Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama ameiagiza migodi mikubwa ...
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu) Jenista Mhagama ameiagiza migodi mikubwa nchini Tanzania
kuanzisha programu maalum kwa ajili ya kutoa elimu ya afya na usalama
kwa wachimbaji wadogo wa madini ili kuepuka ajali zinazotokea kwenye
maeneo ya migodi.
Waziri
Mhagama ametoa agizo hilo leo Ijumaa Aprili 28,2017 katika viwanja vya
Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro wakati akikagua mabanda
ya maonesho ya migodi mbalimbali nchini ikiwemo inayomilikiwa na
kampuni ya Acacia inayomiliki migodi ya Bulyanhulu,Buzwagi na North
Mara.
“Serikali
imeridhishwa kuhusu namna migodi mikubwa nchini inavyozingatia suala la
usalama na afya mahali pa kazi,migodi hii mikubwa inatakiwa kutengeneza
program maalumu za kufundisha migodi midogo midogo inayowazunguka ili
watanzania wote waweze kujua namna gani wanaweza kuwa salama katika
shughuli za uchimbaji madini”,alisema Mhagama.
“Tumekubaliana mwaka ujao kila mgodi utatoa taarifa namna gani kuwasaidia watanzania kuwa salama katika maeneo ya kazi”,alieleza Mhagama.
Akizungumza
katika mabanda ya Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Acacia
inayomiliki migodi ya Buzwagi,Bulyanhulu na North Mara,Mhagama alieleza
kufurahishwa kuhusu namna kampuni hiyo inavyokusanya na kutumia takwimu
za afya na usalama mgodini.
Waziri Mhagama alikuwa mgeni rasmi katika siku ya Usalama na afya mahali pa kazi duniani kitaifa mkoani Kilimanjaro.
Nimekuwekea
hapa picha za matukio wakati Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama
akitembelea mabanda ya kampuni ya Uchimbaji madini ya Acacia
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu) Jenista Mhagama akiwa katika banda la mgodi wa Bulyanhulu
katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi kwa ajili ya kuangalia
vifaa vya kisasa vinavyotumika katika uokoaji na namna mgodi huo
unavyofanya katika kuhakikisha wafanyakazi wao wanakuwa salama mgodini
Kulia
ni Afisa Uhakiki wa Usalama mgodi wa Bulyanhulu Amina Mohamed
akimweleza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama kuhusu namna
wanavyokusanya takwimu za afya na usalama mgodini
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu) Jenista Mhagama akiangalia vifaa vya kisasa vinavyotumika
katika kutunza takwimu za afya na usalama katika mgodi wa Bulyanhulu
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu) Jenista Mhagama akisisitiza maafisa kutoka mgodi wa Bulyanhulu
kuanzisha programu maalumu ya utoaji elimu ya usalama na afya kwa
wachimbaji wadogo wadogo wa madini
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu) Jenista Mhagama akizungumza na maafisa kutoka mgodi wa
Bulyanhulu
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu) Jenista Mhagama akiangalia kitabu maalumu kinachotumika
kukusanya takwimu za afya na usalama katika mgodi wa Bulyanhulu
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu) Jenista Mhagama akizungumza jambo na Kiongozi wa kitengo cha
afya mgodi wa Bulyanhulu Dkt. Kudra Said (kushoto).Katikati ni Afisa
Mahusiano mgodi wa Bulyanhulu Mary Lupamba
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu) Jenista Mhagama akifurahia jambo na maafisa kutoka mgodi wa
Bulyanhulu
Kulia
ni Kiongozi wa Idara ya Mahusiano ya Jamii mgodi wa North Mara Fatuma
Mssumi akimkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama katika banda la
mgodi wa North Mara
Afisa
Usalama na Afya mgodi wa North Mara Alfred Mwema akielezea kuhusu namna
mgodi huo unavyozingatia masuala ya usalama mgodini.Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu) Jenista Mhagama akizungumza katika banda la mgodi wa
Bulyanhulu
Kulia
ni Dkt. Ludovick Silima kutoka mgodi wa Buzwagi akionesha vifaa vya
uokoaji vinavyotumiwa na mgodi huo wakati Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista
Mhagama alipotembelea banda la mgodi wa Buzwagi
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu) Jenista Mhagama akizungumza katika banda la mgodi wa Buzwagi.
Aliyeshikilia kipaza sauti ni Kaimu Mtendaji kutoka OSHA Hadija Mwenda
Kulia ni Mkufunzi Idara ya Uokoaji Mgodi wa Buzwagi Azael Kitange akionesha takwimu za afya na usalama za mgodi huo
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu) Jenista Mhagama akisikiliza kwa umakini maelezo kutoka kwa
Mkufunzi Idara ya Uokoaji Mgodi wa Buzwagi Azael Kitange.Kushoto ni
Afisa Mawasiliano mgodi wa Buzwagi Magesa Magesa
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu) Jenista Mhagama akiondoka katika mabanda ya kampuni ya Acacia
inayomiliki migodi ya North Mara,Buzwagi na Bulyanhulu.
(Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog)
COMMENTS