkGiVqat6tYLEdXIMZhh3S3C/s72-c/DSCN8083.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/mkuu-wa-mkoa-wa-tanga-akoleza-vita-ya.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/mkuu-wa-mkoa-wa-tanga-akoleza-vita-ya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy